CPR: Huduma muhimu inayookoa uhai wa watu walio kifoni

CPR: Huduma muhimu inayookoa uhai wa watu walio kifoni

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
CPR, ama Cardiopulmonary Resuscitation ni njia ya dharura na haraka, inayotolewa kwa mtu aliyepatwa na changamoto ya mshtuko wa moyo (Cardiac arrest).

6C894DAC-7F82-4053-973A-D52F28C1FD4D.jpeg


Huhusisha kubonyeza kifua pamoja na kutoa hewa mbadala kwa mhusika ili kutunza mzunguko wa damu kwenye viungo muhimu vya mwili ikiwemo ubongo.

Ikiwa itaanzishwa haraka, CPR hupunguza vifo kwa asilimia 50 hadi 75 kwa watu wenye mshtuko wa moyo (Cardiac arrest).

NAMNA YA KUFANYA
  1. Kwa watoto wachanga, tumia vidole viwili
  2. Watoto wakubwa kidogo, walau chini ya miaka 5 tumia mkono mmoja, au unaweza kutumia mikono miwili.
  3. Watu wazima tumia mikono miwili.
  4. Bonyeza kifua kuelekea upande wa kushoto ambapo moyo umelalia zaidi mara 100-120 kwa kila dakika. Kila unapobonyeza kifua hakikisha kimezama ndani, na unapaswa kuruhusu kirudi juu kwanza kabla haujabonyeza tena.
  5. Kama upo peke yako hakikisha kila baada ya kubonyeza kifua mara 30, mpumulie mdomoni mwake mara 2. Kama mpo wawili unapaswa kubonyeza kifua mara 15 kisha mpumulie mdomoni mara 2.
  6. Wakati huu, hakikisha mawazo na akili zako zote zipo hapo. Usifanye kazi nyingine zaidi ya hii.
  7. Hakikisha mgonjwa anazungukwa na hewa ya kutosha
Kwa kuwa mtu asiye na ujuzi wa elimu ya afya ni ngumu kujua mshituko wa moyo ni nini, hivyo atapaswa kufuata kanuni hizi tatu kama silaha yake ya utambuzi.

  • Kukata kauli ghafla
  • Kukosekana ghafla kwa mapigo ya moyo, hasa kwa kutazama mishipa inayopatikana sehemu ya juu ya shingo, au kwenye maungio ya kiuno na paja (karibu na sehemu za siri)
  • Kuzima kwa upumuaji wa mgonjwa
Kama kuna ndugu karibu yeye ndiye aendelee kuita msaada wa watu wengine wa karibu, pamoja na kufanya taratibu za kumpeleka mgonjwa hospitalini huku wewe ukiendelea kubonyeza kifua.

Badala ya kumpumulia moja kwa moja hasa kwa mtu ambaye hufahamu historia ya afya yake, unaweza kutumia kifaa chochote (mfano puto) chenye uwezo wa kusukuma hewa ya kutosha mdomoni mwa mgonjwa.

STG NEMLIT 2021
 
Kwa dunia ya sasa haishauriwi kumpumulia mdomoni labda awe ni mtu unayeijua afya yake.... La sivyo tumia manuva angalau msigusanishe majimaji yenu.

All in all good thread...
 
Kwa dunia ya sasa haishauriwi kumpumulia mdomoni labda awe ni mtu unayeijua afya yake.... La sivyo tumia manuva angalau msigusanishe majimaji yenu.

All in all good thread...
Hatari inayotokana na kugusana na mate au hewa yake sio kubwa kivile. French kisses zingeshatuua sana.

Ila mtoa huduma unatakiwa kuwa mbinafsi usijitoe mhanga mfano kugusanisha damu na majeruhi
 
Kusema ukweli wa Mungu. We ushawahi ona wangapi wamepona kwa CPR?

Vipi kuhusu Post CPR Care ikitokea mtu amepona?!
 
Kusema ukweli wa Mungu. We ushawahi ona wangapi wamepona kwa CPR?

Vipi kuhusu Post CPR Care ikitokea mtu amepona?!
Kuna condition na condition..

Trauma wengi wanaofanyiwa cpr wanapona....

Na watoto pia ni rahisi kurudi...

Infact cpr inapaswa kufanyika kwa wale waliopata sudden cardiac arrest, cpr kwa walio na chronic illnesses ni kujisumbua na kumsumbua mgonjwa tuu.
 
Back
Top Bottom