Unapouliza swali, saidia unaowauliza waweze kukujibu vizuri, bila matatizo na kukupa details kwa kuwapa wao details.
Unataka kuja bongo utafikia mji gani? Maana costs of living zinatofautiana mji na mji. Utataka kukaa sehemu yenye hadhi gani? Maana kupanga nyumba Oysterbay Toure Drive si sawa na Manzese kwa mfuga mbwa.
Lifestyle yako ikoje? Unajirusha vipi, mara ngapi? Mambo ya usafiri vipi, utapata au utataka ku rent au utanunua kitu kikusaidie kwa miezi hiyo minne?
Ndiyo maana "Who Cares?" kaanza kukulundikia bajeti za kuanzia Manzese Uwanja wa Fisi kwa mfuga mbwa mpaka za Kempinski kwenye kutumia $ 500 kwa siku (that was kwa siku by the way, not kwa mwezi kama ulivyomnukuu, ukifikiri kwa mwezi hiyo haitoshi hata rent viwanja vya kati tu, achilia vya Toure Drive huko).
Kwa sababu hukuitoa specifics, naamini ukienda na budget ya $ 100 kwa siku, which comes to about $ 12,000 hutakuwa katika range mbaya ingawa viwanja vya Mzee Who Cares vinavyotaka bajeti za kifisadi za $ 500 kwa siku utakuwa hugusi.
Na hapo sijagusa big ticket items mambo ya kununua gari au kiwanja kama una hesabu hizo, kama una hesabu hizo na resources ziko mkandaa unaweza kufupisha ziara ili ufanye mambo makubwa mengi, au unaweza ku relax independency yako na kubanana na ndugu wa karibu kwani huko nyumbani tunasema ndugu hawabanani.
La kama ushageuka Mmarekani na hutaki kubanana poa tu, but your $ 100 is nothing nowadays, hata nikiwapa watoto wa shule kununua ubuyu hawachelewi kuja kuniomba tena, kwamba imeisha, na nikiangalia cost of living hata sishangai.