CRDB hii siyo haki. Ndo mambo gani haya?

Ulivyowauliza, and I assume umeshawauliza walikujibu nini ?

Nadhani pamoja na wizi wao hapo ndio tutapata mzizi wa fitina na jibu lao kwako litakuwa msaada kwa wengine watakaopata shida kama wewe zaidi ya kuonyesha umahili wao wa kukasirika na kutukana
 
Kila maboresho kuna makato? Ndivyo walivyosema?

Umenikumbusha case yangu na Tanesco siku moja, nimenunua umeme elfu 20k saa sita usiku nikaweka ukakataa, sikuelewa tatizo ninini… Nikanunua mwingine 10k ukagoma. Nikalala giza, Asubuhi nikaamka nao nikapiga simu eti ohh mara nyingi umeme ukinunua saa sita usiku huwa hauingii sijui nini nini kwahiyo fika ofisini nikajaze form ndio waifanyeje sijui hiyo token.

Aiseee nilifoka, nikamuuliza yule dada jana mlitu-notify wateja tusinunue umeme usiku? Jibu ni hapana, Nikamwambia kwahiyo kosa langu mimi mteja ni lipi nianze kutumia resources zangu kurekebisha makosa yenu? Nitoke kijitonyama hadi ofisi zenu mikocheni mtanilipia nauli? Muda wangu mtaulipa? Dada kaniambia huo ndio utaratibu… What!!!! Mimi nije sio nyie mnifuate?

Baada ya mabishano wakanitumia vijana/sijui mafundi wale wakaja na makaratasi rundo ya kujaza, wakajaza sijui wakafanyaje umeme ukaingia.

Sikuona utofauti wa huo usumbufu na tukio la unyang’anyi.. Nilipoteza masaa matatu kusumbuana nao kwa simu.
 
Mimi walinileteashida last week nilitoa hela atm hazikutoka kwenye mashine ila kwenye acc zilitoka wee niliwandikia barua kali wakazirudisha
 
Tumechukua pesa to crdb kwa ajili ya kampeni ya mama kizimkazi.......mama mitano tena!
 
Kwa nini watu hawatoi pesa zao CRDB?

Mbona NMB sisikii ujinga huu?
 
Na kila siku wanasema tayari wameshaweka sawa mfumo hawa wataua watu kweli kabisa.
 
Chai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…