Ndio..SGR!?
Lakini bado Dar-is-a-scam ndio jiji kubwa danganyika na ndio port kubwa danganyika na bado Mombasa inaipiga kwa ukubwa wa port.ulitegemea bandari iwe Nairobi,,
Dar siyo jiji kuu,kwa Tanzania Dodoma ndiyo jiji kuu,tulishatoka huko,Dar ni jiji la biashara kama unavyoona U.S.A kwa New york city na Washngton DC
we kweli kibaka
Jiji lolote lisilo na miundombinu ya BRT, electrified SGR au modern flyovers like 3level interchange basi hilo jiji liko stone age.Lakini bado Dar-is-a-scam ndio jiji kubwa danganyika na ndio port kubwa danganyika na bado Mombasa inaipiga kwa ukubwa wa port.
Mombasa port is bigger and better than dar-is-a-scam portJiji lolote lisilo na miundombinu ya BRT, electrified SGR au modern flyovers like 3level interchange basi hilo jiji liko stone age.
Tuongezee modern airport na bus terminal itapendeza zaidi [emoji23][emoji23][emoji23]Jiji lolote lisilo na miundombinu ya BRT, electrified SGR au modern flyovers like 3level interchange basi hilo jiji liko stone age.
sehemu ilipo bandari ya Dar ni sehemu ambayo ni ndogo tofauti na Mombasa hiyo ni moja ya changamoto la kieneo ambayo tunayo kiasi cha kwamba miaka mingi ijayo italeta shida na ndiyo maana tupo kwenye hatua za kutaka kujenga bagamoyo port ambayo itateka kila kitu ni muda tu unahitajika.Lakini bado Dar-is-a-scam ndio jiji kubwa danganyika na ndio port kubwa danganyika na bado Mombasa inaipiga kwa ukubwa wa port.
So Mombasa port is bigger than dar port and Mombasa is smaller than dar. LEVELS.sehemu ilipo bandari ya Dar ni sehemu ambayo ni ndogo tofauti na Mombasa hiyo ni moja ya changamoto la kieneo ambayo tunayo kiasi cha kwamba miaka mingi ijayo italeta shida na ndiyo maana tupo kwenye hatua za kutaka kujenga bagamoyo port ambayo itateka kila kitu ni muda tu unahitajika.
Ndio mana tunaitaji kuendelea na yarp maerkez kwanza kazi yao ni bora na inaufwnisi ukiachia kuchelew...hawa wachina ni wahuni sanaHivi kuna ukweli gani?[emoji116][emoji116]
Top Menu

Gazeti la Jamhuri
Tunaanzia wanapoishia wengine
Walivyojipanga kuihujumu SGRJamhuri September 29, 2021Walivyojipanga kuihujumu SGR2021-09-29T07:22:56+00:00
*Waibua hoja zilizokufa wakati wa Rais Magufuli, masilahi binafsi yatangulia
*Mawaziri, makatibu wakuu wameelewa, watendaji wapingana na sheria ya ununuzi
*Mkono wa Kenya watajwa katika vita ya biashara ya reli kubeba mizigo ya majirani
*Yadaiwa kuna kampuni zimejipanga kushinda zabuni zikwamishe ujenzi Tanzania
Na Mwandishi Wetu
Baada ya wiki iliyopita kuchapisha habari za jinsi baadhi ya wanasiasa na watendaji walivyojipanga kuhujumu ujenzi wa reli ya kisasa katika kipande cha 3 & 4 cha kutoka Makutupora – Tabora – Isaka, sasa ni rasmi yameibuka makundi yanayoonyesha sura halisi ya kile yanachokipigania kuwa ni kuhujumu ujenzi wa reli ya SGR, uchunguzi wa JAMHURI umebaini.
Makundi haya yamekuwa na mjadala mzito katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari, yakisisitiza kifuatwe kifungu cha 64(1) cha Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2011 na Kanuni ya 149(1) ya Mwaka 2013 ya sheria hiyo, ambavyo kwa pamoja vinataka kutangaza zabuni kupewe “kipaumbele” katika miradi ya kitaifa. Wenye taarifa za ndani wanasema kundi hili linatumia kifungu hiki kwa masilahi binafsi.
