Cosmas Cheka na Issa Nampekeche waamua kuzichapa "Kavu Kavu"

Cosmas Cheka na Issa Nampekeche waamua kuzichapa "Kavu Kavu"

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
Kwema wakuu?

Hawa wawili ilikua wazichape Leo ukumbi wa PTA, pambano limeshindikana sababu Cheka anasema kapata ajali, amekuja na "hogo" mkono wa kushoto wakati anahojiwa na Mtangazaji Ahmed Ally wa Azam TV.

Issa Nampekeche anasema Cosmas hajapata ajali popote, ka fake ajali ili amkimbie. Cosmas anasema Issa analazimisha wapigane ili apate jina, apate hela.

Wametupiana maneno mwisho wakaamua kurushiana ngumi hapo hapo mbele ya Mtangazaji kabla ya kuamuliwa.
 
Video niliyoiona mimi sikuona wakirushiana ngumi ila Cheka kampiga ngumi Issa akiwa anaongea kwenye mic
 
Cosmas alipaniki mpaka karusha ngumi
Uncivilized kabisa, kasema amepata ajali alafu anarusha ngumi mbele ya mahojiano ya kawaida kabisa, je Nampekeche angemuumiza mkono wenye majeraha lawama zingerudi kwa nani
 
Sasa Cheka kama ameweza kurusha ngumi akiwa kwenye majeraha si wangelitenga kabisa tukajua moja,angeona Issa angempiga ngumi za kiufundi na zenye vipimo.
 
Huyo Cosmas si ndio alipiga mabusu mwenzake jana!!
Cosmas alipaniki mpaka karusha ngumi
Uncivilized kabisa, kasema amepata ajali alafu anarusha ngumi mbele ya mahojiano ya kawaida kabisa, je Nampekeche angemuumiza mkono wenye majeraha lawama zingerudi kwa nani
Anapaswa kufungiwA huyo maana hana maadili ya kabisa kama bondia.
 
Cosmas alipaniki mpaka karusha ngumi
Uncivilized kabisa, kasema amepata ajali alafu anarusha ngumi mbele ya mahojiano ya kawaida kabisa, je Nampekeche angemuumiza mkono wenye majeraha lawama zingerudi kwa nani
Yeah,
Alipaniki aisee. Pengine hata ni kweli ali fake ajali.
 
Back
Top Bottom