Crdb waiba katika akaunti yangu

Msema yote

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2013
Posts
448
Reaction score
299
Mimi ni mteja wa CRDB BANK, leo nimefanya uhamisho wa pesa majira ya saa 4:20 asubuhi kutoka akaunti yangu ya benki hiyo kwenda M-PESA, nimesubiri mpaka nikachoka sijaona kitu hivo nikaamua kuwapigia VODACOM/M-PESA wakaniambia hakuna pesa zozote zilizoingia kwenye akaunti yangu ya mpesa hvo, wakanishauri niwasiliane na CRDB nikadanya hvo kwa kutafuta namba zao nikazipata ambazo ni 0755197700 na 0714197700 sasa cha ajabu kila nikipiga hiyo ya voda inakata nikaamua kupiga hyo ya voda inaita kisha inapokelewa na kukatwa bila mpokeaji kusema chochote, nikaamua kwenda kuangalia balance nikakuta hiyo hela niliotoa imekatwa, nikafanya tena mawasiliano na benki hiyo ila sikupata msaada, sasa wakuu naombeni ushauri wenu nifanyeje kuweza kupata pesa zangu hizo

Naomba kuwasilisha.

ANGALIZO
Nahitaji ushauri tafadhali kama unaona huna ushauri naomba upite tu kuliko kukashifu

MOODS NAOMBA MWACHE HII THREAD NIPATE UTATUZI WA PESA ZANGU
 
OK mbona ni rahisi sana kaka ww nenda crdb waombe bank statement utaona kama pesa imehama kutoka kwenye account yako na kama imehama na haijaingia kwenye acc yako ya mpesa then unafanya mawasiliano na vodacom pia itajulika ina hang wapi kaka pesa yako hawezi kupotea
 
Hizi benki sijui kama wali fanya utafiti wa kutosha kabla ya kujiunga na hizo huduma za mobile money na makampuni
ya simu,naona kesi zimekuwa nyingi sana...ngoja tusubiri waje ila kama huna matumzi sana usijiunge na hizo huduma
 
Nashukuru kwa ushauri wenu wakuu ngoja niwarudie tena kisha ntawafahamisha kinachoendelea
 
...Niweke wazi tu kwanza mimi ni Mteja wa CRDB kama wewe Mkuu.Kuna maswali kadhaa ya kujiuliza kabla huja-panic sana kuhusu hili:
Je hii ni mara ya kwanza kuitumia hiyi huduma?
Kama sio mara ya kwanza, ina maana huko nyuma umeishawahi kuitumia na hukupata matatizo yoyote sio??
Maelezo yako ni kama unaunganisha kupotea pesa zako na kukatwa simu yako inapojibiwa, lakini elewa kuwa huo utakuwa ni uzembe wa huyo mpokea simu tu na si kwa sababu anajua kuwa umeibiwa na hivyo hataki hata kusikia unachotaka kusema! Fahamu Mpesa na Switchboard ni sehemu mbili tofauti.

Mimiimeishawahi kunitoke mara 2 hali ya kutuma pesa isiingie kwenye simu yangu lakini iwe imeondolewa kwenye accaount yangu ya CRDB.
Hiyo mara ya pili ilichukua karibu masaa 16 kupata hela yangu kuanzia jumamosi saa 11 jioni hadi jumapili saa Tano mchana!
Jema ni kwamba nilifuata taratibu hizo hizo ulizofuata wewe na bahati njema zaidi ni kuwa mimi nilipokelewa kwenye hizo namba unazosema na kuelezwa kuwa kuna mtu alighafirika na kusahau kufanya alichotakiwa kufanya ili hela ihame!
Waliomba radhi kwa hilo na nikakubali yaishe kiungwana.
Naamini hela yako ipo.
Kazana kupiga hiyo namba ama ukiona vipi sogea kwenye tawi lolote la CRDB lililo karibu nawe ueleze madhila yako na ninaamini utapata Uchache (Wingi????) wako!
Utujulishe Kitakachoendelea.
Pole sana Mkuu.
 
kuna complains nyingi za kupotea kwa fedha kutoka mabenki kwenda tigo money,airtel money na mpesa ushauri wangu kama unataka kuhamisha fedha nenda kachukue fedha physically kutoka atm ya banki yako na peleka kwa agent wa mpesa ili uendelee na matumizi yako!!!
 
