Crazy things you did in secondary school

★Mimi hii ilinitokea kipindi nipo Form 4 (2012) ilikuwa Mocko Mkoa nikapiga Literature na English 20% kwa 22% na sio kawaida washazoea ni mtu wa 80~96 huko nikaitwa Staff nipigwe Collaboration nilipoona Fimbo zimezagazwa zakutosha na walimu wamekamia wanichape Nikaanza kutoa chozi nikasema Kipindi nafanya Mtihani nilifiwa na Wazazi wote wawili kwa ajari ya gari tena nalia haswa cha ajabu nilikuwa Boarding ko taarifa lazima zingeletwa waalimu bila kufikiri wakaachana na swala lakunichapa wakaanza kunipoza wakanipa na Rambi Rambi [emoji23] .
Kilichinisitua waliposema watangaze shule nzima wajue nikasema hiki kisanga sasa nikagoma nikasema ishapita achaneni nayo, nilipo enda likizo nyumbani nikamuomba MaMa samahani akauliza yanini nikamwambia nilikuuwa akasema kivipi? Nikajielezea Alicheka mpaka Kichomi kikamshika [emoji23]★
 
★Nimekumbuka siku moja nipo Form 2 Boarding school tulikuwa tuna mtindo wakutoroka muda wa prepo mnaenda ku watch movies kitaa. Sasa mkiwa mnatoroka mfano mkikutana na Mwalimu hapo mnakuwa mmevaa nguo za nyumbani mnavunga kutembea style tofauti na za kawaida mwingine atatembea kama mchunga ng'ombe,kirema,Tahira ili kumchanganya tu mwalimu asiwafahamu maana Walikuwa wanakaa hapo hapo shule.
Kama kawaida za mwizi arobaini Wenzangu walinitangulia kuondoka baadae nikatoroka ile natoka tu maeneo ya shule Mala mbele yangu Headmaster huyo nikavunga kutembea kama kilema wa mguu mmoja kumbe keshanifahamu bwan:-
Headmaster-We si mwanafunzi wa Bweni?
Me-Ndio (nilijibu kwakuwa niliona keshanistukia)
Headmaster-Unaenda Wapi usiku huu wenzako wanasoma?
Me-Daftari limeisha na sabuni sikuwa na muda ndio nafuata hapo kibandani.
Headmaster-Sawa nenda uwahi kurudi.
Nikafurahi nikajua msara ushaisha ujinga na upumbavu wangu si nikajisahau nikatembea kawaida nikasikia sauti Bwana NtYga kesho uje ofisini (Tʖ̯T).
Sitasahau kipigo kile asee [emoji23][emoji23][emoji23]★
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] aisee nmecheka balaa... kweli kahawa ya njano ulitisha sana kwahyo wazazi walivojua ikawaje baadae
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] pole sana...
 
kugombania ugali.
kuvamia madisco ya mitaani na kuchukua mademu za watu.
ligi za kula chakula kingi.
 
Nakumbuka miaka ya 2016 nikiwa form three miaka hiyo.......
Shule ya boarding senti kunani huko mkoani
Hile shule bana kulikuwa Kuna miratiba ya kusali Mara nne kwa siku yani hadi kanisa linakuzoea jina....
So mzee baba la baba Kuna siku nikaamua kudoji Yan kutokuenda church asubuhi nikaendelea tu kuvuta shuka kilichonipata duhh hatari.
Kama kawaida maticha wanoko hawakosi kuwepo kila shule wenyewe tunawaitaga watumishi wa wenye mbinu za kijeshi so ticha katimba room kaanza kukagua wasioenda kusali ... Baba la baba si nikavuliwa Kama samaki ziwa victoria Mara paaaah!
Nipo macho kwa macho na mtumishi wa sherikali. Akaniamsha wewe? wewe?.... nikavunga kimtindo si mnajua tena..... Nikaona isiwe tabu wacha nijifufue. Ticha akanihuliza mbona ujaenda church ? Nikamjibu naumwa kidole. Ticha alicheka kinoma yani Alf baba la baba nikawa serious kinoma
Akaona isiwe kesi akanihuliza jina unaitwa Nani? Nikamjibu naitwa Paul Joseph...
Kumbe teacheri ananipata kinoma akaniambie wew si unaitwa ..... Mtu fulan
Nilipoona nishaumbuka nikamjibu Hilo ni jina langu la utotoni hahahahahahah et twende stafu akamwambia father recta uku akiwa anacheka
Tokea siku hile nikapewa jina la bashite mpaka namaliza shule siku ya graduashen niliitwa bashite upo? Nikaitika nipo father uku nikienda kuchukua cheti.
Sitosahau mkasa huu
 
hahahaha bweni gani hilo mwongozo au mapinduzi.

sema Anney mchizi sana
 
nikikumbuka karatu boys tulileta mgomo kisa simu zikiwa zimebaki siku tatu tupige necta form six daah wakafukuzwa watu ilibaki kidogo na mimi nisifanye necta asee.
 
Miaka 90s Jitegemee
mkifugua shule wiki nzima ni gwaride na kwata kwa kwenda mbele
 
Nilishachajia watu simu
Nilikuwa na access na funguo za duka, kila nikijaribu kuwakatalia wananilazimisha dah.. na hivi nilikuwa na huruma basi najikuta nimewasaidia ila kwa sharti moja!siku wakikamatwa wasinitaje kabisa kama wanachajia huku.

Siku Moto ukawaka sasa,mmoja si akaropoka kuwa anachajiaga dukani..Tumbo lilipata joto.
 
Kipingu alikuja kua headmaster wa makongo sec years ahead
Kipungu alienda kuianzisha Makongo sec kwa maombi ya JWTZ baada ya mafanikio ya Jite(JKT)
Alikuwa Sports Master Jite, Umiseta Dar es Salaam 1993, Tulishinda Football( Chanzo cha Tambaza Sec kufungiwa), Tulishinda Basketball, Tulishinda NetBall na Volleyball, kimkoa(Dar) tukapelekwa kula bata Mikumi National Park, duuuhh!! Jite ilikuwa miaka hiyo
Naona sasa Colonel Massawe ni RC Kagera, na Kipingu alieenda kwenye uongozi mambo ya Mpira sijui
 
Bahati mbaya nilishia la saba hii mada hainihusu
 
Mkuu Invisible unanifurahisha lakini ndio ukweli wenyewe. Disco likipigwa na mademu jamaa wanapagawa wiki moja kabla.
Haha mimi piah nimmoj wap kabla disco kale ka wik upol kama wote ili nipate nafasi ya kucheza na manz mzur
 
Haha Kuna cku nlifukuzwa ada,so kuna cool kids flani wakanishawishi tuende kwao,tulipofika tukaanza kupiga gambe nikazingua nataka kurudi shule. Dah bahati mbaya nlirudishwa sema mlinzi anafungua geti nakutana ana kwa ana na hedimasta..asee nlichezea fimbo na sasipensheni juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…