CRDB wanakwama wapi?

CRDB wanakwama wapi?

Watika

Member
Joined
Feb 9, 2014
Posts
19
Reaction score
18
Habari wakuu,

Kwa wazoefu au wenye umelewa wa hili jambo, na ni kawaida kwenye baadhi ya mikoa. Nilichokikuta mkoa huu ni ajabu.

Niliwasili Morogoro usiku wa saa nne. Nikawa na uhitaji WA pesa. Kitu cha Kwanza kufikiria ni kwenda ATM.

Nilichoshuhudia ilikuwa ajabu sana kwangu. Nimezunguka kuanzia msamvu mpaka Morogoro mjini yote, ATM zote hazina pesa. Nilipata hasira kuteseka na pesa zangu mwenyewe. Hawa wenzetu wanakwama wapi. Je, Wana wateja wa kutosha so wamerelax?
 
tatizo umekariri maisha
CRDB wana mawakala wa mtaaminkila sehemu,sim banking pia wanayo,basi tu unapenda shida
 
Mtoa mada yupo sahihi naona watu wanacomment bila kufikiria. Yeye ameshasema amefika Moro usiku, unadhani ni wapi angepata wakala kwa muda huo, lakini pia simbanking ina kiwango cha mwisho je mnajua ni kiasi gani alihitaji?.
Mwisho wa siku uwepo wa mawakala au simbanking usihalalishe uwepo wa fedha kwenye ATM.

Mimi pia yalishanikuta, unaenda kwa wakala anakwambia hana salio la kutosha.

CRDB lazima wabadilke.
 
Mkuu unakujaje bila kutoa taarifa kwa wenyeji? Pole sana, nadhan huwa inatokea,,ungehamisha pesa kutoka CRDB kwa kutumia sim banking, halafu ukatoa kwa wakala, ama ukaenda kwa mawakala wa CRDB ukato huko pesa yako.

ATM ya masika huwa iko vzuri wakati wote, sijui nini kilitokea! Pole sana mkuuu
 
tatizo umekariri maisha
CRDB wana mawakala wa mtaaminkila sehemu,sim banking pia wanayo,basi tu unapenda shida

Hizo nauli ulizotumia kuzunguka mji mzima ungejiongeza mapema ukatumia huduma za MasterCard au CRDB wakala usingelalamika hapa.

Mbona mnachangia wakati hamjamuelewa vizuri mleta mada kasema alifika morogoro usiku wa saa nne, hao mawakala angewapata wapi muda huo? Ndio maana kaamua kutumia MasterCard yake kutoa hela zake[emoji23]
 
Mawakala wa hz bank wananiachaga hoi sana.... ukihitaji kutoa hela akiwa hana salio eti anakujib mtandao unasumbua kumbe yeye ndo hana flot,Yan jibu hili linakukatisha tamaa kbs usiende pengine
 
Kwahiyo unataka kuniaminisha kuwa Morogoro kuna matajiri sana wanamaliza hela kwenye ATM au!??


Kichwa BoX
 
Kwahiyo unataka kuniaminisha kuwa Morogoro kuna matajiri sana wanamaliza hela kwenye ATM au!??


Kichwa BoX
Au kuna masikini sana mpaka Benki zinaona uvivu kuweka Pesa kwenye ATM..
 
Of recent CRDB wamekua wakiwaangusha sana wateja wao. Juzi kati kadi yangu ilimezwa kwenye moja ya atm’s . Niliambiwa nisubiri wiki moja ndo niende nikachukue. Siku nimeenda kuchukua yani wanajizungusha wee, fomu nimejaza ila naona wao wanajizungusha tu. Yani kuchukua kadi yangu iliyonasa kwa atm ikichukua karibu saa nzima . Ila niliwatolea uvivu, niliwapa makavu live halafu nikawaambia wakiwa tayari wanitafute namba zangu wanazo. Hii bank ufanisi wao upo chini sana siku hizi, sio kama ilivyokua zamani. Kama mupo humu hebu badirikeni
 
Huna simbanking unaingia kwa wakala unavuta muamala unaendelea na mishe zako.
 
Back
Top Bottom