Cristiano Ronaldo aendelea kutisha ndani na nje ya uwanja anunua gari la bei kubwa katika historia ya dunia bilioni 43 hakuna mwingine atakayelinunua

Course Coordinator

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2019
Posts
1,742
Reaction score
3,224
Lijue Gari ghali zaidi duniani, Cristiano Ronaldo atajwa kulinunua

Hili gari, Bugatti La Voiture Noire ndilo gari ghali zaidi katika historia ya dunia, likiwa linagharimu US Dollar Milioni 18.7 sawa na Tsh. Bilioni 43.1.

Gari hili lilizinduliwa Machi 5 mwaka huu kwenye maonyesho ya magari ya kimataifa, Geneva International Motor Show kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa kampuni ya Bugatti.

Wakati wa uzinduzi wake, gari hili tayari lilikuwa limelipiwa na mnunuzi ambaye hakutaka kujulikana. Bwana huyo alilipia gari hilo hata kabla kutengenezwa kwenye kiwanda.

Kuna fununu ambazo zingali hazijathibitishwa kwamba gari hilo lilinunuliwa na nyota wa soka Cristiano Ronaldo.

Gari hili ambalo lina injini yenye ukubwa wa 8,000cc na turbo nne, linabeba abiria wawili na linaweza kuenda kasi ya kilomita 465 kwa saa. Kampuni ya Bugatti ilitengeneza toleo moja pekee ya La Voiture Noire. Hivyo basi hakuna mwingine atakayekuwa na gari sawa isipokuwa aliyenunua hili toleo.

Watu wana hela ila hela hazina watu...mwandae mwanao awe mcheza soka akishindwa masumbwi pesa zipo nje nje.
 
Ujinga ulizaliwa na fahari.
(sio maneno yangu, wahenga hao!)
 
Back
Top Bottom