CRDB Visa Card: Utata wa matumizi yake mtandaoni


Aaaaghhhh!! Nilishajikatia tamaa zamaaaani!
 

Sasa mkuu wangu kuangalia salio lako kila siku itakusaidia nini kama mtu alishaweka disclaimer kuwa ukiibiwa huko mtandaooni utajiju? Je ukishagundua kuwa kuna transaction huitambui inakuaje? Wewe shukuru Mungu kuwa mpaka sasa bado hujagongwa na huyo nyoka. Najua benki zote duniani huwa zinamtaka mteja awe mwangalifu na hela yake. Lakini linapoingilia suala la tekinolojia hapo mteja wakati mwingine anakuwa hana ujanja zaidi ya kupata ushirikiano toka kwa banker.Mimi hao CRDB kwanza nilishasumbuana nao mpaka nikaamua kufunga akanunti yangu na za watoto wangu wote. Kibaya zaidi walikuwa wananiboa kwenye customer care (hawajali kabisa). Najua kuna baadhi ya matawi wanajitahidi, lakini matawi mengine wanajiona kama miungu fulani hivi. Just imagine hata suala la bank statement mtu anakudengulia ku print wakati ni haki yako.Utadhani tuko enzi zile za benki moja tu NBC. Kwakweli hiyo benk inabidi watu wabadirike.
 
pole sana. hatua katika perfection ya system zetu itachukua muda. tuvute subira wakati tukiendelea na mapambano
 
What if nikikariri zile namba 3 za nyuma kisha nikazifuta kutoka kwenye kadi yangu, inaweza kunilinda kidogo?

Wewe jamaa ni bonge la jiniasi ...

Kama unaona kuitunza kadi isiingie kwenye mikono ambayo si sawa ni ngumu, basi wazo lako ni bomba sana kama inawezekana ku kwangua pale bila kuiharibu sana kadi.

Kumbuka mikono ambayo si sawa inaweza kuwa ni kipenzi chako chenye tamaa, mtoto wako mtukutu, au ndugu yako aliyeshindikana ... Sio lazima awe mwizi, maana at least kama imeibiwa utagundua imeibiwa na utatoa taarifa. Soo ni pale mtu anachukua namba anakuachia kadi kama ilivyo.
 
Asante Manitoba kwa kuleta hili. Binafsi sijawahi kuiona CRDB kuwa benki bora. Kuna wengi wanaipigia debe kunishawishi nijiunge. Moyo unasita.

Ila karibuni hapa nilipata wazo la kuwa mteja wao, baada ya kuona mambo ya visa card ambayo unaweza kuitumia mtandaoni. I am out!
 
Mimi mwenye kusema kweli nilikuwa nimeshaitosa CRDB long time, nikaacha akaunti sijafunga just incase ikitokea ninaiitaji.

Kilichonikera wakati ule ni pale kadi yangu inaexpire kila mwaka halafu wananikata 8,000 kwa ku-renew bila hata kuniambia. Ukienda kuwauliza hii hela ya nini hapa ndio wanakwambia.

Sasa mwaka jana niliposikia hiyo Visa Card nikaona pengine muda umefika wa ku-renew hiyo kadi. Sasa baada ya hapo ndio chamoto nkakiona. tehetehe πŸ™‚ Ikafika mahali nikadhani mimi ndio nina mkosi mwanawane ... Saa nyingine nafika kaunter naanza kucheka kwanza nikiimagine yatakayonikuta dakika kadhaa zinazofuata.

