...Ongeza na hizi:
-Maintenance fee 700/= ( nina hakika hii wameishapandisha!)
- Withdrawal fee 500/= ( pia nadhani imeishapanda!)
- Visa ATM Charges 2000/-
- Mimi binafsi nina cheki ya shs 30,000/- ambayo huingia kila Ijumaa kwenye Account yangu na inapoingia tu jamaa wanachukua 1,500 kama Commission na mimi kubaki na 28,400/= kwa maana hiyo katika 120,000/= ya kila mwezi jamaa wanavuta 6,000/= zangu kama commission yao mbali na makato yote hayo mengine!! Dah. Naanza kufikiria sana kuhusu kuweka hela zangu chini ya Godoro!
-
toka nlipomalizachuo na bumu kukata sijawahi tumia hawa wapuuzi!!miaka 7 sasa
Unatumia benki gani mkuu kwa sasa? Huduma zao zinaridhisha?
NMB,for sure am enjoying!!tena nataka nifungue nyingine hapohapo,Fixed accnt
Mkuu mimi ni mteja wa NMB, CRDB na Exim Bank lakini pengine hujuwi vizuri makato ya NBM mkuu. Siku moja nimefika pale Bank house nikakutana na bango kubwa pale mlangoni limeorodhesha makato nilichoka. Nikajisemea "Benki hii si ya makabwela tena". Inawezekana hapo ulipo unapata huduma nzuri lakini kuna watu wako sehemu tofauti na wewe ukiwaambia habari za NMB hawataki hata kusikia. Na kama unataka kufungua fixed akaunti sikushauri ufungue NBM kwani faida zao ni ndogo ukilinganisha na benki zingine kama vile FNB (First National Bank - hawa ndo wanaongoza kwa faida kubwa kwa fixed akaunti) pia Exim ni wazuri kwa fixed akaunti.
Leo nilikuwa naperuzi account yangu ya CRDB through internet banking na nikashtuka kidogo na fees zao. Nimekutana na kitu kama ifuatavyo:
Monthly maintenance fee ........Tshs. 1,000
Card fee June ........................Tshs. 4,000 (hii transaction ya tarehe 9 July)
Card fee June ........................Tshs. 4,000 (hii transaction ya tarehe 13 July)
Withholding Tax .....................Tshs. 63.39
Nilikuwa sijanotice hivi vitax kwa muda na nashangaa kama huu ni utaratibu mpya. Kama wanamfanyia kila mteja namna hii, basi wanatengeneza faida ya hatari sana
ok. Kama uko wilayani sawa ila kama uko tanga mjini kuna exim bank ni wazuri kwa akaunti za watoto pia.
sina experince na exim bank
hivo nao ni wazuri??
Mkuu nilichojifunza ni kuwa benki zinatofautiana kutoka tawi moja hadi jingine ndani ya benki hiyohiyo kwa ubora wa huduma. Binafsi sijawahi kupata tatizo na hawa Exim. Na cha zaidi gharama za kuendesha akaunti ni ndogo zana ulinganisha na mabenki mengine.