Cristiano Ronaldo bishoo wa Madeira na miguu iliyompa ubilionea

Cristiano Ronaldo bishoo wa Madeira na miguu iliyompa ubilionea

RAKI BIG

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2020
Posts
394
Reaction score
456
Wakati Dunia ikiwa katika uso wa tabasamu baada ya janga la Corona kupungua ni wakati wa kusema asante sana Mungu. Nyakati ambazo tulipoteza baadhi ya watu muhimu sana katika maisha yetu, ila yote kwa yote ni mipango yake na lazima itimie

Katika kisiwa cha Madeila moja kati ya maeneo yenye umaskini mkubwa sana kutoka nchini Ureno kuna mwanamama mmoja Maria Dolores dos Santos Aveiro alituletea kijana mmoja ambaye baadae alikuja kuishangaza dunia. Kutokana na kuishi katika mazingira magumu sana mwanamama huyu na mumewe ambaye alikuwa akifanya kazi kama mtunzaji bustani wa Manispaa

February 5,1985 mwanamama Maria Dolores dos Santos Aveiro alituletea kijana katika uso huu wa Dunia kijana Cristiano Ronaldo dos Santos aveiro. Katika ukuaji wake kijana huyu kutokea visiwa vya Madeila alikulia katika mazingira magumu sana kutokana na wazazi wao kuwa maskini sana.

Ronaldo alipofikisha umri wa miaka 14 mama yake aliamua kumuachisha Ronaldo shule na kumpeleka shule ya soka kutokana na kuonyesha kuupenda mchezo huo. Na hatimae kwasasa anafurahia mafanikio ya mwanae. Lakini wakati Ronaldo ndio anaanza kuchomoza katika ulimwengu wa soka aliweza kumpoteza baba yake mzee Jose dinis Aveiro mwaka 2005 wakati huo Ronaldo akiwa na umri wa miaka 20 tu, na kitu kilichopelekea kifo cha mzee wake ni ulevi uliopindukia.

Kwasasa Dunia inafurahi kila kitu ambacho Ronaldo amefanikiwa kukitoa katika ulimwengu wa soka. Ana kila kitu maishani katika maisha ya soka anakosa kombe la Dunia pekee. Maisha kwake yahitaji nini zaidi.

Ndio mfungaji bora wa muda wote wa ligi ya mabingwa ulaya, ndio mfungaji bora wa muda wote wa Ureno, ndio mfungaji bora wa muda wote wa Real Madrid natabasamu kisha napiga makofi kwake na kusema asante sana Ronaldo.

Amefanikiwa kushinda ligi ya mabingwa mara 5,katika maisha yake ya soka mara nne akiwa katika kikosi cha Real Madrid na mara moja akiwa katika kikosi cha Manchester united. Kama tukiamua tuangalie mafanikio yake nadhani tunaweza kumaliza walau siku nzima kumuelezea.

Mkononi ana tuzo tano za mchezaji bora wa Dunia akizidiwa tuzo moja na swahiba wake Messi. Tushukuru sana na kusema asante kwa kuweza kushuhudia kipaji cha Ronaldo huko mbele tutakuja kuwaelezea wajukuu zenu namna gani mchezaji huyu alivyoweza kuvunja karibu rekodi zote za soka. Katika maisha yake ya soka amefanikiwa kufunga mabao zaidi ya 700 unadhani maisha ya soka yangehitaji nini kutoka kwake.

Nje ya soka Ronaldo ni mshindi pia, anapiga pesa za maana sana hapa ndipo mahala ambapo hata wachezaji wetu wanatakiwa kujifunza. Ronaldo anafanya kazi na matangazo mengi ya kibiashara yakiwemo Electronic Arts, Altice, DAZN, Herbalife, MTG, Egyptian Steel haya ni baadhi ya makampuni ambayo humlipa pesa Ronaldo

Kutokana na kutambua uwezo wake nchini kwao Ureno na kwa heshima wameamua kuupa uwanja wa ndege Cristiano Ronaldo Madeira International Airport mahala ambapo alizaliwa, unadhani kuna kipi Ronaldo anakihitaji kwa sasa ni mshindi wa ndani ya uwanja na nje ya uwanja.

Kujitunza kwake na kuitunza miguu yake imeweza kumpa utajiri mkubwa sana duniani. Ronaldo amekuwa bora kwa misimu 15 mfululizo kwanini asitupe thamani ya miguu yake. Kwasasa yupo zake pale Turin, Juventus akiendelea kutupa ufahamu wa miguu yake.

Nyakati kwake zinavyozidi kwenda ndio anazidi kuwa mtamu, anazidi kufunga kadri awezavyo, huyu ndio bishoo kutoka Madeila. Hivi majuzi jarida kubwa duniani la Forbes liliweza kumtaja Ronaldo kama bilionea haikuwa rahisi kwake mpaka kufika hapo zilihitajika nguvu, bidii na maarifa mpaka kuwa Bilionea.


Shukrani sana kwa akademi zilizofanikiwa kumtunza Ronaldo mpaka kufika hapo alipo leo. Haikuwa kazi rahisi sana Andorinha, Nacional na Sporting Cp hawa wote kwa pamoja walishiriki katika malezi ya kijana huyu ambae ameweza kuuteka ulimwengu wa soka.Kizazi kijacho kitakuja kushuhudia utamu wa huyu BISHOO WA MADEILA MPAKA MIGUU ILIYOMPA UBILIONEA
By Gascoigne Brian
Ista Mrope_10
 
Umemtendea vyema CR7,naenjoy kumuona na sitaki ushauri Kama mwingine ana wake naye amsifie, my mi inanihusu nini?
 
mimi timu cr7 wa kutupwa,huyu bishoo haswa,laiti kama angeanza pamoja laliga na mesi,mesi asingemweza kwenye magoli laliga
 
Back
Top Bottom