Cost comparison SGR Kenya vs SGR Tanzania

Mpaka hapa nadhani imeonekana wazi.. Kwenye hii game ya reli, Tanzania imeiaibisha Kenya pakubwa sana...

Kuna issues ambazo majirani hawataki ziongelewe kabisa...
1. Large, empty, and expensive to maintain railway stations.
2. The cost of running diesel trains.
3. Chinese loan, and the fact that Chinese are the ones operating the railway (shame).
4. The Naivasha ICD saga (this shows majirani mlikuwa hamjajipanga kabisa hiyo reli yenu ilikuwa inaenda wapi na kufanya nini)

BTW nishawahi kusema humu, kama nchi yako haina reli ya umeme usiwe mwepesi wa ku comment..
 

Ngoja nikusaidie kujibu..

1. Reli itakwenda Bandarini, maana hiyo ndo main plan, hawawezi kujenga ICDs huko kwenye njia ya SGR ikiwa hawana plan ya kuifikisha Bandarini. For now reli inajengwa mpaka Dodoma.. na tenda ya kuelekea Isaka inatangazwa soon, demand ya mizigo ipo kubwa huko kwa majirani, by the time Reli imefika Isaka na Mwanza, tayari itakuwa imesha connect Bandarini. Halafu the fact that the rail is less than a Kilometre from the port.

2. Nenda dunia nzima na uniambie Railway stations huwa zinakaa nje ya mji au ndani ya mji.. hakuna mjinga ataweka station nje ya mji kwa kuwa katikati ya mji ndio mahali rahisi kufikiwa na kila aina ya usafiri (na ndio maana stand ya bus ilikuwa ipo Kisutu), so kuweka station pale ni sawa kabisa ukizingatia eneo la Gerezani-posta ni transport hub ya jiji. Dodoma na Morogoro siyo miji mikubwa na ndio maana wakaweka Stations nje ya mji ili ku encourage mji kusogea.

Ikulu ya Dar imeshahamwa, Dar is no longer a Political City, hakuna umuhimu wa kuogopa kuweka miundombinu kama hiyo katikati ya Jiji.

3. Hakuna mtu alitaka mradi uchelewe, lakini suala la hali ya hewa ndilo lilichongangia, msimu wa mvua ulikuwa mrefu sana (October-April) sasa hapo sioni unalalamika nini maana hamna mwenye control ya mvua inyeshe lini au isinyeshe lini.

4. Bado tunaihitaji reli ya mjerumani maana inafika maeneo ambayo SGR haijafika, SGR haijakamilika bado, je tuache kukarabati reli ya zamani kwa kuwa tunajenga reli inayokamilika miaka 7 inayokuja? Hilo halihitaji hata mtu uwe na akili kubwa sana kuelewa.

Kama unahisi walikurupuka basi tuambie what could be the best way ku-execute SGR...
 
Reli inafika bandarini kwenye hii project ya phase I hii ya mpaka reli ya Isaka ianze kujengwa si kweli! Ujenzi wa Overpass Gerezani ukiisha nayo route ya Bandarini hii itaanza kumbuka kunahitajika underpass ya MGR pale keko ipanuliwe hii ina maana Nyerere road itafungwa kwa muda na diversion ya kwenda City center itakuwa chang'ombe-Jitegemee-BP-Reli Gerezani! Kumbuka pia kuna BRT Chang'ombe overpass nayo inaanza soon! Pia Bandarini kwenyewe kuna ujenzi wa berths!
 
Lakini pia tuulize maswali juu ya reli ya Tanzania
1. Stesheni ya Nairobi na Mombasa are the large ones and they were full to capacity. Wasafiri wa sgr tanzania watakaa nje kwa nyasi juu stesheni zenu ndogo hazina waiting area.
2. Je , Mtabeba cargo yote kutoka Dar kwenye reli na kumaliza kazi za wenye ma lorry pia dar? Au mtasema wacha market forces? Kumbuka Kenya ina uhuru ya kutumia market forces kushinda Tz enye Magu hatakubali project yake ikose containers? Noise from lorry drivers will be muzzled out sio kama Kenya tumewacha wapige kelele
3. Cost of running diesel trains.. manjua aje electric itakua cheaper? utafiti iko wapi na reli ya Tz haija anza kazi. Mta ambiwa kweli ikipata losses na serekali siri? Reli ya Ethiopia na pata faida juu inatumia stima?
4. Chinese loan ilikua na better terms kushinda bank loans zile hamja ambiwa details. Commercial loans always more expensive.
5. Shida ya Naivasha ICD ni transporters need to add it as port of receiving for insurance purposes and where work of the shipper ends to the customer. With time shippers will align in the process and didn't like being caught off guard, Nairobi ICD had same toothing problems but is doing very well now. Mai mahiu road is a major traffi headache to transporters, now logistics providers can avoid it.

