ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 150
- 173
"UGLY FACES" WALIVYO WAPIGA MASHUTI "WAPAMBE NUKSI"
_________________
"Wapambe nuksi wapingwe mashuti...!!
Eeeh Wapambe nuksi wapingwe mashuti..!!!
Wapambe nuksi wapingwe mashuti...."
🎶🎶🎶🎶🎶🎶
"Wapambe Nuksi" ni moja Kati ya hit Song moja kali sana ambayo ilitutambulisha sisi kama " Ugly faces" kwenye Ramani ya Muziki Enzi hizo kwenye Kiwanda cha Muziki wa Bongo Fleva..
Nyimbo hii ya "Wapambe Nuksi" sisi kama Crew ya "Ugly faces" Tulizungumzia wale "wapambe" Waliokuwa wanapatikana mtaa wa " ilala " Enzi hizo..
ambao walikuwa na ukaribu/ Urafiki na Wazungu Kutoka Ughaibuni , Wazungu ambao walikuwa wanajihusisha na Uuzaji wa " ndumu" & Drugs( madawa ya kulevya)..
mtaani Kwetu "Ilala" miaka hiyo ..
Kwahiyo wale Wazungu Enzi hizo kutokana " Ughaibuni" walikuwa wakitoka huko Ughaibuni na kuja Hapa Bongo Dar es Salaam, mtaani kwetu " ilala" Kulikuwepo Tayari na wale "wapambe Nuksi"
Ama kwa jina lingine ( machawa) unaweza kuwaita kwa msemo wa leo...
Wale wapambe Nuksi walikuwa na Nguvu kubwa sana ya Ushawishi wa kusikilizwa na hao Wazungu wauza Madawa ya kulevya kutoka. " Huko Ughaibuni"
Kwahiyo wao " wapambe Nuksi" ndio walikuwa wanatoa maelekezo kwa Boss..
Utasikia Tu vijimaneno Ooh !! Msaidie huyu na wala usimsaidie Huyu !! Kwa kifupi Walikuwa na Nguvu ya kusikilizwa na " Ma Boss" .
"Yaani !! Ilikuwa hivyo na ukitazama wale Wazungu kutoka ughaibuni walikuwa vizuri kifedha , kwa kifupi "wapambe Nuksi " kwa miaka ile ya zamani Tunaweza kusema ni kama hawa wanajiita " machawa" kina Baba levo & mwijaku lifestyle zao zilivyo ..
"Haya ni sehemu ya Mashairi / lycris zilizopo katika wimbo huo wa " Wapambe nuksi"
"Remember i was born bongo tafu,yala ooh!! Yala ooh!!.../ hapana Eh!!!...Kufa kufa kwa namna hii/ kaa chocho saa mbaya wewe mpambe huna Aya!/ ....Zungu likishuka wapambe wanalizunguka/ usipoenda huku watu wanakushawishi/ kiulani.....,/ na wote walichomoka...!!/ utakuja kushtukia wapambe Wana kula corner / pembeni una No ng'ona Zungu lime chacha linauza kashata.."
Halafu kuna nyimbo nyingine tulishafanya inaitwa " Wacha kuchachatika.."
( kuangaika)
Yaani..!! kama una kitu kimoja unataka kufanya fanya kwanza.. au shika kimoja
Nyimbo hii ilikuwa inazungumzia gonjwa la " ukimwi" na ukitazama kwa jicho la pili miaka ile gonjwa la " ukimwi" lilikuwa ni gonjwa hatari mno , vifo vya kutokana na Gonjwa hilo vilikuwa vingi sana, kutokana na kwamba kwa wakati ule kulikuwa hakuna Tiba wala vidonge vya kupunguza makali ya v.v.u (A.R.V) kwahiyo watu walikuwa wakipata maambukizi ya virus vya ukimwi ujue ni maumivu tu baada ya muda fulani..
Wasanii wengi pia Enzi hizo nao walikuwa mstari wa mbele Ama sehemu ya utoaji wa Elimu juu ya hili Gonjwa na Kazi nyingi zilitolewa na wasanii kuhusu virusi vya ukimwi ..
Na sisi kama " ugly faces" tukasema tufanye kitu.. ndio tukatoa huo wimbo unaitwa " Wacha kuchachatika" ( kuangaika)
kama una kitu kimoja unataka kufanya fanya kwanza.. au shika kimoja
Ili kutoa ushauri kwa jamii kwamba waache kufanya Ngono bila kinga na vitu vingine kuhusu mahusiano
....."Yaani wabaki njia kuu kama ilivyokuwa kauli mbiu ya "ishe kampeni"
Enzi hizo..
Na nyimbo nyingine Tuliotoa kama " Ugly faces " ilikuwa inaitwa "Funky fat " hii nyimbo tuliimba kwa lugha ya kiingereza..
Washkaji zangu wa "Ugly faces" niliyoimba nao hizi nyimbo mmoja anaitwa " Eazy Dazz na mwingi Richard mack " rich mack " huyu alikuwa sio mwimbaji alikuwa kama vile kaka yetu Ama kiongozi wetu katika Crew ya" ugly faces !! ..
UKWAJU WA KITAMBO
0767542202