Hata hivyo, hawataki kutumia Kanuni ya 161(c) ambayo inasema bayana kuwa inaruhusu kuwapo mzabuni mmoja iwapo faida za kutumia mzabuni mmoja (single sourcing) ni kubwa kuliko kuitisha zabuni.
“Sababu za msingi zipo na zisizotiliwa shaka. Mwanzo tulikuwa tunapata taarifa tunaziona si za msingi, kumbe hawa watu wamejipanga. Hawakuthubutu kuyafanya haya wakati wa Rais [John] Magufuli, sasa amefariki dunia wanataka kurejesha mwendo wa kuruka kupiga fedha ndefu, hili halikubaliki,” amesema mtoa habari wetu.
Ukiacha hilo, Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma (PPRA) katika barua kadhaa ilizowasiliana na Shirika la Reli Tanzania (TRC) inaungana na Bodi ya Zabuni ya TRC kupingana na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa, anayependekeza kuwa kwa masilahi mapana ya taifa kipande cha 3 & 4, kitumie utaratibu wa kumpa kazi mzabuni mmoja.
“Hapa utaona Kadogosa yuko sahihi. Mwaka 2016 ilitangazwa zabuni ya Lot 1, zikaomba kampuni 40. Ilipofika muda wa kurejesha zabuni ilirudisha kampuni moja tu ya Yapi Merkezi kama mlivyoandika wiki iliyopita. Kampuni hizi zote ambazo hazikurudisha zilikuwa za China. Tulipata mawasiliano na mazungumzo yao, walikubaliana wasirudishe zabuni nchi yetu itikisike, twende kuwabembeleza waje kutujengea reli.
“Ukumbuke walifanya hivyo, baada ya awali kuleta benki ya kwao ikasema ingelikopesha taifa letu Sh trilioni 7.6 kwa ajili ya ujenzi wa reli (Julai 20, 2016). Kampuni za kwao zilipojitoa, hii benki nayo ikajitoa katika kutukopesha. Lot 2, nayo walifanya hivyo hivyo. Ziliomba kampuni 27, kampuni 26 kutoka China zikajitoa, tukabaki na Yapi Merkezi. Rais Magufuli akasema waache, hatutishiki, ipo siku watatamani kuja kujenga hapa kwetu.
“Lot ya 3 zilijitokeza kampuni 7. Kampuni 5 kutoka China hazikurejesha zabuni. Rais Magufuli alikuwa amesema hata hawa CCECC/CRCC JV tusiwape wanaweza kuwa wameweka bei ya chini kuwatisha Yapi Merkezi, maana bei si kigezo pekee cha kushinda zabuni. Inaangaliwa na uwezo wa kampuni kifedha na mambo mengine yakiwamo ya ubora wa kazi na usalama wa nchi. Mjadala ulikuwa mkali, ila mwisho akasema basi tuwape tuwajaribu. Tumemaliza miezi 9 sasa kwenye mkataba na hizi kampuni, hawajafikia hata asilimia 10 ya kazi waliyopewa.
“Mwaka 2015 mtakumbuka kampuni moja kutoka China iliingia mkataba wa kimagumashi na Tanzania kuwa ingejenga reli kwa kilomita moja dola milioni 6.2 sawa na Sh bilioni 14.26. Reli yenyewe ilikuwa spidi 80 na ni analogue. Walioingia mkataba huo wako mahakamani hadi sasa. Januari, 2021 kampuni moja kutoka China ilishusha bei na kusema itajenga kwa wastani wa dola milioni 3.9 kwa kilomita moja ya reli, karibu Sh bilioni 8.9. Ikapewa. Wasichojua wananchi ni siri kubwa.
“Kampuni hiyo hiyo inayojenga kwa dola milioni 3.9 kwa kilomita, katika mazungumzo mapya inataka kujenga kilomita moja kwa dola milioni 6.5 sawa na Sh bilioni 15.95 kwa Lot 3 na 5. Imeleta bei zilizopakwa rangi za dola milioni 5.7 sawa na Sh bilioni 13.11, lakini katika gharama hizo hakuna VAT 18%, hakuna gharama za kujenga vituo kama Tabora, hakuna gharama za mafunzo, gharama za maeneo ya kuteketeza taka na mambo mengine mengi.
