Country Boy asema hawezi kufanya PlayBack

STUNTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
13,076
Reaction score
17,247
Rapa Country Boy amefunguka na kusema kuwa kwa sasa amekua kisanaa hivyo hayuko tayari kufanya ‘Playback’ katika show zake na kwamba sasa anafanya muziki ‘live’ na band yake na ameamua kufanya hivyo kuwaonesha watu kuwa ana uwezo wa kufanya hivyo.

Rapa Country Boy alisema hayo kupitia kipindi cha Bongo Fleva Top 20 ya East Africa Radio na kudai kuwa muziki wake sasa ni mkubwa hivyo haoni sababu ya kuendelea kufanya ‘Playback’ katika show hivyo sasa ni mwendo wa live music pamoja na band yake.

Pia Country Boy amedai kuwa kwa sasa amenzisha ‘tour’ yake mwenyewe kuzunguka nchi nzima ambayo ameipa jina la ‘Dakika 45’ za Country Boy. “Sasa hivi nimeanza tour yangu ya ‘Dakika 45’ za Country Boy nafanya live Music, live band, na watu wa Band nyuma, wapiga gitaa, wapiga Solo, Piano, watu wa Drums, kila mtu anafanya set up ya live show.

Aliendelea “hivyo kila nitakapokuwepo nitafanya live show na Band, ni kitu ambacho nataka nikifanye. Hata ukiangalia wasanii wa Marekani wanapofanya how wanafanya live mzee,mimi siwezi kufanya ‘playback’ wakati mimi ni msanii mkubwa ambaye nina uwezo wa kufanya vitu kibao.

Nataka kuwa prove watu kuwa nina uwezo wa kufanya live lakini pia nataka kuwaonyesha energy ndiyo maana nimeweka dakika 45 za Country Boy sidhani kama kuna msanii yeyote anaweza kufanya show ya dakika 45 non-stop ya ngoma zake mwenyewe bila mtu mwingine mimi nimeamua kufanya hivyo”
alimalizia Country Boy
 
Akili za usiku, Country boy ft Young D & Msodoki (nice song)
*wazo zuri sana kwa country boy kuachana na playback
*wazo zuri kufanya tour nchi nzima
*wazo zuri kuajiri wenzake katika band
Mipango yake hii itamfikisha mbali kimziki na mafanikio
 
Sawa country.boy ila wew na na stamina miaka yote hamkui kisanaa tatizo nini mpo pale pale
 
Sawa country.boy ila wew na na stamina miaka yote hamkui kisanaa tatizo nini mpo pale pale
Aisee wabongo tuna uelewa tofauti, hivi mpaka MTU amekuwa na live band , ameandaa tour ya bend yake nchi nzima bado unasema hajakua kisanaa??? Labda mm sielewi kukua kisanaa maana yake
 
Live band ndio kipimo cha kujua muziki....Playback ni kichaka cha wengi
siku zote walikua wapi?
kwanini kila msanii kabla hajatoka asingekua anaimba kwanza liveee ndo anatoa single ili awaimbie hizo live..

maana kila kona live live mpaka sasa inekua kero
 
siku zote walikua wapi?
kwanini kila msanii kabla hajatoka asingekua anaimba kwanza liveee ndo anatoa single ili awaimbie hizo live..

maana kila kona live live mpaka sasa inekua kero

Playback kila mtu anaweza fanya, hata shishi imemtoa...live band ni chekecheo la pumba na mchele
 
DOGO NAMUELEWA SANAAA....ANATISHA SEMA NDIO HIVYOOO...ANAPIGA MUZIKI KWA WENYE UPEO MKUBWA WA KUELEWA NA SIO KWA AKILI ZA VIJANA WA KARNE HII....ANGEKUWA MAREKANI DOGO ANGEKUWA LEVEL ZA KINA WIZZY F BABBYYYY
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…