#COVID19 Covid-19 ipo, tuhamasishane kila mtaa kuanza mazoezi ya kutembea angalau kilomita 1 kila Jumamosi

4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2019
Posts
8,406
Reaction score
9,619
Mazoezi pia ni fursa nzuri ya kujikinga na Corona,

Kwa umoja wetu kuanzia MTAA Tanzania nzima tuhamashishane Sasa kufanya mazoezi ya kutembea angalau km1- 3 kila jmosi ya wiki, itapendeza Sana tukianza jmosi ya week ijayo.

Mazoezi ya kutembea ni mepesi mno hata mzee anaweza kufanya.

Kwa nafasi zetu tuelimishe watu kwenye mitaa yetu nyumba kwa nyumba ili watu washiriki mazoezi ya kutembea, lazima tubambane na corona KWa NJIA zote.

Niwaombe Watanzania kupokea ushauri huu kwa mikono miwili

Shukrani.
 
Sahihi kabisa mkuu. Warundi wana utamaduni wa kufanya mazoezi, utawakuta kila jioni wanatembea wengine wanakimbia. Nadhani Covid 19 haijawapiga sana.
 
Mimi kutokana na shughuli zangu kwa siku natembea wastani wa kilometa 9, jumamosi acha nilale🤣
 
Kutokana na harakati za maisha ya kila siku bila shaka watu wanatembea zaidi ya km1 kila siku.

Hivyo hiyo ya kutembea km1 kila jumamosi itakuwa njia nzuri ya kusambaza ugonjwa ukichangia mtakuwa mkitembea pamoja kwa karibu which is highly unsafe.
 
Mkuu, ushauri wako ni mzuri sana. Mheshimiwa wetu Ndugu Mizengo Pinda aliwahi kuongelea kitu kama hiki, hasa kwa wale wastaafu.
Wengi wao wanajisahau sana, kutwa wako ndani. Ni hatari sana.
 
Kutokana na harakati za maisha ya kila siku bila shaka watu wanatembea zaidi ya km1 kila siku.

Hivyo hiyo ya kutembea km1 kila jumamosi itakuwa njia nzuri ya kusambaza ugonjwa ukichangia mtakuwa mkitembea pamoja kwa karibu which is highly unsafe.
Sio kweli mkuu ,Mbona watu tofauti tunakutana sokoni kila siku
 
Corona ya sasa hivi ni kama kipindupindu.Kuna kuharisha na kutapika,sina uhakika kama mazoezi yatafua dafu tena!
2849129_1626694979894.png
 
Mkuu yatasaidia Sana , mazoezi ni afya , naona UVCCM wamezindua ya kwao , huu ni uchoyo ,tuhamasishe watu wote kuanzia kwenye mitaa yetu kufanya mazoezi bila kujali itikadi za vyama,

TWENDE NA MAZOEZI YA KUTEMBEA KM 1- 3 KILA JMOSI TUTAMSHINDA CORONA NA MAMBO YAKE YOTE
Corona ya sasa hivi ni kama kipindupindu.Kuna kuharisha na kutapika,sina uhakika kama mazoezi yatafua dafu tena!
View attachment 1875272
 
AC utumie wewe, gari uendeshe wewe kutwa kucha, misosi uzidishe kula wewe, sukari uzidishe kula wewe, kwichikwichi uzidishe wewe alafu mazoezi ndio tufanye wore. Kila mtu ashike hamsini zake bhanaaaaa. Wengine tunashinda shambani kusukuma jembe.
 
Kutokana na harakati za maisha ya kila siku bila shaka watu wanatembea zaidi ya km1 kila siku.

Hivyo hiyo ya kutembea km1 kila jumamosi itakuwa njia nzuri ya kusambaza ugonjwa ukichangia mtakuwa mkitembea pamoja kwa karibu which is highly unsafe.
Wale wa kwenye mashangingi na viyoyozi watembea saa ngapi
 
AC utumie wewe, gari uendeshe wewe kutwa kucha, misosi uzidishe kula wewe, sukari uzidishe kula wewe, kwichikwichi uzidishe wewe alafu mazoezi ndio tufanye wore. Kila mtu ashike hamsini zake bhanaaaaa. Wengine tunashinda shambani kusukuma jembe.
Mkuu nimecheka Sana neno kwichikwichi, tafadhali naomba tushiriki mazoezi
 
Mazoezi pia ni fursa nzuri ya kujikinga na Corona,

Kwa umoja wetu kuanzia MTAA Tanzania nzima tuhamashishane Sasa kufanya mazoezi ya kutembea angalau km1- 3 kila jmosi ya wiki, itapendeza Sana tukianza jmosi ya week ijayo.

Mazoezi ya kutembea ni mepesi mno hata mzee anaweza kufanya.

Kwa nafasi zetu tuelimishe watu kwenye mitaa yetu nyumba kwa nyumba ili watu washiriki mazoezi ya kutembea, lazima tubambane na corona KWa NJIA zote.

Niwaombe Watanzania kupokea ushauri huu kwa mikono miwili

Shukrani.
Mimi ninayeendesha baiskeli saa 1 kila siku haya yatanihusu kweli?
 
Back
Top Bottom