...tatizo nikifungua website yao nikienda ktk option ya hiyo huduma kinachofunguka ni saver timeout. naomba msaada kwa wanaojua namna ya kutumia hii huduma au labda hawana hii huduma?.
Huwa inafunguka vizuri tu, labda kwa sasa wana tatizo la mtandao.
Huduma hii ya internet banking wanayo. Mimi ni mteja wao na naitumia sana tu. Kujiunga ni lazima uende mwenyewe kwenye tawi lolote la CRDB. Huwezi kujiunga online
Hata mimi nilihitaji hii huduma nikaambiwa kuwa lazima uende kwenye tawi lao na kujaza form. Ila wanatoa huduma mbili tofauti ambazo ni online banking na nyingine nadhani wanaita internet banking (sina hakika). Mojawapo inakuruhusu kuingia kwenye account yako kutokea kwenye website yao na kufanya transactions ila nyingine inakuruhudu kutumia kadi yako kununua vitu online. Ni muhimu kwenda CRDB ili wakufafanulie. Mimi sikuwa na muda wa kutosha kwa hiyo nilishindwa kujiandikisha.
Kutumia Visa card yako kufanya manunuzi online sio lazima huende kwenye site , una-swipe tuu kadi yako dukani au unaweka namba online.Hata mimi nilihitaji hii huduma nikaambiwa kuwa lazima uende kwenye tawi lao na kujaza form. Ila wanatoa huduma mbili tofauti ambazo ni online banking na nyingine nadhani wanaita internet banking (sina hakika). Mojawapo inakuruhusu kuingia kwenye account yako kutokea kwenye website yao na kufanya transactions ila nyingine inakuruhudu kutumia kadi yako kununua vitu online. Ni muhimu kwenda CRDB ili wakufafanulie. Mimi sikuwa na muda wa kutosha kwa hiyo nilishindwa kujiandikisha.