KITALIKA Titho E
Member
- Jun 25, 2019
- 14
- 20
Je umekuwa ukijiuliza juu ya benki gani ina matawi mengi na waajiriwa wengi Zaidi nchini? Vipi kuhusu mali zake na faida ipatikanayo? Mchango wake katika bajeti ya serikali ni wa kiwango gani?
Kanuni ya saba na nane ya kanuni za mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2014 inayataka mabenki na taasisi za fedha kuonyesha kwa umma taarifa zake za kifedha kila baada ya miezi mitatu ya uendeshaji. Ikiwa imeshapita miezi tisa sasa, yaani robo tatu za uendeshaji wa taasisi hizi kwa mwaka wa fedha 2019 taarifa za robo tatu ya mwaka zipo hadharani na zitatusaidia inatosha ufanisi wa mabenki katika kukuza uchumi wa taifa letu.
Leo tuangazie taarifa za fedha za CRDB na NMB na tutazilinganisha kwa vigezo vitano yaani; mali, faida, ufanisi katika matumizi ya raslimali watu, vitu na fedha, kiasi kilichowekezwa katika hati fungani za serikali na idadi ya matawi. Muhimu kujua kwamba vigezo hivi vitasaidia kujibu maswali yafuatayo; ni benki ipi inatengeneza faida kubwa? Ni benki ipi imeikopesha serikali pesa nyingi? Ni benki ipi imeajiri wafanyakazi wengi? Ni benki ipi imeajiri wafanyakazi wengi?Lakini pia ni benki ipi inazitumia raslimali zake(watu, vitu na fedha) kwa ufanisi.
Mosi, Tuangazie faida ya mabenki haya mawili. Faida ni tofauti kati ya mapato na gharama za uendeshaji, kama ilivyo kwa biashara nyingine sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2014 inaelekeza makampuni kutozwa asilimia thelathini ya faida halisi ya uendeshaji kama kodi na hivyo kuchangia katika maendeleo ya taifa na watu wake.
CRDB ilijivunia faida ifuatayo kwa robo tatu ya mwaka huu wa kifedha; mwezi machi billioni 17.86, mwezi juni billioni 26.49 na mwezi septemba billioni 36.9. Wakati NMB ikijizolea faida kama ifuatavyo katika kipindi cha robo tatu; mwezi machi billioni 19.71, mwezi juni billion 36.5 na mwezi septemba billioni 25.4. Hivyo basi NMB ndiyo iliyotengeneza faida kubwa Zaidi kuliko CRDB na hivyo kutarajiwa kuchangia kodi ya mapato ya kubwa Zaidi.
Pili tuangazie ufanisi katika matumizi ya raslimali. Juma ya mali za CRDB na NMB mpaka robo ya tatu ilikuwa trioni 6.06 na trioni 6.12 mtawalia huku idadi ya wafanya kazi ikiwa 3277 na 3436 mtawalia. Hivyo basi ufanisi wa CRDB katika matumizi ya raslimali watu na fedha/Vitu kwa kila shilling millioni moja ya faida ni mara kumi na tatu(13) na mara ishirini na tano(25) mtawalia. Na kwa upande wa NMB ni mara kumi na tatu(13) na mara ishirini nan ne (24) mtawalia. Kiujumla CRDB imeendeshwa kwa ufanisi Zaidi ya NMB kwa kipindi cha miezi tisa iliyopita.
Katika kuangazia ufanisi wa undeshaji wa shughuli za benki ni muhimu tuangalie wastani wa mchango wa kila tawi na mfanyakazi katika faida ya benki husika. Tawi moja la CRDB limechangia wastani wa millioni 342.8 katika faida ya benki wakati tawi moja la NMB limechangia wastani wa millioni 364.3 kwa faida ya benki. Lakini hali iko tofauti kwa upande wa mchango wa kila mfanyakazi katika faida ya benki, Mfanyakazi mmoja wa CRDB amechangia wastani wa millioni 26.9 wakati kwa upande wa NMB ni millioni 23.6.
Tatu, tuangazie ni kiasi gani benk hizi zimeikopesha serikali kupitia manunuzi ya hati fungani za serikali kuu. CRDB iliwekeza kiasi cha shilling trioni 1.2, 1.2 na 1.1 kwa robo tatu za mwaka mtawalia wakati NMB ikiwekeza billion 820, 924 na 694 mtawalia. Hakika CRDB imeonyesha mchango mkubwa haswa katika kuiwezesha serikali kutimiza majukumu yake kwa kupitia uwekezaji huu. Uwekezaji wa CRDB ni sawa na asilimia tatu nukta sita (3.6%) ya bajeti nzima ya mwaka wa fedha 2019/20 wakati NMB ni sawa na asilimia mbili nukta nne sita (2.46%) ya bajeti ya mwaka 2019/2019.
Katika vigezo vitano tulivyo ainisha awali, CRDB imefanya vizuri Zaidi ya NMB katika uwekezaji wa hati fungani za serikali, idadi ya matawi, ufanisi wa wafanyakazi na matumizi ya raslimali fedha na vitu. NMB imekuwa ikifanya vizuri Zaidi katika wingi wa mali(watu, vitu na fedha), jumla ya faida kwa robo tatu na tengo la kodi ya mapato itokanayo na faida na mchango wa tawi katika faida ya benki.
Ni matumaini yangu kwamba Makala hii itakuwa imekupa mwangaza juu ya muono wako katika sekta ya kifedha hasa kwa benki hizi mbili kubwa na zenye historia iliyotukuka. Endelea kufuatilia Makala hizi wiki ijayo tutaendelea na benki nyingine mbili kubwa tukiangazia vigezo hivi hivi vitano tulivyo viangazia leo. Je ungependa kujua ni benki gani zitaangaziwa? Ambatana nami katika Makala ijayo.
Mwandishi wa Makala hii ni Mwanafunzi wa shahada ya pili ya Usimamizi wa mashirika, Mhasibu aliyeidhinishwa(CPA), Mhitimu wa Shahada ya Uchumi na fedha na ni mwajiriwa wa Benki.