CRDB yaanza kuuza hisa zake DSE

CRDB yaanza kuuza hisa zake DSE

Andindile

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2009
Posts
304
Reaction score
17
Makubo Haruni, Musoma; Tarehe: 20th April 2009 (Habarileo)

Hisa za benki ya CRDB zimeanza kuuzwa kupitia Mtandao wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) toka jana ambapo sasa wananchi wote wana fursa ya kuzipata. Awali hisa hizo zilikuwa zikiuzwa kwa wanahisa wa benki hiyo waliokuwapo kabla ya benki hiyo kujiunga na DSE.

Mkurugenzi wa Huduma za Benki Makao makuu ya CRDB, Joseph Witts, alisema hayo wakati alipokuwa akijibu moja ya maswali ya wanahisa wa benki hiyo mkoani Mara waliotaka kujua pamoja na mambo mengine mpango wa benki hiyo kuongeza wigo wa uuzaji wa hisa hizo kwa lengo la kuboresha huduma za kibenki hapa nchini.Mkurugenzi huyo aliwahakikishia wanahisa hao waliohudhuria mkutano wa 14 wa benki hiyo mjini Musoma kwamba CRDB imekamilisha taratibu zote zinazoiwezesha kuanza kuuza hisa hizo kwa wananchi wote.

Witts alisema hisa hizo sasa zitakuwa kwenye soko hilo na kuongeza kuwa sheria inaruhusu mwanahisa kuuza hisa zake. Bei ya hisa moja kutoka CRDB inauzwa kwa Sh. 150.
Aidha aliwatoa wasiwasi wanachama waliohoji iwapo kuna madhara yoyote ya kifedha katika benki hiyo yaliyotokana na kuyumba kwa uchumi duniani na kuwahakikishia kuwa fedha za wateja ziko salama na zimetunzwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Ndugu zangu wenye vijisent ni wakati wa kuchangamkia tenda. Baada ya sakata la DECI twendeni tukapande CRDB labda huku italipa ingawa hawaifikii DECI ila usalama wa pesa ni 'wakuridhisha kiasi" Bei yenyewe si mnaiona ilivyo ya chini. muda si kitambo itapanda kwenda juu.
 
Back
Top Bottom