COVID19: Tafiti zinaonesha mama hawezi kumwambukiza mtoto aliye tumboni; maziwa pia yako salama

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Hadi sasa hakuna utafiti uliopata hitimisho kuhusu mama mjamzito kumwambukiza mtoto aliye tumboni endapo ameathirika na #COVID19

Kwa mujibu wa WHO, kuna tafiti mbalimbali zinazoashiria kuwa hakuna uwezekano wa maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto aliye tumboni. Pia wameeleza kuwa #CoronaVirus havikukutwa kwenye maji ya uzazi “amniotic fluid” wala maziwa

Wakati inaelezwa kuwa wajawazito wasio na matatizo mengine hawako katika hatari ya kuambukizwa #COVID19 kuliko watu wengine, wanashauriwa kuchukua tahadhari kubwa

Vilevile, si lazima mjamzito ambaye anaonesha dalili za #COVID19 kujifungua kwa njia ya upasuaji bali njia ya uzazi itategemea na mapendeleo yake na ushauri wa mtaalamu

Mama aliyeathirika anaruhusiwa kumnyonyesha mwanae huku akizingatia taratibu za kuzuia maambukizi ikiwemo kuvaa barakoa muda wote awapo na mtoto na kunawa mikono kabla ya kumshika

Source: Coronavirus: Can pregnant mothers infect their children with COVID-19?
 
Upvote 0
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…