Cristiano Ronaldo avunja simu ya shabiki wa Everton, aomba radhi, Polisi waingilia kuchunguza

Cristiano Ronaldo avunja simu ya shabiki wa Everton, aomba radhi, Polisi waingilia kuchunguza

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Polisi wa Merseyside wamethibitisha kuwa wanafuatilia taarifa ya tukio ambalo Cristiano Ronaldo wa Manchester United anatuhumiwa kwa kuikwapua simu ya shabiki wa Everton na kuivunja.

Tukio hilo inadaiwa lilitokea jana Aprili 9, 2022 baada ya Man United kufungwa bao 1-0 na Everton kwenye Uwanja wa Goodison Park katika Premier League ambapo Ronaldo aliomba radhi kupitia ukurasa wake wa Instagram

Ronaldo amesema anamkaribisha shabiki huyo kutembelea Uwanja wa Old Trafford wakati wowote United itakapokuwa inacheza. Shabiki huyo alikuwa akimpiga picha Mreno huyo wakati akireja vyumbani baada ya mchezo.

Source: Daily Mail

Ronaldo anapokuja kuniangusha ni hapo kwenye kushindwa ku control temper zinazompelekea kufanya maamuzi ya ajabu kupitia panic zake
Dogo alikuwa anataka kupiga picha jeraha la mguuni la Ronaldo halafu pia kulikuwa na maneno ya matusi kumshambulia Ronaldo na wachezaji wote wa United.

Ronaldo na yeye ni binadamu kama sisi tu kuna muda mtu unashindwa kuji-control na naamini ni mara nyingi sana anajitahidi kuficha hisia zake kwasababu inabidi alinde brand yake ila alichofanya jana ni kitu cha kawaida tu kutokea kwa mtu.
 
Ronaldo anapokuja kuniangusha ni hapo kwenye kushindwa ku control temper zinazompelekea kufanya maamuzi ya ajabu kupitia panic zake
Hapo hata Messi alishawahi kupigwa chenga na kumsindikiza Mtu na konde [emoji38]
 
shabiki kalamba dodo.
kwanza anafungua kesi ya kuathilika kisaikolojia na simu yake kulipwa pesa kubwa kama hii
IMG_6072.jpg
 
Huyo shabiki aliruhusiwa na Ronaldo mwenyew ampige picha?
Ni sawa tu CR7 alichofanya
 
Ronaldo anapokuja kuniangusha ni hapo kwenye kushindwa ku control temper zinazompelekea kufanya maamuzi ya ajabu kupitia panic zake
Hata will smith anazo hizo tambo..
 
Back
Top Bottom