COVID19: Afya ni muhimu kuliko utanashati

COVID19: Afya ni muhimu kuliko utanashati

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Baadhi ya Watanzania bado wamekuwa wakienda kwenye saluni kwa ajili ya huduma za kunyoa, kusuka, kusafisha kucha, huduma za kusafisha ngozi na masaji. Jamani tunaweza kuishi bila hivi vitu kwa muda. Tujitahi

Huduma hizi zinahusisha ukaribu wa mhudumu na mteja na ni rahisi kupeana maambukizi endapo mmoja ameathiriwa na #CoronaVirus

Afya njema ni muhimu kuliko utanashati. Tutakaposhirikiana kama jamii kwa kujikinga na #COVID19 ndivyo tutakaporudi kwenye taratibu zetu kwa haraka na kufanya yote tunayoyapenda

Endapo inawezekana, kaa ndani na utoke pale tu unapokuwa na ulazima kama kununua chakula au dawa na uhakikishe unavaa barakoa na kusafisha mikono yako mara kwa mara

Endapo inakulazimu kutoka, hakikisha unazingatia umbali wa mita 2 kati yako na watu wengine

Kama utanashati ni kipaumbele sana kwako au kazi au kazi yako inakulazimu, angalia uwezekano wa kununua vifaa vya kufanyia shughuli hizo na ujipe huduma mwenyewe.
 
Upvote 1
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom