Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Salam,Wakuu naomba kujua kuhusu hili - Nimeona cheti za Death Certificate kimeandikwa (Course Of Death is CCF) Naomba kwa wale wataalamu wa udokta nini maana ya CCF! Asante.
Salam,
C C F ni neno la msamiati wa kitabibu ambalo ni kifupipisho cha NENO C= CONGESTIVE C= CARDIAC F= FAILURE ni ugonjwa unaotokana na moyo kushindwa kufanya kazi zake na kusababisha mrundikano wa damu kwenye mwili ambao huambatana na dalili za mgonjwa kushindwa kupumua vizuri hususan akilala chali, kuvimba miguu na hata kufikia hatua ya kuvimba tumbo, natumai kwa maelezo hayo kwa mtu wa kawaida, utakuwa umefarijika kama bado jamvi liko wazi karibu tena.