Crazy things you did in secondary school

Kupiga collabo la kande kwenye tawi la mgomba/magimbi maana sahani zilikua hazitoshi! ~Oldadai sec
 
Baada ya kuonekana hatunyoosheki kwa bakola, mwalimu mkuu aliamua kutuomba msamaha na kutuomba tuchomekee shati zetu walau tu pindi Shure inapotembelewa na wageni.
Advance hii kitu niliichukia kishenzi
 
hahahaaa mm nakumbuka mwaka 2008 niko form 4 galanos tanga, kuna mwalim mmoja alikuwa anaitwa macmaster Luziro, alinidaka mtaani..., Sasa akajifanya mjanja et ananiita ananiuliza kijana unasoma wapi, nikamwambia nguvumali sec. Akasema bas nimekufananisha na mwanafunz wang nilimfundisha Ecknford.., Nikamuambia umenifababisha... Sasa hapo wote tukawa tumedanganyana wakat mm nilikuwa namsoma...

Ila alikuja akajua akaniambia we dogo ulinichezea sana akili[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Siku za mvua hatutaki enda morning prepo so tunaweka vitanda kwenye entrances zote za bweni, tunapanda dalini na kutoa bulbs then tunakaa juu mpaka mvua ikate. A friend of mine almost fell down kwa kupitiliziwa na usingizi, ahahahahaha remembering this makes me laugh
 
DAH SIJUI KWANINI NILIKUWA MZEMBE
 

Hii tuneifanya sana watoto wa Tanga School....
 
Kukwepa kukaa mstarini kisa kuadhibiwa kwa viboko msimu wa baridi.

Nakumbuka nilikuwa kidato cha kwanza mwezi agosti, ilisikika sauti mwanafunzi wa kidato cha nne akiongea assemble, tulipigwa wote. Tangu siku ile nilikaa assemble siku ya national and Mock exams tu (Form 2 $ 4)
 
Wewe ulikuwa Ifunda technical nimekustukia!!!
 
Karatu high school..... Muda wa kulala Kuna jamaa alikuwa anatoa ushuzi balaa siku ya makande sasa siku moja alijisahau akawa amazungushia kitanda chake Na shuka Ile kutoa ushuzi harufu ikamzidia ndani ya shuka jamaa akatoka nduki...toka siku hiyo alikoma tabia hiyo
ii ii
 
Nilipokuwa shuleni, piga sheria nyingi. Ingawa nilikuwa mwanafunzi mkali, nilifurahia vitu vya uzimu shuleni
 
kuna kijamaa tumesoma nacho high school vile vinatumwa na jimbo kilikua kinajifungia kupiga msuli kuanzia sa moja asubuhi mpaka kumi na mbili jioni eti kikitoka huko madini yanajaa kichwani mpaka sauti inapotea inakua ukikisemesha kinaongea kwa shida kama ile ukinigwa na moshi wa bangi unavokua kinaongea sauti haitoki eti!!

nyingine nilikuaga na tabia ya kutoroka shule usiku naenda kuangalia miziki ya kikongo kwenye tv kwenye vibandaumiza kijiji cha jirani siku moja mida ya saa tano usiku kuna ki mbalamwezi niko narudi shule kwenye njia ninayopita kama mita 25 hivi kushoto nikaona fisi kama tisa wanagombania fisi jike mmoja!!!

aisee asikwambie mtu binadam anaweza kufanya vitu vikubwa sana anapokua kwenye hali ya kufa ama kupona na sifaham hata nilivuka vipi pale manake mbio nilizotimua siku hiyo hata uchukue bodaboda hunikuti, umbali ambao kikawaida nilikua natembea dk 20 siku hiyo sikuzidisha dakika nne nilikua nishapanda kitandani nimelala.

sitaki kuikumbuka hiyo siku make hua napata uoga sana
 
Ulikuwa fala sana wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…