CoronaVirus: Uhamiaji Tanzania yawaongezea Wageni muda wa kukaa nchini baada ya kushindwa kusafiri

CoronaVirus: Uhamiaji Tanzania yawaongezea Wageni muda wa kukaa nchini baada ya kushindwa kusafiri

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa #Corona na baadhi ya Wasafiri kushindwa kusafiri kurudi kwao, Tanzania imetoa muda wa nyongeza kwa wageni hao kukaa nchini

Wageni wote waliokuwa wanatarajia kuja na tayari wamepewa ‘Visa Grant Notice’ lakini ameshindwa kusafiri ameongezewa miezi mitatu kutoka muda wa Visa zao ulipoanza

Wageni ambao Pasi zao sa Kusafiria zimeisha muda au zinakaribia kuisha muda na hawawezi kusafiri kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa #COVID19, wanatakiwa kwenda Kituo Kituo chochote cha karibu cha Uhamiaji ili kuongezewa mwezi mmoja wa bure kwenye Pasi zao za kusafiria

Hata hivyo kama hali hii itaendelea baada ya kuisha kwa mwezi mmoja wa nyongeza, Wageni hao watatakiwa kufika katika Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji yaliyopo Kurasini, Dar es Salaam

Kwa wale wenye Kibali cha Ukazi, Pasi ya Kusafiri ya Wageni, ‘Exemption Certificate’ na Dependant Pass ambazo zimeisha muda amepewa mwezi mmoja wa nyongeza kukaa nchini. Lakini muda huo ukikaribia kuisha wanashauriwa kufika Makao Makuu ya Uhamiaji

Aidha, wale wote wenye Kibali au Pasi ya Ukazi ambao tayari wameshakusanya nyaraka zao wanatakiwa kuripoti mara moja Makao Makuu ya Uhamiaji yaliyopo Kurasini Dar es Salaam

304A7955-C106-451B-9165-019204CF8412.jpeg
 
Afadhali uhamiaji wamefikiria hili.
 
Back
Top Bottom