CRDB mpo sawa kweli?

CRDB mpo sawa kweli?

clinician

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2014
Posts
2,098
Reaction score
4,926
Mwaka jana mwishoni nilikuwa na uhitaji wa Akaunti kwa ajili ya kuingiza vipesa fulani vinavyopita mara kwa mara.

Hivyo niliona vipesa hivi nivifungulie akaunti ya bank tofauti na ile nayotumia kila siku.

Nikaenda tawi la CRDB mkoani kwangu kwa ajili ya kufungua akaunti, kweli nilifungua akaunti haraka kwa Tsh 10,000 tu.

Kwa kuwa nilikuwa na mpango wa Kwenda Mwanza karibuni, nikaomba kadi yangu nikaipokelee huko Mwanza.

Bahati Mbaya ile safari yangu ya Mwanza ikachelewa, nimeenda Mwanza nikafika kwenye Tawi nililoomba kupokelea kadi yangu nikaambiwa mie nimechelewa kufuata kadi kwahiyo imerudishwa Makao makuu.

Nikaambiwa nitoe pesa Tsh 32000 (kama sijakosea) ili nitengenezewe kadi nyingine.

Huu ndiyo wazimu nilioona, nitoe elfu 32 kwa ajili ya kadi wakati naweza kwenda Bank nyingine mtaa huo huo nikapata akaunti na kadi kwa Tsh 10,000 tu?

Kadi yangu ilirudishwa makao makuu kwanini? Ni bomu kwamba likikaa ofisini linalipuka?
Kwanini wasimwambie aliyepeleka kadi makao makuu arudishe badala ya kutengeneza kadi nyingine?

Nyie CRDB mie ni baba yenu hata niwape pesa zangu kijinga namna hiyo?

Sasa hiyo kadi na akaunti kaeni nazo, Tsh 32,000 yangu siwapi.
Mtakuja kupelekewa pumzi za moto kwa kupenda hela zisizokuwa zenu.
 
Benki imekaa kijambazi jambazi sana hiyo. Mimi mwezi December nilishangaa nimekatwa elf 25 ambayo haina maelezo kuuliza kwa afisaa wa benki ananiambia hizo ni gharama za kutunza kadi sijui kukarabati. Ukizingatia wananikata mida wote ninapotoa hela nikasema kwasasa bora nikae na hela zangu ndani.
 
Pole sana...


Cc: Mahondaw
Hiyo charges sio bank wanaziweka Bali ni kwa wanaotengeneza kadi (Visa card/ Master card) ,kumbuka hizi Bank hazitengenezi kadi ndio maana ya kupata kadi mpya, kurenew iliyoisha muda, kutengeneza kadi mpya baada ya kuharibika/kupotea gharama ni TOFAUTI.
Muhimu tujue imekaa muda gani kabla hujaenda kuichukua.
 
Mtakuja kupelekewa pumzi za moto kwa kupenda hela zisizokuwa zenu.CRDB hapa someni polepole ndio mtaelewa😄😄😄
 
Back
Top Bottom