Unajua jana nimekaa nikawa nacheka mwenyewe, nikakumbuka kipindi hicho hicho nasumbuana na CRDB, nikawa na kimeo cha TTCL. Yaani toka mwaka jana mwezi kama wanane nilipojaza fomu ya kwanza wiki iliyopita ndio line inafanya kazi. Mara fomu imepotea jaza nyingine (baadaye wakagundua ilikuwa missplaced), mara haiwezekani maana line zenu hazijafika huko, mara anakuja engineer kufanya survey, halafu husikii jibu ukienda kuwauliza wala hawajui kama kuna engineer amefika kwako, ... yaani ilimradi tu. Kuna mshkaji wangu akaniambia wape kitu kidogo tu utashangaa jinsi line itakavyofungwa faster, maana yeye yalimkuta kama hayo akarekebisha hivyo, bahati mbaya hata sijui jinsi ya kuanza. Huwa naonaga kumhonga mtu ni kama kumtukana, na sipendi kutukana watu πŸ™‚

Pengine matatizo kama haya ni ya watendaji, lakini kampuni inabidi ilaumiwe kwa kushindwa kuweka jinsi ya kuhakikisha watendaji wanatenda inavyotakiwa, na watambua pale inapokuwa visivyo. Wengeweka jinsi ya wateja ku-complain kwa mfano wanapokuwa wanapewa huduma mbaya ...

Kwa mfano kwenye ile issue ya kupata verification code ya paypal. Nilienda pale mlimani CRDB nikamwambia yule dada wa reception kwamba nahitaji details za transaction moja ya mwezi wa kumi. Harakaharaka akaniambia inabidi uombe statement. Nikamwambia ni transaction moja tu, akasisitiza tena statement huku akienda kwa mteja anayefuata. Kichwani ilikuwa wazi huyu dada either amechoka, ama kuna kitu wameboana huko, yaani psychologically hakuwa ametualia. Nikamuonea huruma tu.

Akabidi niwe mpole, niombe statement. Ilikuwa jtano akaniambia nije ijumaa maana inabidi ziwe-printed kwenye tawi langu (AZIKIWE ). Nikaongeza siku moja, just in case, nikaenda jmosi. Akaniambia bado hazijaja. Nikawasha moto kidogo na kuwakumbusha nimelipia 5,000TZS hiyo kazi ya kutoa statement, na sio bure, halafu nikamwabia dada mwenzake pale kwamba ninachotaka ni details za transaction moja tu. Unajua akasemaje "Sasa si ungesema?". Na kweli akanichekia, ingawa tukakuta hakuna details za paypal na kulikuwa na tatizo lingine, lakini kumbe inawezekana kuchekiwa transaction moja bila kuomba statement yote na kusubiri siku kadhaa. Sasa nimepoteza siku nyingine kusafiri mpaka pale, halafu nimepoteza siku kadhaa kusubiri jibu la kitu kidogo tu kwa sababu kuna muungwana mmoja amechoka, au yuko in bad-mood, au yuko kwenye siku zake.

Au labda wanaona raha watu mkiwa mnakujakuja pale mnaunga msururu mpaka nje waonekane wako busy sana.
 
nilishawishika sana kujiunga na CRDB baada ya kuambiwa mambo ya tanzanite account............dah nilipotaka kufungua hiyo account ilkuwa kasheshe mpaka basi......si unajua jamaa mpaka sijui wakuone umevaa kimamtoni mtoni ndio wanajua unatoka nje........pamoja na kuonyesha docs zangu bado nilisumbuka mpaka nikakata tamaa kabisaaa...........sitaki hata kuisikia tena.........very very poor customer service
 
Hawa jamaa wa CRDB pia nao wananikera sana kwenye hizi ATMS zao. Utatoa hela then hazitoki ukiangalia salio wameshakula. Ukiwasiliana nao wanakuambi usihofu zitarudishwa. Now inachukua mpaka a month kurudishwa hizo hela. Ukilalamika wanakuangalia kama vile we sijui vipi. Sasa kweli if you deduct my money from my account and you return it one month later hawajui kwa mtu kama mimi kipato changu ameharibu every thing on my budget. sasa sijui kwa nini hawan systeme ya kuhakikisha hiyo hela inarudi instantly????
 

5000 kwa ajili ya statement??!!huu ni wizi!!
 

Mkuu,

Hii ya kuchukua hela kwenye ATM halafu hela haitoki, halafu ukicheki salio unakuta wamekula imeshanitokea. Sijaelewa, huwaga nakaa chini nawaza na kuwazua, nadhani some things happens ONLY IN BONGO.

