Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
"Wakati mwingine unakuta baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa na dhana hiyo yakudhani labda Jeshi la Polisi limekuwa likiwakandamiza jambo ambalo sio" amesema CP Awadhi Haji
CP Awadhi Haji amesema kwamba dhana hiyo inaweza kuwa ikawa inatokana na utofauti wa mitazamo na uelewa uliopo kwa Watu.
Lakini amesema kuwa Jeshi la Polisi lipo kwa ajili ya kusimamia uzingatiaji Sheria bila kuwa na upendeleo isipokuwa kwa kuzingatia Sheria na taratibu.
Ameyasema hayo wakati akishiriki mafunzo ya kukumbushiana Sheria na miongozo mbalimbali kwa makamanda wa Jeshi la Polisi kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu, ambapo mafunzo hayo yanaratibiwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)
Ikumbukwe kauli hiyo anaitoa ikiwa ni siku chache baada ya baadhi ya vyama vya siasa na wanaharakati mbalimbali kulitaka Jeshi la Polisi kutekeleza majukumu yao kwa uweledi kwa kuzingatia Sheria, taratibu na maadili vinavyowaongoza katika utekelezaji wa majukumu yao.