#COVID19 Covid-19 hawaihusu walio chini ya umri wa miaka 18?

Lyaka Mlima Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2020
Posts
361
Reaction score
521
Sijaelewa utaratibu wa chanjo hii ya uviko kuwabagua walio chini ya miaka 18 tumejiridhisha vipi kuwa wao hawawezi kuambukiza na kuambukiza??¿

Taifa lisipokuwa na sera zake litafanyia kazi sera za mataifa mengine..

Tufikiri pamoja kama taifa

 
Nijuavyo mimi, kwa ufahamu mdogo, chanjo, kwa kawaida, hujaribiwa kwa watu wazima kwanza, na baadaye kwa watoto baada ya kutathmini uwezo wake na usalama umethibitika katika watu wazima. Hii ni kwa sababu watoto bado wanaendelea kukua. Pia UVIKO-19, kwa sasa, umekuwa ni ugonjwa mbaya na hatari miongoni mwa wazee.

Kwa kuwa chanjo hizo zimekusudiwa kuwa salama kwa watu wazima, zinafanyiwa utafiti kwa ajili ya watoto.
 
Kwa hiyo ipo ktk majaribio ????
 
Chanjo ya Janssen kwa sasa ni 18+ lakini Pfizer na Moderna zimeruhusiwa pia kwa wenye miaka 12 kwenda juu ná hivi karibuni labda November au December zitaruhusiwa mpaka wenye miaka mitano kwenda juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…