“Lakini mbaya zaidi, tuna uzoefu sasa. Kampuni nyingi za China zinaleta bei ndogo wakati wa kuleta zabuni. Mkiisha kumpa zabuni anaanza kazi, kisha anaanza kuleta gharama mpya nyingi tu wanazoziita variation (tofauti ya gharama halisi na zilizopo kwenye mkataba).
Nenda Busisi (daraja la Kigongo), Ubungo Interchange, angalia mikataba mbalimbali ya barabara jinsi wanavyojenga na kuleta variation cost kubwa.
“Unakuta mkataba ni Sh bilioni 20 kwa mfano, lakini hadi mnamaliza mnajikuta mmemlipa Sh bilioni 45. Unajiuliza, ilikuwa na faida gani kumkatalia aliyekuwa wa pili akiwa na gharama ya Sh bilioni 30, tukampa huyu wa Sh bilioni 20 ambaye tumeishia kumlipa Sh bilioni 45? Tumejifunza kwa njia ngumu. Tunao wataalamu wetu wenye ujuzi wa hali ya juu katika negotiation (majadiliano) tuainishe gharama halisi, tuzipe kampuni zenye uwezo na miradi ijengwe na kuisha kwa wakati,” kimesema chanzo chetu.
Alipoulizwa juu ya hoja iliyotolewa na PPRA kupitia barua ya kwenda kwa TRC kuwa mchakato wa zabuni umesaidia nchi kuokoa dola 1,030,068,831.21 sawa na Sh trilioni 2.37 kwa kuipa zabuni Kampuni ya CCECC/CRCC JV, akasema:
“Wewe tafuta hizo Lot 3 na 4 wanataka kuzijenga kwa shilingi ngapi. Si wamewasilisha maombi wote? Wewe uliza tu. Yapi wamekuwa wanajenga kwa dola milioni 4.07 sawa na Sh bilioni 9.36, uliza hawa wanataka kujenga kwa shilingi ngapi? Wasiwasi uliokuwapo juu ya kushusha bei wakati wanapewa hii zabuni, tayari umedhihirika. Hili la bei tumekwisha kuwafahamu, tunasubiri la kutokamilisha ujenzi kama nalo lipo. Niulize swali hili ukiisha mwaka mmoja tangu wamepewa mradi,” amesema.
Mmoja wa mawaziri anayelifahamu vizuri suala hili ameliambia JAMHURI: “Kwanza tunapaswa kufahamu nani anayetaka kutukopesha fedha za ujenzi huu. Si unaona? Kuwait wakitoa fedha za maji kama ule mradi wa maji Moshi, wanazipa zabuni kampuni zao. India nao vile vile. China ndiyo usiseme. Japan utaona JICA ndiyo wanaojenga, kwa hiyo sitashangaa tukipata mkopeshaji kutoka China, japo tuombe yasitukute yaliyowakuta Wakenya, kwa hakika itajenga kampuni ya Kichina. Fedha zikitoka Ulaya, basi hakika ujue hata mjenzi atatoka Ulaya. Hili ni la kawaida tu.
“Hizi fedha zinazokuja kama mikopo kwa njia ya misaada zinalindwa na kifungu cha 4(1)(b) cha Sheria ya Ununuzi wa Umma kinachosema mtoa msaada asikilizwe kwanza anataka nani ajenge. Achana na hizo hadithi kuwa tunajenga kwa hela zetu. Ni fedha zetu ndiyo, ila kwa njia ya mkopo. Mkopo wenyewe unakuja kama msaada, hivyo tutalipa baada ya kujenga. Sasa akikwambia mtu ni fedha zetu, mwambie ndiyo. Ila muulize tunazo kwenye akaunti? Akikujibu, unipigie simu.”
Chanzo kingine cha uhakika kimeliambia JAMHURI kuwa katika ngazi ya mawaziri na makatibu wakuu wamelizungumza suala hili na wakakubaliana fedha zitatoka wapi na kwa nini ipewe kampuni iliyosimama pamoja na nchi wakati nyingine zimeisusa Tanzania.
“Wewe fikiria zimeomba kampuni 40, 39 zote kutoka China zikajitoa. Yapi Merkezi, akabaki. Zikafanya hivyo Lot 2 na Lot 5 nayo ni kama zilijitoa zikaiacha moja ‘kutest zali’.
