CRDB bank yapata faida ya billion 236 mwaka 2020

Kinuju

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2021
Posts
2,386
Reaction score
5,325
Licha ya changamoto za corona zilizojitokeza, Benki ya CRDB imetangaza faida kabla ya kodi kiasi cha Sh236 bilioni mwaka 2020.

Faida hiyo, ni sawa na ongezeko la asilimia 35 ikilinganisha na Sh172 bilioni iliyopata mwaka 2019, kabla janga la corona halijafika Afrika na kuathiri biashara kwa kiasi kikubwa.

Baada ya kodi, faida ya benki hiyo ni Tsh165.18 bilioni iliyoongezeka kutoka Sh122.64 bilioni iliyopata mwaka juzi.

Mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela ufanisi huo umetokana na maboresho ya mifumo na mkakati wao wa kupunguza gharama za uendeshaji.

“Licha ya corona, biashara ilienda vizuri na mapato yetu yaliongezeka. Tuliijiimarisha katika maeneo tuliyokuwa na udhaifu,” alisema Nsekela.

Mapato ya benki hiyo yaliongezeka kutoka Sh774 bilioni mwaka 2019 na kufika Sh854 bilioni mwaka 2020 wakati akiba za wateja zikipanda kutoka Sh200 bilioni mpaka Sh5.4 trilioni katika kipindi hicho.

Faida ya benki hiyo pia ilichangiwa kwa takriban Sh15 bilioni na kampuni tanzu zake ambazo ni CRDB Burundi iliyopata faida ya Sh11.2 bilioni na CRDB Insurance Broker Limited iliyoingiza faida ya Sh3.6 bilioni.

“Mkakati wetu wa kuwasikiliza wateja na kuwaaidia kurejesha mikopo yao kipindi cha corona ulisaidia kwani ulituwezesha kuendana na mazingira yaliyokuwapo,” alisema Nsekela.

Mwaka jana benki hiyo ilikopesha zaidi ya Sh3.9 trilioni ambazo ni sawa na ongezeko la Sh500 bilioni ikilinganishwa na mwaka 2019 huku ikipunguza uwiano wa mikopo isiyolipika kutoka asilimia 5.5 mpaka 4.4.

Mkurugenzi wa fedha wa benki hiyo yenye zaidi ya wateja milioni tatu nchini wanaohudumiwa kwenye matawi yake 268, Fredrick Nshekanabo, alisema “tutaendelea kushirikiana na wateja wetu hasa waliopo kwenye sekta zilizoathirika zaidi na corona.”

CRDB ambayo mwezi uliopita iliboresha programu yake ya Simbanking ili kuwaruhusu wateja wapya kujifungulia akaunti mahali popote walipo au kwa mawakala wao 18,542 waliopo, in amtandao wa mashine 550 za kutolea fedha pamoja na vituo 1,900 vya mauzo vinavyofanya kazi kwa saa 24 wiki nzima.

Chanzo: Mwananchi
 
Makato makubwa ndio Mana wanapata faida wateja ndo tunaumia kwa kwel Yan mwaka huu naiaga CRDB kutumia huduma zao
Unaweza kuta badala ya benki kupata faida kubwa kutoka kwenye riba za mikopo wao wanatoa kwenye makato ya huduma zao.
 
Inawezekana siku za nyuma walikuwa wanatupa riport feki.

Kwa sisi wanahisa wa CRDB, Nimeshangaa kuona tangu mwaka jana tunapata Gawio kubwa kuliko miaka yote ya nyuma.
 
Bank zote mwaka huu zimepost faida kubwa.

NMB walipata 294B, CRDB 230.

Hii maana yake ni kua biashara imeimarika.

Kazi kubwa ya bak ni kutoa mikopo na kutoza riba, sasa biashara ingekua mbovu bank zimngemkopesha nani na wangetoa wapi riba?

Tukumbuke pia kua bank hizo zilishusha riba ya salalried loaners kama vile watumishi kutoka 22% hadi wastani wa 15%.

Watakuja misukule wa Mafia Boss Mbowe na kuropoka biashara mbovu, uchumi haukui, sijui utumbo gani.
 
