CRDB Bank: Tatizo ni kubwa

Asante

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2009
Posts
2,086
Reaction score
1,081
Nilifungua account benki ya CRDB mwezi wa March 2013. Waliniahidi kunipatia kitabu cha hundi baada ya wiki mbili.

Imebakia saa moja kuingia mwezi wa june 2013 wameshindwa kabisa kunipatia kitabu cha hundi, kila ukiwauliza wanatoa sababu chungu nzima.

Nashindwa kabisa kuelewa hii benki ilipataje tunzo ya super brand, miezi mitatu sasa hakuna mauzo ya vitabu vya hundi.

Ndugu zangu hivi huduma za benki zingine ni chafu kama ilivyo kwa CRDB Bank?

Najuta na kumlaumu aliyenielekeza CRDB, naomba msaada wa benki nyingine yenye mtandao mkubwa nchini niweze kuwasiliana nao.
 
Hilo libenk kwa nje huwa linajitangaza sana...lakini kwa ndani lina uozo sana...
 
Hilo libenk kwa nje huwa linajitangaza sana...lakini kwa ndani lina uozo sana...

Fikiria adha tunayoipata ukitaka kufanya malipo ni lazima uende kwa Manager na barua ya kuomba kuchukua pesa, uchukue cash ndipo ufanye malipo kwa wateja wako.
 
Uozo mwingine unapatikana pale CRDB - IRINGA BRANCH ....kitengo cha Maulizo! Yaan unaeza simama zaidi ya lisaa, wao wqnapitapita tu mle ndani wakiuza SURA! Mara ashike hiki aache hiki, Yaan kero mtindo mmoja! Akitokea mtu wanaemfahamu ndio bahati yenu wengine!
 
Na wafanyakazi wake wote wanajiona ni wakina kimei ful mazalau kuanzia mfuta numbi,tela had mpanga madaili ful pozi
 
Mkuu Asante bank za CRDB, NBC na NMB kuna vitu mameneja inabidi wavifanye kuna kero nyingi za kijinga....na wafanyakazi wao wengi wapo kama hawataki kufanya kazi(n way sisi watanzania kwa ujumla hatupendi kufanya majukumu yetu) unaweza kwenda pale kuuliza kitu mtu anaona kam unamsumbua...wakati mwingine mtu anakupa jibu la kukuondoa tu tu...na ni kwanini huwa wanaweka teller window nyingi lakini zinaudumia mbili au moja..?
 
Mkuu linapokuja suala la mabenki Tanzania service ni mbovu sana aisee. uzoefu unaonesha benki ikiwa changa huduma zinakua super sana ila ikishakamata matawi tu, balaa linaanza.
The more the growth the poorer the management and service. Kwa kifupi angalia hizo benki ndogo ndogo mkuu ambazo unaona zinaweza kuwa na manufaa katika utendaji wako na kampuni yako mkuu.
Ni hayo tu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
We kama mimi wananizingua sana ,huku kwetu MASASI ATM mbovu ,kadi yangu usiku ilizama ningekuwa na mgonjwa angekufa.Asubuhi wananipa majibu mepesi eti ATM inazingu.kitabu cha check wanipiga kalenda tu, kama wananipa bure vile!!! Kwenu Moshi hivi hiv???
 

Hii imenikumba juzi mkuu, wateja mnasimama kusubiri huduma ila wahudumu wanajipitisha mara huku mara kule ila akija mtu wanaemfaham ndo inakua bahati yenu.
 
Tuzo za supper brand nazo ni za hovyohovyo tuuu, wameipa blauzii fm, itv nazo kasoro kibao, mimi nadhani wajipange hao crdb coz ni benki inayotoa huduma vizuri kwa kiasi flani
 
hii bank ya kichaga inashida sana ...
 
we pia mzugaji ulichukua hatua gani baada ya kuona cheque book yako inachelewa je ulienda kumwona manager ukamwelezea tatizo lako jamaa wako poa huwezi linganisha na bank yoyote hapa ya kibongo adress tatizo lako sehemu sahihi wafanyakazi sio malaika mmoja mmoja anaweza kosea
 
Nimezunguka benki nyingi lakini hadi sasa nimeamua kutulia na Azania bank maana sijawahi kupata tatizo.
 
Mimi nime re-new card yangu toka mwezi wa kwanza hadi leo hii haijatoka.
 

Ni wangapi watakuwa wanaingia kumuona Manager?
Basi itabidi wot wafukuzwe aje atoe huduma Manager kama Teller na Customer Care
 
ukiangalia kwa umakini utakuta kingine kinacho haribu ni MAPENZI KAZINI ambako hupelekea mazoea ya kuona kama na wewe ni bosi kisa bosi ni mtu wako.na yeye pia kushindwa kuchukua hatua husika ni ktu wake.pamoja na hilo UNDUGUNIZATION NA URAFIKI NA KUTETEWA NA WAKUBWA AMBAO HUTAFUTIA KAZI WAPENDWA WAO.
 
Hizi benki zote uozo tuu!!foleni haziishi, wahudumu wanajipitisha tu na kujishebendua kisa mwajiri kabila moja shee!!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 

Mkuu kwanza pole
Lakini hii kusema ukweli si kawaida kwa CRDB unless kuna tatizo hujaliweka wazi, kwa kawaida CRDB cheque book ni ndani ya wiki moja kwa matawi ya DSM na wiki mbili kwa matawi ya nje ya DSM na hii ni kwasbabu Cheque book zote zinatengenezwa sehemu moja tu DSM

Ninauzoefu mkubwa na CRDB kwa hizi siku ni nyingi sana nakusahuri muone Branch manager mueleza nakuhakikishia akiitisha cheque book oder yako aone tarehe ulioomba utaipata siku hiyo hiyo kama upo DSM

Ni kweli wakati mwingine hizi Bank kubwa CRDB, NMB NBC zinakuwa na usumbufu fulani nahii ni kutokana na idadi kubwa ya wateja ilionao na mifumo ya kizamani inayotumika nna mabank TZ, lakini kwa issue yako imekuwa too much
 
Mimi Nilifunga account kwa ajili ya huo ujinga wao.. Ninashangaa sana watu wanaopata huduma katika bank hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…