Cosy cafe Dar es Salaam: ''Kijiwe'' cha Julius Nyerere na Zuberi Mtemvu 1950s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074



Ilikuwa Julius Nyerere akiwa rais wa TANU ndiye aliyemshawishi Zuberi Mtemvu kuacha kazi na kuwa mtumishi wa kuajiriwa wa TANU.

Mtemvu akaacha kazi kama Assistant Wlefare Officer na kuwa mtumishi wa TANU kama Secretary General wa kwanza wa TANU.

KIla siku asubuhi Mwalimu Nyerere na Zuberi Mtevu walikuwa wanakunywa chai pamoja Cosy Café na kupanga ya kufanya kwa siku nzima huku wakistaftahi.

Mtemvu alikuwa akiishi Mtaa wa Somali Gerezani na Nyerere alikuwa akiishi Magomeni Maduka Sita.

Miaka hiyo ya 1950 Cosy Café ilikuwa moja ya hoteli zenye hadhi yake.

Jengo hili hadi leo bado lipo Mtaa wa Mkwepu, Dar es Salaam.

Kwa hakika Cosy Cafe ni moja ya sehemu ya kumbukumbu katika historia ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika.
 
ingelifaa ungeliweka picha ya hiyo caff
 
Taratiiibu tutaandika historia ya kweli ya Tabganyika,yenye harakati za kweli za ukombozi mpaka uhuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…