“Leo zimepata wapi ghafla mapenzi ya kuja kutujengea reli? Ile benki iliyogoma kutoa hela, imebadili msimamo? Si tutawapa zabuni watuache solemba? Tupambane tumalize reli hii ifike Mwanza kwanza, kama ni reli za kujenga nchi hii ndipo imeanza. Kuna ya Tabora – Kigoma, Mtwara – Mangaka, Rukwa – Tunduma – Ruvuma – Lindi – Dar es Salaam. Tutajenga Tanga – Kilimanjaro – Arusha hadi Musoma. Hii yote ni miradi.
“Lakini jambo jingine, nadhani umeusikia mgogoro wa Ufaransa na mataifa ya Marekani na Uingereza katika mkataba wa ujenzi wa nyambizi (submarine) zenye thamani ya dola bilioni 66 sawa na Sh trilioni 151.8 za Tanzania. Mkataba huu walianza kuzungumza kwa siri mwaka 2016, miaka 5 baadaye ukawaponyoka. Hukusikia mamlaka zao za ununuzi zikipiga kelele. Zinaungana na serikali zao kwa masilahi mapana ya taifa. Tulifanya hivyo katika bomba la mafuta ghafi la Hoima, Uganda hadi Tanga.
“Kuna mambo tunapaswa kukomaa kama nchi. Yapi Merkezi sisemi wapewe kama wana bei kubwa, lakini uhalisia wana vifaa vyote, wamekaribia kumaliza lot 1 & 2 za mwanzo, na kwa uzoefu mchakato wa mkataba wa ununuzi unachukua si chini ya mwaka mmoja kuukamilisha. Badala ya kuingia nao mkataba Novemba au Desemba, mwaka huu wakaanza kazi hii itakayochukua miezi 48, tunataka kuingizana kwenye nyimbo za PPRA.
“PPRA wafahamu kuwa hawapo kusimamia baadhi ya vifungu vya sheria na kanuni, huku wakivipuuza baadhi ya vifungu visivyotimiza matakwa yao. Sheria inaruhusu njia zote mbili. Kuitisha zabuni ukashindanisha wazabuni au kutafuta mzabuni mmoja (single sourcing) mwenye sifa, uzoefu na gharama halisi.
“Mimi nadhani mawaziri wanaosimamia hizi mamlaka watazungumza na watendaji wao, wasiyumbishe nchini. Vifungu vyote vya Sheria na Kanuni vina nguvu sawa. Tumetangaza huko nyuma yaliyotukuta tumeyaeleza. Leo tunataka tutangaze tena waombe, baadaye wajitoe, kisha tuwabembeleze, muda unakwenda tu! Hapana. Tuitendee haki nchi yetu,” amesema waziri mwandamizi.
Kuna taarifa kuwa kampuni nyingi za China zinajitoa katika mchakato mara zote ili kulinda masilahi yao nchini Kenya.
Wakati wanajenga reli ya kutoka Mombasa hadi Nairobi, walilenga reli hiyo iende hadi Uganda, Rwanda na Burundi, hivyo mpango wao wa biashara ulilenga wapate faida kwa njia hiyo. Kitendo cha Tanzania kuanza kujenga reli ya kisasa kinaelekea kuvuruga mpango wa biashara wa Kenya, hivyo kuifanya reli ya Tanzania kuwa na mzigo mwingi kuliko ya Kenya.
Ukiacha eneo la kijiografia la Tanzania, reli inayojengwa Tanzania ni ya umeme ikilinganishwa na ya Kenya inayotumia dizeli. Uwezo wa reli hii ya Tanzania kubeba mizigo ni ekseli ya tani 35 wakati Kenya ni ekseli ya tani 25.
Kwa maana hiyo, reli ya SGR inayojengwa Tanzania ina uwezo wa kubeba mzigo mkubwa kuliko ya Kenya. Kwa kasi pia nako kuna tofauti. SGR ya Kenya inakwenda kilomita 80 kwa saa, wakati ya Tanzania inakwenda kilomita 160 kwa saa kwa treni za abiria.
