Cosmas Cheka, Issa Nampepeche wapigwa faini na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC)

Cosmas Cheka, Issa Nampepeche wapigwa faini na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC)

Do santos

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2011
Posts
635
Reaction score
338
Kamisheni inayosimamia ngumi za kulipwa Tanzania TPBRC, kupitia makamu wake imewapa adhabu za faini bondia Cosmas Cheka na mwenzie Isa Nampepeche.

Cosmas Cheka amepigwa faini ya Tshs laki nne (400,000/-) na Isa Nampepeche faini ya Tshs Laki Tatu (300,000/-).

Faini zote zilipwe ndani ya mwezi mmoja.

Aidha wamepewa onyo kali kwa sababu ni kosa lao la kwanza.

Bondia Cosmas Cheka alimpiga ngumi bondia mwenzie Isa Nampeche wakati wanafanyiwa mahojiano yaliyokuwa yanarushwa mubashara kwenye Runinga.

Mabondia hao walitarajiwa kupambana lakini ilishindikana baada ya Cosmas Cheka kuumia mkono jambo ambalo Isa Nampeche alipinga kama janja ya Cosmas kumkimbia.

Mara kadhaa mabondia hao mapambano yao yaliahirishwa kwa sababu kadhaa.

Licha ya kukubali msamaha wa Cosmas Cheka, bondia Isa Nampeche hakuridhishwa na faini aliyopigwa kwa sababu hakuna kosa alilofanya zaidi ya yeye ndio aliyopigwa ngumi.
 
Licha ya kukubali msamaha wa Cosmas Cheka, bondia Isa Nampeche hakuridhishwa na faini aliyopigwa kwa sababu hakuna kosa alilofanya zaidi ya yeye ndio aliyopigwa ngumi.[/QUOTE]

Issa alikuwa na maneno ya shombo. Hata mimi ningempa za uso
 
Labda alimtolea lugha ya matusi ndo maana nae amehukumiwa.
Labda baada ya mapigano ya kurushiana ngumi lakini wakati wakihojiwa na mwandishi ni maneno ya vijembe tu wala hapakua na matusi.
 
Kama vipi Cosmas Cheka apumzike tu kwa muda kupambana ulingoni, au astaafu kabisa masumbwi.

Anaupenda sana mchezo wa boxing, lakina kwa bahati mbaya mwili umechoka.
Huyu Cosmas ni mdogo wa Frances Cheka.Cosmas bado yuko vizuri
 
Back
Top Bottom