The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) imeteketeza vifaa na bidhaa vilivyokamatwa kwenye operesheni ya kutokomeza uharamia nchini dhidi ya kazi za sanaa na fasihi pamoja na usambazaji wa matangazo ya televisheni kinyume na sheria
zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Tsh Milioni 75 amesema Mkurugenzi wa taasisi hiyo Doreen Sinare, ambaye amebainisha kwamba madhara ambayo yangesababishwa na vifaa hivyo ni makubwa kuliko thamani yake.
Soma pia: Waziri Dkt. Ndumbaro aipongeza COSOTA na kuipa maagizo
Vifaa hivyo vilivyokamatwa na COSOTA vimekusanywa kutoka maeneo mbali mbali ambayo operesheni hiyo ilikuwa inaendelea ikiwemo mikoa ya Dar Es Salaam, Arusha, Mwanza, Lindi, Mtwara, Pwani, Shinyanga, Dodoma, Kagera na mingeneyo.
“COSOTA imejipanga kuhakikisha kwamba wale wanaojihusisha na vitendo hivi wanakamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa mujibu wa sheria” amesisitiza Mkurugenzi wa taasisi hiyo