Jamani CRDB mlikuwa mnasikiliza wateja zamani na si siku hizi. Nasema hivyo kwa sababu ya huduma yenu ya kuhamisha pesa kutoka kwenye account kwenda kwenye mtandao wa simu, huduma hii inachelewa sana, haina umuhimu tena kama kusudio lake. Una shida hospitalini unahitaji pesa kwa haraka unazipata kesho, inahitajika kuwepo kweli? Ukiwapigia customer care wanakuambia vuta subira kidogo, kidogo yenyewe kesho. Anzisheni huduma mkiwa tayari na si kukurupuka.