Na
Reli ya Tanzania will be more expensive than Kenya because it longer and serves smaller countries, Rwanda and Burundi, mki fika Rwanda reli ita gharamia $15b, $5b more than Kenya will take to finish at Malaba, a bigger economy. Na loans za za Tz ni commercial and more expensive. Je, mlijenga reli kushindana na Kenya tuu?
 
SGR Station ya Dar ni 13,000 sq m vs 15,000 sq m Nairobi, sasa unapodai stesheni zetu ni ndogo unamaanisha nini wakati Dar city alone ina stations mbili moja city center na nyingine Pugu! Hamnaga akili nyie na ubishi wenu wa Kifalamanga? Hivi mnafikiri abiria wa JNIA ataenda city center kuifuata SGR kweli? wa Mbezi Luis bus terminal pia? Hawa wataenda Pugu na plan ni kuunganishwa JNIA, Pugu station na Mbezi bus Terminal pia! BTW Station ya Dodoma will be bigger than all SGR stations in EA at over 15000 sq m! Sasa unapata wapi idea ya kuwa SGR stations za Tanzania ndogo wakati za majiji zinalingana na za Kenya?

 
Nikujibu mawili tu. Dsm station haihitaji kuwa kubwa kama Nairobi au Mombasa. Na hata ststions nyingine pia. Sababu ni kuwa trains zetu zitakuwa na frequency kubwa hivyo zitabeba watu wachache wachache. Tofauti na "long trains" zenu zenye abiria kama wote. Hivyo hapana abiria kukaa nje.

Kuhusu cost ya umeme hata ikiwa kubwa (siyo kubwa anyway) bado iko economically justifiable as watalipwa Tanesco (no leakages).
 
Hapo kwenye TANESCO ni sawa na kuchukua pesa mfuko wa kushoto na kuhamishia mfuko wa kulia [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Hapo kwenye TANESCO ni sawa na kuchukua pesa mfuko wa kushoto na kuhamishia mfuko wa kulia [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Ndiyo hivyo. Sisi ni net importers wa mafuta. Hivyo kutumia diesel kunamaanisha kupunguza akiba ya fedha za kigeni ambazo ndiyo chachu ya ukuaji wa uchumi (new capital for investment). Hapo ndipo huwa najigamba kuwa na rais jembe.
 
Ndiyo hivyo. Sisi ni net exporters wa mafuta. Hivyo kutumia diesel kunamaanisha kupunguza akiba ya fedha za kigeni ambazo ndiyo chachu ya ukuaji wa uchumi (new capital for investment). Hapo ndipo huwa najigamba kuwa na rais jembe.
net exporter au net importer?
 

@Ezz chezzale juu na wengine wengi, wewe Giza ukiwa mbele ukisema hapa Kenya tunajenga steni kubwa za bure, sasa una ringa mnajenga stesheni kubwa EA mzima.. Kenya iki jenga kubwa ni shida, Tz ikijenga kubwa zaidi ni nzuri?!
 

Uko na hakika kweli? Wapi proposed timetime table? The railway design says the opposite. Longer and fewer crossing stations means you will run long trains with more people and at less frequency. Au unadhani single track terni hazitangojeana in the few stations? Nangoja reli imalizwe tuone hizi theory
 
@Ezz chezzale juu na wengine wengi, wewe Giza ukiwa mbele ukisema hapa Kenya tunajenga steni kubwa za bure, sasa una ringa mnajenga stesheni kubwa EA mzima.. Kenya iki jenga kubwa ni shida, Tz ikijenga kubwa zaidi ni nzuri?!

Napata shida kukujibu kwa kuwa huwezi kuandika Kiswahili vizuri. Jitahidi basi kutumia lugha ya malkia.. 🙂
 
We jamaa acha kutumia kijaluo, humu ndani lugha ni mbili tu either utumie kiswahili au English
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…