Cristiano Ronaldo aongoza orodha ya wachezaji wenye gharama na ushawishi duniani

Cristiano Ronaldo aongoza orodha ya wachezaji wenye gharama na ushawishi duniani

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1663697550186.png

Wakati Kombe la Dunia likibakiza miezi miwili kuanza, tayari inaonekana nyota wa Ureno na Manchester United Cristiano Ronaldo ataingia kwenye michuano hiyo akiwa mchezaji mwenye nguvu zaidi duniani kwa kuzingatia ushawishi wake kwenye mitandao ya kijamii.

Ronaldo amewapiku mastaa wengine kama Lionel Messi na kuongoza orodha iliyokusanywa na wachambuzi wa vyombo vya habari vya michezo Nielsen, ambayo ilitathmini wingi wa wafuasi wa Instagram wa wachezaji wote wakuu na timu zilizopangwa kushiriki Kombe la Dunia nchini Qatar.

Utafiti uliofanywa na taasisi ya Nielsen Gracenote pia umewataja nyota 10 wa Soka ambao wanaolipwa pesa nyingi kwa kila bandiko wanaloweka kupitia mtandao huo

Ronaldo ameongoza orodha hiyo akiwa na wafuasi wa Instagram Milioni 480 na akilipwa zaidi ya Tsh. Bilioni 8 kwa post moja ya kibiashara kwenye mtandao huo

Orodha hiyo imewajumuisha nyota wengine akiwemo Lionel Messi, Kylian Mbappe, Neymar, Vinicius Junior, Karim Benzema, Paulo Dybala, N'Golo Kante, Paul Pogba na Sergio Ramos.

1663699914041.png
 
Yaani akipost tangazo moja unamlipa Bilion 8 sasa si tayari ajira hiyo.
 
Back
Top Bottom