JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Anga la Tanzania likiwa limefunguliwa na kuruhusu wasafiri kutoka pande mbalimbali za dunia, inategemewa kuwa hivi karibuni nchi mbalimbali zitafungua mipaka na shughuli za utalii zitaanza kuimarika upya.
Ingawa si jambo linaloshauriwa lakini hakuna namna ya kulizuia kwani Maisha lazima yataendelea na kila mtu ana uhuru endapo havunji sheria wala taratibu.
Mapendekezo yanayotolewa kwa Watalii wa Kimataifa ni kama ifuatavyo
Ø Ni jambo jema zaidi endapo unaumwa au una matatizo ya kiafya kama Kisukari, Shinikizo la Damu, Pumu au una umri mkubwa kuepuka au kusubiri kwanza kabla ya kufanya safari za kimataifa
Ø Taratibu za jumla za usafi ikiwemo kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni mara kwa mara, uvaaji barakoa, Kukohoa kistaarabu (kwenye sehemu ya ndani ya kiwiko cha mkono au kwenye tishu ambayo itatupwa mara tu baada ya kumaliza), na kuepuka kushika pua au mdomo zizingatiwe
Ø Umakini unahitajika katika suala zima la chakula kuanzia usafi wa mikono ya mlaji na eneo utakaponunua chakula, uandaaji wake pamoja na ufungashaji. Epuka chakula ambacho hujaona uandaaji wake au ambacho kinauzwa eneo la wazi ambalo watu wanapita au kinachouzwa na mtu asiyevaa barakoa
Ø Epuka kwenda maeneo ya misongamano ya watu ambapo itakuwa ngumu kuweka umbali wa mita 1 kati yako na mtu mwingine
Ø Uendapo kwenye “museums” au vivutio vingine epuka kushika sehemu za pembeni ya ngazi, kushika vitu vilivyo katika maonesho, kushikana mikono na watu kwani ni sehemu zinazotembelewa na watu wengi kwa siku
Ø Epuka kujihusisha kingono na watu wa eneo utakaloenda kwani ni rahisi sana kupata maambukizi wakati wa tendo
Ø Kuwa makini unapotumia vilevi. Inashauriwa zaidi kutumia vilevi uwapo ndani ili kuweza kujidhibiti unapolewa
Ø Utakaporudi nchini ni sharti ujitenge kwa siku 14 ili kuepuka kusambaza maambukizi (endapo umepata) kwa wengine

Upvote
0