Polisi wa Merseyside wamethibitisha kuwa wanafuatilia taarifa ya tukio ambalo Cristiano Ronaldo wa Manchester United anatuhumiwa kwa kuikwapua simu ya shabiki wa Everton na kuivunja.
Tukio hilo inadaiwa lilitokea jana Aprili 9, 2022 baada ya Man United kufungwa bao 1-0 na Everton kwenye Uwanja wa Goodison Park katika Premier League ambapo Ronaldo aliomba radhi kupitia ukurasa wake wa Instagram
Ronaldo amesema anamkaribisha shabiki huyo kutembelea Uwanja wa Old Trafford wakati wowote United itakapokuwa inacheza. Shabiki huyo alikuwa akimpiga picha Mreno huyo wakati akireja vyumbani baada ya mchezo.
Dogo alikuwa anataka kupiga picha jeraha la mguuni la Ronaldo halafu pia kulikuwa na maneno ya matusi kumshambulia Ronaldo na wachezaji wote wa United.
Ronaldo na yeye ni binadamu kama sisi tu kuna muda mtu unashindwa kuji-control na naamini ni mara nyingi sana anajitahidi kuficha hisia zake kwasababu inabidi alinde brand yake ila alichofanya jana ni kitu cha kawaida tu kutokea kwa mtu.