Mimi wameshaniibia sana hao crdb, benki hizi za
kizawa ni utapeli na wizi mtupu, customer care yao
mbovu sana, nilochokifanya ni kuhamia Barclays na
kuachana nao, solution hapo ni kuachana nao tu
 
Mimi sijui ni ushamba ama nini yaani hata hizo tigopesa wala mpesa sijawahi kujiunga kabisa, tena ukileta hizo habari za internet banking ndiyo sitaki kabisa
 
Ulihamisha saa ngapi? Make muda mzuri ni kuanzia asubuhi saa mbili hadi jioni. ukihamisha usiku inatokea hivyo na ukiwailiza wanakuambia systeam inakua imezimwa. ila utarudishiwa tu. make mimi mara zote ilirudishwa. na hizo namba usipige muda ambao sio wa kazi make hupati mtu.
 
Mimi sijui ni ushamba ama nini yaani hata hizo tigopesa wala mpesa sijawahi kujiunga kabisa, tena ukileta hizo habari za internet banking ndiyo sitaki kabisa

Huduma kama sim banking ni nzuri sana, unaweza usiende bank au kweny ATM zao kabisa
 
Acha kupaniki mleta mada pesa huwa inarudishwa. Mimi ishanitokea wala sikupaniki, na wala sikuwapigia simu kwakuwa nafahamu kuwa "technology is not perfect". Pesa yangu iliingia siku ya pili yake kwenye mpessa. Halafu jifunze kuwa na subira sio unakimbilia kurusha shutuma kwa kusema crdb wezi kabla hata hujathibitisha kama umeibiwa au laa. Kumbuka, HEKIMA BORA ZAIDI, Kuliko lawama. "Mara nyingi Subira ni sehemu ya hekima. Asiye na subira hana hekima" Tarakilishi 2013
 
Kuhamisha pesa kutoka CRDB kwenda M-Pesa ni tatizo kubwa sana, pesa zinachelewa kufika. Pesa utaipata ila tegemea kuanzia kesho mida ya saa 5 - 7 mchana. Mimi imeshanitokea kama mara nne sasa.
 
Mimi wameshaniibia sana hao crdb, benki hizi za
kizawa ni utapeli na wizi mtupu, customer care yao
mbovu sana, nilochokifanya ni kuhamia Barclays na
kuachana nao, solution hapo ni kuachana nao tu
hhaahaaa hao nao ni wale wale mkuu hamia MBULULA COMMERCIAL BANK ULE RAHA USIOGOPE KUKUTA MENO YA WACHAGA YAMEOZA PALE NDIO VICHWA VYENYEWE
 
Eti meno yameoza! Mbona mgomvi hivyo?
hhaahaaa hao nao ni wale wale mkuu hamia MBULULA COMMERCIAL BANK ULE RAHA USIOGOPE KUKUTA MENO YA WACHAGA YAMEOZA PALE NDIO VICHWA VYENYEWE
 

Kaka unakosea......hii product bado ni changa apa kwetu Tanzania nikimaanisha aina mwaka,ivyo matatizo ya ela kutomfikia mlengwa muda muafaka au kutokufika yapo ila in long term yatapatiwa ufumbuzi.hii product ni mapinduzi makubwa and its an african born technology.........Benki aina haja ya kukuibia cjui laki mbili zako au elfu hamsini
 

...HAWA CRDB SASA WAMANICHEZEA.
Toka jana nimefatilia mpaka leo sijapata kila nikienda naambiwa niwe mvumilivu sasa leo tena nimekwenda naambiwa niende kesho hivi huu si ni wizi wa mchana kweupe,
SASA NAHITAJI KUWASHITAK KWA UBADHILIFU WALIONIFANYIA HIVO NAOMBENI MSAADA WA KISHERIA WAKUU NIANZE VIPI KUWAFUNGULIA KESI

MAONI YENU NI MUHIMU SANA KWANGU ASANTENI,
 

Nilihamisha jana saa nne asubuhi mkuu
 
Mimi sijui ni ushamba ama nini yaani hata hizo tigopesa wala mpesa sijawahi kujiunga kabisa, tena ukileta hizo habari za internet banking ndiyo sitaki kabisa

Nilihamisha toka jana saa nne mkuu
 

piga ya TTCL ndiyo reliable
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…