CRDB BANK: Huu ubabaishaji umevuka kiwango

CRDB BANK: Huu ubabaishaji umevuka kiwango

Crucifix

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2011
Posts
1,655
Reaction score
592
Nimenunua LUKU 50,000/= kupitia ebanking toka Jumapili saa 10 jioni hadi leo Jumanne nawasiliana nao kupitia ukurasa wao wa facebook wanasema niwe mvumilivu.

Huu ni upumbavu, dharau kwa mteja, kukosa weledi. Kwa sababu wanajua wateja hawana haki, hawawezi kushitaki popote, wanatuona mapimbi tu.

Basi, bora niuhabarishe umma; CRDB siyo benki ya kuiamini.
 
nadhani shida itakua TANESCO vs BENKI maana mimi pia niliunua upitia Exim bank nikaletewa sms " no response from service provider" (TANESCO). Hela ilikua ishakatwa wakanirejeshea. Nikanunua kwa aitel money ikakaa kama dk 10 ndio nikapata tokens
 
CRDB ni benki moja hadi nimeamua kutoa pesa yangu yote na kuachana nao mazima! Just imagine, unakuwa blocked kwenye internet banking kisha unawatumia taarifa zako zote kuanzia nakala ya passport, Visa Card, Last 3 transactions ili kuwaridhisha kwamba ni mmiliki halali wa akaunti husika na kwahiyo unaomba ufanye password reset lakini pamoja na yote hayo, wanakulazimisha uende branch!!

Pamoja na hivyo nikaamua kwenda branch! wakanitolea bank statement bila shaka hawakuwa na shaka kwamba akaunti yangu! Lakini nilipoenda kujaza fomu kwa ajili ya ku-reset password ya internet banking, unaambiwa nilisaini karibu mara 10 lakini mara zote hizo wanasema nakosea eti nisaini tena!

Nilihangaika ile siku hadi nikasusa na kuondoka zangu! Nilichofanya ni kutoa mpunga wangu wote, na kadi na kwa sasa sina hamu nao hata robo.
 
Mkuu hapa mie nakupinga hilo mwenyewe natumia hiyo huduma. Inabidi ujue ni ishu sensitive sana tena sana. Pia kama saini ukiikosea inatakiwa ifanane kama umeshabadilisha nenda kwa advocate uape kuwa umeshabadilisha.
 
Mkuu hapa mie nakupinga hilo mwenyewe natumia hiyo huduma. Inabidi ujue ni ishu sensitive sana tena sana.
Pia kama saini ukiikosea inatakiwa ifanane kama umeshabadilisha nenda kwa advocate uape kuwa umeshabadilisha
Unachopinga wewe nini? Kwahiyo kutumia huduma ni sawa na nilichosema? Kuna u-sensitive upi hadi uondoe mashaka yako zaidi ya mteja mwenyewe kuwa mbele yako over counter akiwa na docs zote ikiwa ni pamoja na mlizotoa wenyewe?

Yaani mteja yupo kaunta mbele yako! Amekuja kwako na kadi yenu wenyewe, valid government issued passport, ana bank statement mlioyomtolea wenyewe minutes ago; halafu mnaacha kumpa huduma hata baada ya kusaini zaidi ya mara 10 kwa hoja eti anakosea??! Hapo mnakuwa mnatafuta ku-prove nini hasa?

Hivi unatarajia digital signature unayosaini kwenye kioo itafanana 100% na signature unayosaini kwenye karatasi? Kama wapo sensitive kiasi hicho basi waanze kutumia dola gumba na sio signature!

And FYI, kuna mengine niliyaacha tu kuyasema for the sake ya Watumishi husika! Kuna huduma ambayo sikuisema hapa ambayo iliniweka pale kwa zaidi ya saa 3 hadi nikakata shauri la kuwapigia makao makuu ndipo walipo-attend!! Na ukitaka kujua nilikaa muda gani pale, jibu ni masaa 5, na kilichonipeleka pale sikufanikiwa!
 
CRDB sio benki ya kuaminika hata kidogo, mara elfu kumi ile AMANA BANK ya kina maalim
 
unachat fb kweli uyo mtu wa fb unakuta hata Bank hajui ipo sehemu gani? ye nikuchat tu uongo na ukweli ili maisha yaendelee
 
Crdb ni jipu sugu,,

Kuna siku nilifata barua ya kunitambulisha mimi kama mteja wao,,ili company yangu iweze kuingiza pesa ktk account yangu ya crdb.

Ajabu ni kwamba walihitaji shilingi 59000/ ,,

Just a letter ..!!!

Duu!! Aisee!!
 
Unachopinga wewe nini? Kwahiyo kutumia huduma ni sawa na nilichosema? Kuna u-sensitive upi hadi uondoe mashaka yako zaidi ya mteja mwenyewe kuwa mbele yako over counter akiwa na docs zote ikiwa ni pamoja na mlizotoa wenyewe?