JAMHURI linaendelea kufuatilia kwa karibu mchakato wa ujenzi wa SRG na litaendelea kuleta taarifa za kila hatua inayopigwa hadi ujenzi utakapokamilika
Ndio mana tunaitaji kuendelea na yarp maerkez kwanza kazi yao ni bora na inaufwnisi ukiachia kuchelew...hawa wachina ni wahuni sana
Gazeti linaloandika "continue welding" badala ya "continuous welding" liache utaratibu wa kupata kandarasi kisheria ufanyike! hao Yapi Merkezi walikosa lot5 kwa vile walitaja gharama za ajabu! Si wasafi vilevile!Mama akivuka hiki kiuzi,ntamwamini
Top Menu

Gazeti la Jamhuri
Tunaanzia wanapoishia wengine
Mafisadi wajipangaJamhuri September 21, 2021 Mafisadi wajipanga2021-09-21T09:57:59+00:00Gazeti Letu, Habari za Kimataifa, page za ndani
*Ni vigogo wazito serikalini, waanza figisu ujenzi wa reli ya SGR
*Washirikiana na wazabuni wa nje kuhujumu ‘Lot 3’ na ‘Lot 4’
*Waanzisha kundi wakijiita wazalendo, latajwa ni fedha mbele
*Kenya walipigwa bilioni 18.4 kila kilomita, wailengesha Tanzania
DODOMA
Na Mwandishi Wetu
Sikio la kufa halisikii dawa. Hili ndilo linaloweza kusemwa kutokana na baadhi ya wanasiasa na watendaji serikalini kuanza mpango wa hatari wa kukwamisha ujenzi wa Reli ya Kati ya SGR; JAMHURI limebaini.
Mpango huo unaosukwa kwa umakini mkubwa, una malengo mawili. Kwanza, kujipatia fedha kwa njia yoyote ile na pili ni kuihujumu Serikali ya Awamu ya Sita kuonyesha kuwa haiwezi kusimamia ujenzi wa reli kama ilivyokuwa awali.
Hivi karibuni kumekuwapo taarifa inayosambazwa na watu wanaojiita ‘wazalendo’ ikitoa shutuma za kuhusu mchakato wa ununuzi unaoendelea vipande viwili; ‘Lot 3’ na ‘Lot 4’, wakitaka utumike utaratibu uliokwamisha ujenzi wa reli tangu enzi za uhuru.
Kuna mgogoro mkubwa unapikwa chini kwa chini na baadhi ya wanasiasa na wataalamu wakitaka vipande viwili vya reli vya kutoka Makutupora hadi Tabora (Lot 3) na Makutupora hadi Isaka (Lot 4) zabuni itangazwe tena, waingize kampuni zao.
Tayari kuna kampuni kadhaa kutoka China ambazo zimewasilisha serikalini nia ya kujenga vipande hivyo na bei wanayotaka kutoza hata kabla zabuni haijatangazwa.
Mbaya zaidi, moja ya kampuni zilizoomba mwaka 2015, iliomba kujenga reli yote kwa gharama ya dola milioni 6.2 kwa kila kilomita, sawa na Sh bilioni 14.26 kwa kilomita.
Kwa urefu wa reli unaojengwa wa kilomita 1,063 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, mkandarasi huyu alitaka alipwe dola za Marekani bilioni 6.59, sawa na Sh trilioni 15.2 za Tanzania.
Ukiacha ughali wa gharama, uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa mkandarasi huyu na wengine walikuwa na upungufu mkubwa uliomsukuma hayati Rais Dk. John Magufuli kuwakataa.
“Muhimu Watanzania wakajua hili group (kundi) la wanaojiita wazalendo ni kina nani. Kwa kudokeza tu hili ni group la watu ambao wanatetea masilahi binafsi, hasa kwa sababu tayari walishakula huko nyuma na wanataka ‘ku-retire imprest’,” anasema Ofisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha na kuongeza:
“Huu ni mlolongo wa matukio. Mwaka 2016 serikali ilipoanza hatua za ujenzi, kampuni pekee iliyojitokeza kuunga mkono serikali ilikuwa Kampuni ya Yapi Merkezi. Katika hatua za awali zilijitokeza kampuni 40, lakini wakati wa kurudisha zabuni kampuni 39 kutoka China zote zilijitoa. Cha kusikitisha hata benki moja ya China iliyokuwa imeahidi kutoa fedha, ilikataa ikitoa sababu zisizokubalika.
