Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
TISHIO la ugonjwa wa Corona limesababisha Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye akabidhiwe kadi ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimya kimya, bila kuwepo shamrashamra zozote kama ilivyozoeleka.
Akizungumza jana katika hafla fupi ya kumkabidhi kadi mwanachama huyo, Katibu Mkuu wa CCM, Dk Ali Bashiru, alisema: “ bila kuwepo na ugonjwa wa corona pangechimbika.”
Amesema CCM imekuwa imekuwa na utaratibu wa kuwa na shughuli na sherehe kubwa kila kinapoongeza mwanachama mpya na kuwa walijipanga kufanya hivyo, lakini kutokana na matatizo ya ugonjwa wa corona, wameshindwa kufanya sherehe ya kumpokea Sumaye.
“Tulishajipanga lakini kutokana na matatizo ya Corona, pangechimbika hapa na tungeitangazia dunia. Hata kama ni mwaka kesho Mungu akijalia hali ya hewa ikatengamaa nakuahidi Mzee Sumaye Mungu akituweka hai sote, tutafanya sherehe kubwa,”alisema.
Alisema sherehe hiyo haijafutwa, bali imesitishwa kutii maelekezo ya serikali ili kulinda afya za wananchi wake.
Akizungumza kuhusu ujio wa Sumaye, alisema: “Mzee Sumaye anapata kadi na kuwa mwanachama, nakukaribisha sana Sumaye, nilikupokea Lumumba kwa niaba ya Kamati Kuu ya CCM na leo nakukabidhi kadi karibu sana nyumbani.”.
Alisema wastaafu bado wapo kazini, na wastaafu wengi wapo CCM na Sumaye ameongeza idadi ya wastaafu ndani ya chama.
Dk Bashiru amesema Dodoma mjini ina idadi kubwa ya wapiga kura kuliko eneo lingine lolote nchini.
“Sasa ni kazi ya Mzee Sumaye kuamua kuhamisha taarifa zake za kupiga kura Dodoma au zibake Manyara, kwenye suala la kura Mtanzania ana hiyari iwe wapi,”alisema.
“Nilimuuliza Mzee Sumaye kwa nini ameamua kuchagua tawi la kujiunga na CCM liwe Mji mpya jijini Dodoma badala ya Hanang nyumbani alikozaliwa, alisema angependa kulinda historia yake, kwa kuwa awali uanachama wake aliupata hapa hapa Dodoma na anatamani kuendeleza historia yake.”
Alisema uanachama wa CCM ni wa utanzania, sio wa eneo la kuzaliwa wala kabila. Alisema CCM ni chama cha watu na ni cha kitaifa.
Sumaye ameshukuru uongozi wa CCM tawi la Mji mpya Kata ya Uhuru,ambao wamemkubali kuwa mwanachama mpya bila kuumizwa au kupewa adhabu kwa kuwa wangememkataa ingekuwa mwisho wa juhudi zake za kurudi ndani ya CCM.
Pia, Sumaye amemshukuru Dk Bashiru kumpa heshima.
HabariLeo