Hawa CRDB ni wasumbufu sana aisee.
 
Mimi ni mteja wa CRDB huu ni mwaka wa tatu, muda mwingi sana nimekuwa nje ya nje, ila katika vipindi vyote ambavyo nimekaa Tz, hakuna siku hata moja ambayo card yangu ya visa ya CRDB imefanya kazi. Kila nikienda bank aidha niambiwe card imekosewa nipewe nyingine. Nikapewa nyingine, tatizo likawa ni kwamba password niliyopewa haiendani na card... nimejikatia tamaa. Nafikiria nikirudi bongo, bora nijiunge na Barclays... sijwahi kupata nao shida kama CRDB....
 

...Kuna Bwana mdogo wangu mmoja yuko shule anasema kuna siku alitumia card yake ya Visa ya CRDB kuchukua hela kidogo ya matumizi kwenye ATM ya Barclays. Wiki mbili baadaye alipotaka kuchukua hela tena kwenye ATM ya CRDB mashine ikamuambia asingeweza kupata hela kwa vile alikuwa anadaiwa! Hela aliyoonyeshwa kuwa anadaiwa ndiyo aliyokuwa anafahamu kuwa ndio salio lake!!! Ni baada ya safari kadhaa kwenye tawi lake ndipo account yake ikafunguliwa kwa maelezo kwamba hela alizochukua kupitia atm ya Barclays zilikuwa hazijakatwa!!!! Anasema aliathirika sana kisaikoloji siku ile kwa sababu ni hela aliyokuwa akiitegemea sana! HIvi kuna Viongozi wa CRDB wanaoingia kwenye mtandao huu na kuona matatizo ya benki yao/yetu????
 
Duh kazi kweli kweli sijui bongo tutaendelea lini,lakini hilo si kwa CRDB tu hata Nmb we nenda Nmb House ukakutane na wateja 100 munahudumiwa na teller mmoja.
 


....Mkuu, naona kadi yako labda ilikuwa na gundu!! Mimi nilijaza fomu ya kuomba hiyo huduma na siku nne tu baadae nikapigiwa simu kwenda kuichukua, nikajaza mkataba na kuwaachia na masaa 24 tu baadae nikawa nina-purchase mtandaoni bila wasiwasi!!! Well, nilitaka kukujulisha tu hilo. Nisiendelee sana, Mgema wangu asije akatia tembo maji....! πŸ™‚
 


Point well noted! Thanks alot Manitoba!
 

lol ... usitake ncheke ... hata mimi nakuombea mgema wako asije akalitia maji.

Yeah kwa hilo la usumbufu inavyoonekana mimi ndio nilikuwa na gundu ... halafu labda inabidi nianze kuvaa suti na tai maana naona wanaovaa tai faster faster wanaruka mistari ... nawaonea donge mliobarikiwa kama wewe, kwa dhati kabisa.

Ila kwa hili la usalama wa kadi, mimi bado sijapata wa kunionyesha kwamba ni salama zaidi ya ninavyofikiria, au ni salama kama kadi nyingine zozote zinazotolewa duniani (kama baadhi yetu hapa walivyokuwa wanadai).

Na nirudie tena: sisemi CRDB wanatakiwa wazifanye salama kama issuers wengine duniani, ni biashara yao na mimi sio mshika dau wao. Ila natoa taarifa tu kwa watumiaji wenzangu kwamba CRDB hawajafanya hivyo, na ukweli ni kwamba wamefanya kinyume. Mwenye macho haambiwi tazama, lakini saa nyingine mwenye macho anaonyeshwa upande wa kuangalia.
 

Naunga mkono hoja. Kwa hakika, kwa jinsi nilivyousoma ule mkataba ni kama unakuwa umejinyonga mwenyewe na kadi yako. Nadhani they should be doing something better than this. Anyway, ngoja nijipe moyo kwamba 'Mwanzo mgumu'....!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…