“Kwanza, benki hiyo ilisema Tanzania imeamua kujenga reli kufuata ‘standards’ (viwango) za kimataifa, yaani kwa kufuata AREMA Standard. Wao hawakulifurahia hili kwa sababu walitaka kufuata standard za Kichina, ikiwa na maana vitu vyote viwe vya Kichina. Kama kuna mtu haelewi tunachozungumza, waulize majirani zetu Kenya. Walifanyiwa mchezo huu.
“Pili, hawakutaka Tanzania ijenge reli kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano ya kisasa, yaani ‘European Level 2 (digital)’, ambayo ndiyo inayotumiwa duniani kote. Walitaka kutuletea teknolojia ya zamani (analogy) kama ya Kenya.
“Tatu, hawakutaka kutumia upembuzi yakinifu wa kwetu. Walitaka wafanye upembuzi wao mpya, na watwambie wanatujengea kwa bei gani. Walitaka makandarasi wote watoke kwao, ‘consultant’ wa mradi wa kwao, ‘design’ Mchina, ‘insurer’ wao na pengine mwishoni kuwa na masharti ya kuendesha wao kama walivyowafanyia majirani zetu. Na hili halikukubalika, na halikubaliki serikalini Tanzania.
“Nne, hawakupenda kubadilishwa kwa mipango yao ya kushirikiana na mafisadi wachache kufuja fedha za walipa kodi waliopanga kufanya na watu wao ambao ndio wanaohaha kila mahala kuihujumu serikali iliyopo madarakani. Mipango haikuwa yenye heri kwa taifa. Kwanza, reli iliyokuwa ijengwe Tanzania ilikuwa kama ile ya Kenya ambayo ni ‘Second hand railway with old technology’, ambayo duniani haitumiki tena,” anasema mtoa habari wetu.
Mtaalamu huyo anatofautisha reli waliyotaka kujenga makandarasi hao na hii iliyojengwa sasa na Yapi Merkezi kwa kusema: “Kwanza, reli yetu ina uwezo mkubwa sana, kwa maana ya kubeba mzigo mkubwa ekseli 35. Reli nyingi zilizojengwa Afrika zina ekseli 25. Ni reli ambazo haziwezi kuchukua mizigo mizito, hasa kwa mtindo wa ‘double stack’.
“Ukitaka kubadilisha reli ya ekseli 25 kwenda ekseli 35, hii pekee itaongeza bajeti kati ya asilimia 15-17.5 ya jumla ya gharama yote ya ujenzi wa reli.
“Pili, reli inayojengwa Tanzania inatumia teknolojia ya kisasa ‘digital’ (European Train Control System Level) ikilinganishwa na analojia inayotembea kasi ya kilomita 80 kwa saa hapo kwa jirani zetu. Kubadilisha mfumo kutoka ‘analogy’ kwenda ‘digital’ unahitaji kutumia asilimia 7 hadi 7.5 ya jumla ya bajeti ya ujenzi wa reli ya kisasa. Na ujue kwamba unapozungumzia teknolojia kwenye reli, unazungumzia mawasiliano (signaling na telecommunications).
“Tatu, reli inayojengwa Tanzania inafanyiwa kitu kinachoitwa ‘continue welding’. Maungio ya reli yamechomelewa kwa teknolojia ya hali ya juu sana. Kubadilisha reli kuipeleka kwenye ‘continue welding’ bajeti inaongezeka kwa asilimia tano ya bajeti ya ujenzi wa reli.
“Nne, reli inayojengwa Tanzania ni ‘electrified line’ (ya umeme). Reli itatumia umeme badala ya dizeli, lakini pia itaweza kupitisha treni za dizeli ukilinganisha na walizotaka kujenga za injini za dizeli pekee.
“Mambo mawili muhimu; kwanza, treni ya umeme ni rahisi mara tatu kuliko treni ya dizeli. Ukitaka kubadilisha treni ya dizeli uweke miundombinu ya umeme inabidi utumie asilimia 25 ya gharama yote ya ujenzi wa reli.