Yaani mteja yupo kaunta mbele yako! Amekuja kwako na kadi yenu wenyewe, valid government issued passport, ana bank statement mlioyomtolea wenyewe minutes ago; halafu mnaacha kumpa huduma hata baada ya kusaini zaidi ya mara 10 kwa hoja eti anakosea??! Hapo mnakuwa mnatafuta ku-prove nini hasa?

Hivi unatarajia digital signature unayosaini kwenye kioo itafanana 100% na signature unayosaini kwenye karatasi? Kama wapo sensitive kiasi hicho basi waanze kutumia dola gumba na sio signature!

And FYI, kuna mengine niliyaacha tu kuyasema for the sake ya Watumishi husika! Kuna huduma ambayo sikuisema hapa ambayo iliniweka pale kwa zaidi ya saa 3 hadi nikakata shauri la kuwapigia makao makuu ndipo walipo-attend!! Na ukitaka kujua nilikaa muda gani pale, jibu ni masaa 5, na kilichonipeleka pale sikufanikiwa!
Pole mkuu hata mie wameshawahi nizingua pale Arusha Hq yao. Nilimkomalia yule Mdada nikamwambia si unaiona picha ni mie Huyo hapo. Kweli nilikomaa akawa mpole akaitoa Hela. Mie ni mteja wa crdb mkuu wala Sina his a nao. Wanachoniboaga ni Yale makato yao.
Kikubwa ungewakomalia mana kama Ungekuwa Umepata dili LA mana sana INA mana ungelikosa.
Mie huwa namaindi tena kwa sauti mpaka pale wateja wanaposimama nasikika mwenyewe.
Nawaambia haiwezekani Hayo mambo ninyimwe huduma.
Nilishaenda kwa lawyer kubadili signature ila pole Sana mkuu
 
SIJAWAHI KURIDHISHWA NA HUDUMA ZAO HATA KIDOGO, IMEFANYA NIHAMIE NMB AMBAPO NNA UHURU
NMB kuna kipindi cha nyuma kidogo nilienda kubadili pesa za kigenk nilichokutana nacho dah acha tu nikaamua kwenda BOA ambako nilishasema sikanyagi tena kwenye hiyo bank lakini ndiko nilipata huduma
 
Uliposema tu umewasiliana nao kupitia Facebook, moja kwa moja nkajua wewe ndio mwenye tatizo
 
NMB kuna kipindi cha nyuma kidogo nilienda kubadili pesa za kigenk nilichokutana nacho dah acha tu nikaamua kwenda BOA ambako nilishasema sikanyagi tena kwenye hiyo bank lakini ndiko nilipata huduma
Aisee, hizi bank zina changamoto sana
 
Nina mkopo nilichukua kupitia tawi la Rock City Mwanza Sasa wamekata njuruku zangu Kama laki hivi eti makato ya mkopo wakati muajiri wangu ndiye anawalipa kwa hundi Kila mwezi Mimi nawapa angalizo hela yangu irudi haiwezekani wachukue akiba yangu Kisha kuni block tarehe ngumu za 18 alafu nikawa field Bush huko kufungua tu Akaunti ilitakiwa elfu 18 hii haipo sawa nitoe Rai tu afisa mikopo jina kitu Kama Ipyana hivi rudisha hela yangu napambana wanangu wapate ada wewe unadonoa hala yangu kiulaini???
 
Pole mkuu hata mie wameshawahi nizingua pale Arusha Hq yao. Nilimkomalia yule Mdada nikamwambia si unaiona picha ni mie Huyo hapo. Kweli nilikomaa akawa mpole akaitoa Hela. Mie ni mteja wa crdb mkuu wala Sina his a nao. Wanachoniboaga ni Yale makato yao.
Kikubwa ungewakomalia mana kama Ungekuwa Umepata dili LA mana sana INA mana ungelikosa.
Mie huwa namaindi tena kwa sauti mpaka pale wateja wanaposimama nasikika mwenyewe.
Nawaambia haiwezekani Hayo mambo ninyimwe huduma.
Nilishaenda kwa lawyer kubadili signature ila pole Sana mkuu
Moja ya ujinga ambao nilikuwa nao ni kutofuatilia wanakata nini manake hata maintenance fee sifahamu wanakata kiasi gani ingawaje miaka ya nyuma sana nilishawahi kuzinguana nao kuhusu money transfer kutoka nje. Kama ilivyo uboya wangu, nilikuwa sikagui; sasa sijui ilitokeaje, sijui nilikuwa nimefulia; sikumbuki ila ninachokumbuka kwa wakati husika nilitoa statement ya miaka miwili na kuanza kukagua transactions zangu! Baada ya kukagua nikakuta ziliingia zaidi ya transfer 10, na kila transfer ilikuwa ina-miss $10. Ikawa kila nikiwauliza, hawana jibu la kueleweka; nikaisusa akaunti yako kwa zaidi ya miaka 2 kabla sijaanza kuitumia tena mwaka 2019
 
Back
Top Bottom