crack inavunja nyumba yetu, msaada plse.

madameA

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
435
Reaction score
176
ukiwa unaenda kwenye vyumba vya kulala lazima upandishe ngazi moja. Sasa hapo katikati kumetokea ufa mkubwa kwenye ukuta ambao unashililia hizo sides 2, umeanzia chini mpaka juu. Ufa huo umeendelea mpaka umeanza kuweka cracks kwenye gypsum na kwenye madirisha ya upande wa chini.
Wataalamu wa ujenzi naomba ushauri nini kifanyike ili kuinusuru hii nyumba, maana naona kama vile itabomoka kabisa.
 
Weka picha.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Nyie ndio mnaweka lenta imara mnaacha kuimarisha msingi,ungemtumia mtaalamu yote yasingetokea.
 
Kwa jibu lako tu wewe uko kinadharia zaid!!!!!

Vipi kama fundi ndo alikosea au ratio ilikuwa ndogo au huyo mtaalamu ashinde site??????
Wasio na uwezo wa kumuajiri huyo mtaalamu wa kukaa site full time wasijenge??????!!!!!
Hujasikia wimbi la nondo zisizokidhi viwango????!!!

Badala ya kulaumu toa suluhisho mkuu au kama vipi ipotezee
 
Mishe kama hizi ni vema mtaalamu akazicheki kabisa maana ushauri wa online yaweza kua tatizo ni tofauti na watu wanavofikiria, labda kama ungekua na images za kila angle ya nyumba angalau kidogo mtu angeweza kujua tatizo liko wapi maana unaweza ukaziba hapo hujaondoa root ya hilo tatizo
 
Weka picha.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Na kuongeza maelezo ya kiwanja kama ni cha mteremko na kilifanyiwa land scaping/kilijazwa udongo
Nyumba ni ya ghorofa au one and a half???!!!!
 
ukiwa unaenda kwenye vyumba vya kulala lazima upandishe ngazi moja. Sasa hapo katikati kumetokea ufa mkubwa kwenye ukuta ambao unashililia hizo sides 2, umeanzia chini mpaka juu. Ufa huo umeendelea mpaka umeanza kuweka cracks kwenye gypsum na kwenye madirisha ya upande wa chini.
Wataalamu wa ujenzi naomba ushauri nini kifanyike ili kuinusuru hii nyumba, maana naona kama vile itabomoka kabisa.

Mkuu nafikiri badala ya kuomba ushauri wa bure hapa jf..ungeulizia km kuna muhandisi(engineer) au msanifu majengo(architect)anayeweza kutembelea hiyo nyumba hiyo na aukukupa ushauri! Acha kuchezea uhai wako na familia, hilo ni jambo la hatari na unahitaji kumpeleka mtaalam akakushauri.usikwepe gharama!!!
 
Kwa jibu lako tu wewe uko kinadharia zaid!!!!!

Vipi kama fundi ndo alikosea au ratio ilikuwa ndogo au huyo mtaalamu ashinde site??????
Wasio na uwezo wa kumuajiri huyo mtaalamu wa kukaa site full time wasijenge??????!!!!!
Hujasikia wimbi la nondo zisizokidhi viwango????!!!

Badala ya kulaumu toa suluhisho mkuu au kama vipi ipotezee

Si lazima mtaalam akae site!
Pia km unaweza kupata pesa za kujenga sidhani km utashindwa kumlipa mtaalam!na iwapo utakuwa na mtaalam yote hayo atayaona kabla ya kuingia kwenye matatizo!usiingie gharama kubwa kwa kukwepa gharama ndogo na za muhimu!
 
ukiwa unaenda kwenye vyumba vya kulala lazima upandishe ngazi moja. Sasa hapo katikati kumetokea ufa mkubwa kwenye ukuta ambao unashililia hizo sides 2, umeanzia chini mpaka juu. Ufa huo umeendelea mpaka umeanza kuweka cracks kwenye gypsum na kwenye madirisha ya upande wa chini.
Wataalamu wa ujenzi naomba ushauri nini kifanyike ili kuinusuru hii nyumba, maana naona kama vile itabomoka kabisa.
hatari hiyo inaweza kubomoka ita wataalam haraka sana, ingekuwa ufa wa kawaida isingeonyesha mpaka kwenye gypsum
 
Tueleze pia aina ya udongo, mchanga au mfinyanzi. Huo uf ni wa kwenda juu tu au kuna wa mshazari? Hiyo nyumba inaweza ikawa inatitia upande mmoja au inavutika upande mmoja au ujenzi hafifu. Mtaalamu lazima afike nyumbani kwako aangalie ndio akupe ushari wa nini kifanyike.
 
ukiwa unaenda kwenye vyumba vya kulala lazima upandishe ngazi moja. Sasa hapo katikati kumetokea ufa mkubwa kwenye ukuta ambao unashililia hizo sides 2, umeanzia chini mpaka juu. Ufa huo umeendelea mpaka umeanza kuweka cracks kwenye gypsum na kwenye madirisha ya upande wa chini.
Wataalamu wa ujenzi naomba ushauri nini kifanyike ili kuinusuru hii nyumba, maana naona kama vile itabomoka kabisa.
Ita mtalaamu akaangalie na aongee na wewe pia kama uliwahi shuhudia wakati ujenzi unaendelea. kwa namna ulivyoeleza ni vigumu mtu kukupa ushauri unaostahili. mtu hawezi jua kama kiwanja kipo kwenye mteremko au tambarare, ulijaza udongo kiasi gani? ni udongo gani uliopo kwenye kiwanja? msingi ulichimbwa urefu gani na umejengwa vipi? ukuta huo uliwekwa beam za chini kabla hujaanza kupandisha kuta na ring beam imepita kwenye hizo kuta? Inaonyesha ukuta huo ni wa ndani fundi anaweza puuzia baadhi ya vitu ingawa unabeba uzito.
 
Huwa wanashona ukuta kwa nondo, sijui kama kwa case yako itakuwa hivyo. Ita mafundi wazuri watakusaidia.
 
Jamani kama ni wataalamu hebu mu m pm huyu mama unajua situation kama hii mtu anaweza kuwa na partial mental block kila akikumbuka gharama
 
Nashukuru kwa ushauri, ila hii kitu imenikosesha amani sana. Kama kuna engineer mtaalamu wa ujenzi plse ushauri wako unahitajika. Na mimi pia naendelea kutafuta mtaalamu ambaye ataweza kuokoa jahazi hili.
 
ukiwa unaenda kwenye vyumba vya kulala lazima upandishe ngazi moja. Sasa hapo katikati kumetokea ufa mkubwa kwenye ukuta ambao unashililia hizo sides 2, umeanzia chini mpaka juu. Ufa huo umeendelea mpaka umeanza kuweka cracks kwenye gypsum na kwenye madirisha ya upande wa chini.
Wataalamu wa ujenzi naomba ushauri nini kifanyike ili kuinusuru hii nyumba, maana naona kama vile itabomoka kabisa.

Mkuu umeniacha hoi, mi nilifikiri crack (unga) umemtawala mwenza wako na unahitaji msaada kumbe ni ufa? Nimekoma.
 
Unaishi wapi kaka, mbona ma engineer wa ujenzi wako wengi tu, nenda halmashauri yoyote ya wilya/manispaa/jiji idara ya ujenzi, mchukue engineer mpeleke home akaangalie akushauri nini cha kufanya, gharama ni usafiri then unaweza kumtoa kwa buku ten
 
Back
Top Bottom