“Tano, reli inayoijenga Tanzania ina kasi ya kilomita 160 kwa saa ikilinganishwa na hiyo waliyotaka kutujengea ya kilomita 80 kwa saa waliyojenga Kenya. Kubadilisha kasi ya kilomita 80 kwa saa kwenda kilomita 160 kwa saa, itahitaji kutumia bajeti isiyo chini ya asilimia 15 ya gharama zilizotumika kujenga reli yote,” anasema.
Anaongeza kuwa iwapo Kenya wangependa kujenga reli sawa na ya Tanzania katika hiyo gharama ya dola za Marekani milioni 6.2, sawa na Sh bilioni 14.26 kwa kilomita, ilibidi waongeze asilimia 70 ya bei hiyo na kuwa dola milioni 10.5, sawa na Sh bilioni 24.15 kwa kilomita au asilimia 70 ya gharama zote za kujenga reli.
Hii ina maana kuwa Tanzania imejenga reli hii kwa gharama ndogo ikilinganishwa na nchi zinazoizunguka. Kwa wastani hii reli ya umeme ya ‘Standard Gauge’, Tanzania inajenga kilomita moja kwa dola milioni 4.1, sawa na Sh bilioni 9.43.
Uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa ujenzi wa kipande cha kwanza kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro; ambacho ni kilomita 300, kwa maana ya kilomita 205 za njia kuu na kilomita 95 za njia ya kupishania, kimejengwa kwa gharama ya dola za Marekani bilioni 1.22 ikijumuisha na VAT. Ukigawa kilomita 300 kwa kiasi hicho cha fedha, unapata wastani wa dola milioni 4.07 kwa kila kilomita, ikiwamo Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Kipande cha pili cha Morogoro mpaka Makutupora ya Singida chenye urefu wa kilomita 422, zikiwa kilomita 336 za njia kuu na kilomita 86 za njia za kupishania, kinajengwa kwa gharama ya dola bilioni 1.924. Ukigawanya kwa kilomita 422 ni sawa na dola milioni 4.6 kwa kilomita moja ikijumuisha VAT.
Ikumbukwe kipande hiki cha reli kimepita milimani kwa zaidi ya kilomita 120, ikiwamo na kuchoronga mahandaki (tunnels) zaidi ya kilomita 2.7.
Kipande cha tano cha Mwanza mpaka Isaka chenye urefu wa kilomita 341 kikiwa ni njia kuu kilomita 249 na kilomita 92 zikiwa njia za kupishania, kimejengwa kwa gharama ya dola bilioni 1.33. Ukigawa kwa kilomita 341 inakuwa dola bilioni 3.9 kwa kila kilomita moja, gharama hii ikijumuisha VAT.
“Sasa angalia kituko cha upembuzi yakinifu uliofanywa Novemba 2015 na kampuni inayoomba sasa kujenga vipande vilivyobaki kwa kutumia wanasiasa na wataalamu wachumia tumbo. Hawa walitaka wapewe mradi wote wa reli kuanzia Dar es Salaam hadi Mwanza na Kigoma. Kila kilomita moja walitaka kuijenga kwa dola milioni 6.2, sawa na Sh bilioni 14.26 kwa kilomita moja,” anasema mtoa taarifa na kuongeza:
“Na hiyo reli ambayo ingejengwa ni kama ya Kenya. Na kama ingejengwa tukataka ‘ku- upgrade’ ifanane na ya sasa ya kwetu, serikali ingetakiwa kutumia gharama zaidi ya asilimia 70. Maana yake nini? Ukiongeza asilimia 70 ya dola milioni 6.2 kwa kilomita moja, maana yake tungejenga kilomita moja kwa dola milioni 10.5 ili tupate reli ya ‘standard’ inayojengwa na Yapi Merkezi.
“Nini maana ya gharama hizo nilizozitaja? Maana yake ni kuwa gharama inategemea na eneo (terrain) ukipita kwenye milima na kuchoronga mahandaki, gharama ni tofauti na ujenzi wa sehemu nyingine. Hao hao waliotaka kutujengea reli ya kizamani kwa kilomita moja kwa dola milioni 6.2, leo ndio wanaopigiwa debe na wanataka kuwaamanisha Watanzania kuwa ni wazalendo. Walikwisha kusaini mkataba mwaka 2015 ambao Rais Magufuli alisema hautambui,” amesema.
