Wana JF,
Nimetumiwa e-mail nyingine yenye kichwa hicho cha habari. Nimeamua kuhifadhi jana la Mzalendo huyo lakini naamini baadhi yenu mmeshapokea skendo hii. Hivi ndivyo viongozi wetu tuliowaamini wanavyotufanyia-USALITI! Tuwafanyeje?
MIZENGWE MINGINE YA KUUZA NCHI YAFICHULIWA
Wadau,
Pata ufisadi mwingine wa TISCAN na TRA hapo chini.
Abbreviations za BWM na EL, hope wote mnazielewa.
Hiyo ndiyo "Nchi ya Changa la Macho".
Hili la TISCAN linafahamaika vizuri sana na BWM
aliamua kwa ujeuri wa hongo baada ya kupewa
recommendations na rafiki yake Jerry Rawlings wa Ghana
, na kuamua against the recommendations of his own
intelligence officers. BWM alipelekewa hiyo ripoti
kuhusu mbinu na tabia za COTECNA ambao wanajiita TSCAN
na ripoti ilieleza kwa undani mbinu chafu za Cotecna
failures zao kule Ghana ,
http://www.thestate smanonline. com/pa... =1&newsid= 4509
na Senegal , pamoja na hongo za kumhonga Kofi Anan kwa
kupitia kijana wake - Iraq 's Food-Oil program.
TISCAN ni jina bandia linatumika na COTECNA kuficha
madhambi yake, na representative wao Tanzania (former
katibu mkuu) ndiye aliwaambia wabadilishe jina na hii
baada ya ku-tender kama COTECNA. Kwa hivyo technically
TISCAN NEVER tendered for Container Scanning Services
na TRA, Central Tender board wanajua hili .
Baada ya BWM kupewa ripoti na makachero wake yeye
badala ya kuamua akawatupia mpira TRA na kuwaambia wao
TRA waamue la kufanya. TRA pia waka amuriwa kupitia
wizara ya fedha Yona akiwa waziri,waende wakaone
shughuli za container scanning zinavyofanywa Ghana ,
kumbe ni mpango wa COTECNA through BWM.
The Commissioner General of TRA wakati huo marehemu
Sanare, baada ya kuelezwa madhambi ya COTECNA akaweka
ngumu na kusema hawa Cotecna hawapati hiyo contract.
Masikini kumbe Sanare kajichongea, kwa vile wahenga
wasema "penye fedheha penyeza rupia". Kumbe zengwe
likawa linapikwa Sanare aondolewe TRA, kwa vile yeye
ndiye analeta kauzibe, wakati list yote ya wazito pale
Mapato House na Matumizi House wameshalainishwa! Basi
Sanare ikabidi ahamishiwe PM's office. Sasa kabla ya
Sanare kuondoka akambiwa pesa hizi hapa mzee, weka
mkono mambo yaende mbele.Wewe unaondoka, mkataba
utasainiwa na pesa utazikosa. Sasa amua kusuka au
kunyoa! The last contract Sanare signed before he left
the office was Cotecnas contract pamoja na hilo jamaa
wakamtolea nje. Kwa kumkomoa zaidi, wale aliokuwa
amewafanyia kauzibe TRA, wakaamua kumnyan'ganya hata
gari lake na kutaka kumfukuza kwenye nyumba hadi EL
akaingilia na kuamua kumuuzia nyumba wakati yuko
mahututi! Sanare amekufa na frustrations za
kunyanyaswa na wenzake TRA kwa vile alikataa kucheza
dili zao !
Issue ya TIScan siyo siri wala lolote, data zote zipo
na zinajulikana, zengwe lililochezwa hata usalama wa
taifa wanalijua na walimweleza BWM kama rais atoe
uamuzi lakinia he acted otherwise. Yaania hata VIN
number ya hilo gari lao la Scanning inajulikana. Liko
re-fubrished kwa vile baada ya kupinduka Ghana
lilipelekwa Ujerumani kukarabatiwa. Bei ya hilo gari
imezidishwa zaidi ya mara tatu ya jipya wakati ni
used. Halafu la kusikitisha ni kuwa undeshaji wa
scanner hiyo TRA officials hawausiki. Risk management
and assessment na profiling of importers TRA kwao ni
ndoto wanawategemea TISCAN!
Lingine linaloudhi ni hili, TIScan are supposed to do
Destination Inspection na hii ndiyo ilikuwa kigezo cha
kuanzisha hiyo scanning. This was supposed to replace
Pre-Shipment Inspection. Hadi leo hii vyote vinafanywa
na kampuni hiyo hiyo, TISCAN + COTECNA. Wewe leo
unatumia pesa zako ulizozihenyea huku nje, na ukatuma
mzigo wa vitabu ambao haulipiwi kodi lakini bado
utalipishwa 1.2% ambayo TScan wanapewa 0.8% kwa nini.
Did you know that TISCan collects 0.8% of the value of
all imports to Tanzania and it is the LAW !!! na 0.4%
wanachukua BOT! Na TISCAn wana mkataba wa miaka 10+!!
Amakweli nchi imeuzwa! Tunayasikitikia ya BOT, TRA ni
balaa!
'the most important part of knowledge is having reverence for the lord'
proverbs 1:7.