CHADEMA ni wajinga sana
 
Ukiangalia salio = makato
Ukitoa hela = makato
Ukihamisha hela=makato
Ukikopa = makato
Ukihuisha kadi = makato

makato+makato+makato+makato+ uwekezajii =bilions of faida
 
Makampuni ya simu nayo yamepata faida ya billion ngapi mwaka huu
Voda
Tigo
Airtel
 
Hawa wana makato makubwa sana ndio maana wanapata faida kubwa ngoja nivizie na ATCL hata wakipata hasara wao wanatoa gawio tuu...
 
Ukiangalia salio = makato
Ukitoa hela = makato
Ukihamisha hela=makato
Ukikopa = makato
Ukihuisha kadi = makato

makato+makato+makato+makato+ uwekezajii =bilions of faida
Kwa nini usihame?
 
Unaweza kuta badala ya benki kupata faida kubwa kutoka kwenye riba za mikopo wao wanatoa kwenye makato ya huduma zao.

They make their profits from bank charges and not out of lending to customers!! Gavana wa BOT anasinzia kwani kwa mtindo huu finacial inclusion will shrink in the economy!
 
Licha ya changamoto za corona zilizojitokeza, Benki ya CRDB imetangaza faida kabla ya kodi kiasi cha Sh236 bilioni mwaka 2020.

Faida hiyo, ni sawa na ongezeko la asilimia 35 ikilinganisha na Sh172 bilioni iliyopata mwaka 2019, kabla janga la corona halijafika Afrika na kuathiri biashara kwa kiasi kikubwa.

Baada ya kodi, faida ya benki hiyo ni Tsh165.18 bilioni iliyoongezeka kutoka Sh122.64 bilioni iliyopata mwaka juzi.

Mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela ufanisi huo umetokana na maboresho ya mifumo na mkakati wao wa kupunguza gharama za uendeshaji.

“Licha ya corona, biashara ilienda vizuri na mapato yetu yaliongezeka. Tuliijiimarisha katika maeneo tuliyokuwa na udhaifu,” alisema Nsekela.

Mapato ya benki hiyo yaliongezeka kutoka Sh774 bilioni mwaka 2019 na kufika Sh854 bilioni mwaka 2020 wakati akiba za wateja zikipanda kutoka Sh200 bilioni mpaka Sh5.4 trilioni katika kipindi hicho.

Faida ya benki hiyo pia ilichangiwa kwa takriban Sh15 bilioni na kampuni tanzu zake ambazo ni CRDB Burundi iliyopata faida ya Sh11.2 bilioni na CRDB Insurance Broker Limited iliyoingiza faida ya Sh3.6 bilioni.

“Mkakati wetu wa kuwasikiliza wateja na kuwaaidia kurejesha mikopo yao kipindi cha corona ulisaidia kwani ulituwezesha kuendana na mazingira yaliyokuwapo,” alisema Nsekela.

Mwaka jana benki hiyo ilikopesha zaidi ya Sh3.9 trilioni ambazo ni sawa na ongezeko la Sh500 bilioni ikilinganishwa na mwaka 2019 huku ikipunguza uwiano wa mikopo isiyolipika kutoka asilimia 5.5 mpaka 4.4.

Mkurugenzi wa fedha wa benki hiyo yenye zaidi ya wateja milioni tatu nchini wanaohudumiwa kwenye matawi yake 268, Fredrick Nshekanabo, alisema “tutaendelea kushirikiana na wateja wetu hasa waliopo kwenye sekta zilizoathirika zaidi na corona.”

CRDB ambayo mwezi uliopita iliboresha programu yake ya Simbanking ili kuwaruhusu wateja wapya kujifungulia akaunti mahali popote walipo au kwa mawakala wao 18,542 waliopo, in amtandao wa mashine 550 za kutolea fedha pamoja na vituo 1,900 vya mauzo vinavyofanya kazi kwa saa 24 wiki nzima.

Chanzo: Mwananchi
Crdb = JPM
 
Faida inatokana na bank charges . CRDB ni bank yenye tozo kubwa sana kwa wateja.
 
Inawezekana siku za nyuma walikuwa wanatupa riport feki.

Kwa sisi wanahisa wa CRDB, Nimeshangaa kuona tangu mwaka jana tunapata Gawio kubwa kuliko miaka yote ya nyuma.
Team Kimei walikuwa wapigaji sana
 
Back
Top Bottom