Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeeleza mafanikio makubwa iliyoyapata tangu kuanzishwa kwake mwaka 1994, ikiwemo ongezeko la vyuo vya ufundi stadi kutoka 14 hadi 80, kuongezeka kwa vyuo binafsi hadi zaidi ya 770, na kupanuka kwa wigo wa udahili wa wanafunzi kutoka 38,560 hadi 380,000 kwa mwaka.
Akizungumza siku ya Ijumaa Februari 21, 2025 mkoani Singida katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi kwa kanda zote nchini, sambamba na kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa VETA, Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, CPA Anthony Kasore, amesema ongezeko la vyuo na wanafunzi ni mafanikio makubwa yanayoonesha dhamira ya serikali katika kuwezesha vijana kupata ujuzi wa kiufundi unaohitajika sokoni.
"Tangu VETA ianzishwe, tumeona mabadiliko makubwa. Mwaka 1994, vyuo vya VETA vilikuwa 14 pekee, lakini leo tuna vyuo 80 vilivyopo katika wilaya na mikoa mbalimbali nchini. Pia, sekta binafsi imeonesha ushirikiano mkubwa ambapo idadi ya vyuo binafsi imeongezeka kutoka chini ya 50 hadi zaidi ya 770, hivyo kufanya jumla ya vyuo vya ufundi stadi nchini kufikia zaidi ya 870," amesema CPA Kasore.