CRDB na Uwakala wa benki

CRDB na Uwakala wa benki

rich1

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
3,020
Reaction score
3,309
Kwema wandugu?

Leo kero yangu kubwa nawapa CRDB, yani mtu unatoa kiasi kama kishika uchumba upate machine ya CRDB wanakaa na pesa yako karibia wiki mpaka wiki mbili kimya no machine (uwakala wa bank).

Nawaomba muwe serious kidogo.
 
Kwema wandugu....

Leo kero yangu kubwa nawapa CRDB yan mtu unatoa kiasi kama kishika uchumba upate machine ya CRDB wanakaa na pesa yako karibia wiki mpaka wiki mbili kimya no machine(uwakala wa bank)....nawaomba muwe serious kidogo.

ninavyojua siku hizi hakuna machine mbona, unatumia simu yako kufanya uwakala
sasa hata transaction za simu leo hakuna....ni zaidi ya 1 hour najaribu kutuma pesa inaniambia Namba ya unayotuma haipatikani, si kuhamisha kwenda kwenye simu wala Acc yenyewe ya CRDB!!
 
Boss wamekaa na 2.35M hata Mimi niliazima za mtu nikiamini siku hiyo hiyo ningepata POS Mzee ilikaa siku 5 mpaka nilijuta siunajua mitaji yetu ya kuunga
 
Uwe na tin na leseni unaenda tawi ulipo karibu nawe....zen machine n 350,000/= na uwe na cash ya deposit shs 1,000,000/=
Naweza kuomba mashine Mwanza alafu biashara nikaenda kufanyia Dar?
 
Naweza kuomba mashine Mwanza alafu biashara nikaenda kufanyia Dar?
Hapana hauwezi kwenda kuwaambia kitu kama hicho. Unachoweza kufanya ni kuomba uwakala wa Mwanza, kimsingi watakuja kukagua ofisi yako au wakati mwingine watakwambia utume picha za ofisi, utakapopata mashine unaweza kuhama (unofficial) kwenda kokote kule ila tatizo ni kwamba wewe utakuwa unasomeka uko Mwanza kwahiyo ukihitaji supplies kama rollers na slips itakuwa ngumu kupata huko ulikoenda. Kuna jamaa yangu alihama kutoka Mbeya kwenda dar akafanya kazi vizuri tu ila shida ikawa ni hizo rolllers na slips, lakini kwa sasa amefanya process ya kumhamisha taarifa zake kwenda Dar
 
Asante bro kwa taarifa.
 
Back
Top Bottom