JAMHURI limefahamishwa kuwa nchi nyingi Afrika zimeliwa katika ujenzi wa reli kwa kutumia gharama ya kati ya dola milioni 5.1, sawa na Sh bilioni 11.73 hadi dola milioni 8.0, sawa na Sh bilioni 18.4 kwa kilomita bila asilimia 18 ya VAT.
“Sasa kelele zimeanza wanataka tuwape hawa kazi hii. Sisi tunasema hapana. Tumsaidie Rais Samia [Suluhu Hassan] nchi yetu isiingizwe majaribuni. Utaratibu uliotumika kupata wazabuni kwa ‘Lot 2’ na ‘Lot 5’ ndiyo utumike kupata wa ‘Lot 3’ na ‘Lot 4’. Kinacholengwa kufanywa hakina masilahi kwa taifa letu,” amesema mtoa habari mwingine.
Duniani ujenzi kama uliofanywa na Tanzania kwa takwimu za mwaka 2015, wastani wa ujenzi wa kilomita moja ya reli ni dola milioni 3.5, sawa na Sh bilioni 8.05 bila kodi ya VAT.
Kwa mabadiliko yaliyotokea ya bei za vifaa ikijumuisha na kupanda kwa bei ya chuma, bei ya mafuta, bei ya saruji na vifaa vingine inakadiriwa sasa kuwa wastani wa kujenga reli ya umeme kilomita moja inagharimu dola milioni 4.0, sawa na Sh bilioni 9.2.
Uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa kelele zinazoendelea zinatokana na kuzipigia debe kampuni tatu za Kichina ambazo zimewasilisha serikalini maombi ya kujenga kipande cha 3 na cha 4 kwa wastani wa bei ya dola milioni 5.5, sawa na Sh bilioni 12.65 kwa kilomita. Gharama hii iko juu kwa zaidi ya dola milioni 1.5, sawa na Sh bilioni 3.45 ikilinganishwa na gharama za sasa za ujenzi zinazotumika.
“Kaka hapa kinachofanyika ni watu wanataka wagawane hizo Sh bilioni 3.45. Tukiwakubalia nchi itapoteza zaidi ya Sh trilioni 2. Hizi fedha zitaingia mifukoni mwa watu na kwa kweli haikubaliki. Tujenge reli kwa utaratibu wa zamani ambao tumeanza nao. Huu mchakato wa zabuni ukianza sasa, kwanza, hautakamilika, lakini hata ukikamilika ni miaka mitatu ijayo. Tutapoteza mwelekeo. Tuendelee kama tulivyokuwa tumalize hii reli, wanaopigania matumbo yao tuachane nao,” amesema mtoa habari mwingine.
JAMHURI limezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa, aliyekiri kuyasikia hayo maelezo wanayotaka mchakato uanzishwe wa kutangaza vipande vya 3 na 4 vya reli naye akasema: “Sisi tupo kumsaidia Mheshimiwa Rais. Tunaamini kwa masilahi mapana ya nchi hii, reli hii ujenzi wake ulianza na unaendelea vizuri.
“Kuna utaratibu wa kisheria wa ‘single sourcing’ ikiwa anayetoa zabuni anazifahamu gharama halisi za mradi. Naamini utaratibu huu ni mzuri na utatupunguzia kelele. Rejea yaliyotokea mwaka 2016. Kelele zilikuwa nyingi kuliko sasa na tuliendelea kwa masilahi mapana ya taifa letu. Matunda bora kabisa ya ujenzi yanaonekana.”
Kadogosa anasema anasubiri mchakato wa kumpata mzabuni unaondelea serikalini ukamilike ‘Kazi Iendelee’.
JAMHURI linafahamu kuwa kuna kundi la watu wanaoamini kuwa baada ya kufariki dunia Rais John Magufuli, kwa sasa wanaweza kupenyeza masilahi yao binafsi katika miradi ya kitaifa na kujipatia fedha nyingi. Gazeti hili litaendelea kufuatilia sakata la mradi huu kuhakikisha nchi haiingizwi katika gharama zisizostahili
at what cost?msiangaike sana.. taarifa zilizopo sasa ni Yapi Merkez watapewa hio lot 3&4