Swahili AI
JF-Expert Member
- Mar 2, 2016
- 10,174
- 89,364
Cross Examination Day;
Wakili:
Mhe. Mkuu wa Wilaya ijuze mahakama kiwango chako cha elimu.
Mkuu wa Wilaya:
Shahada
Wakili:
Ieleze mahakama majukumu yako kwa kifupi
Mkuu wa Wilaya:
Mwakilishi wa Mhe. Rais Wilaya ya Ubungo na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Wilaya
Wakili:
Je! Unawafahamu madada 36 walioko hapa mahakamani
Mkuu wa Wilaya:
Siwafahamu
Wakili:
Ilikuwaje ukaamuru Polisi wawakamate na kuwashikilia mahabusu?
Mkuu wa Wilaya:
Ni 'madada Poa'
Wakili:
Mhe. Mkuu wa Wilaya ieleze mahakama unamaanisha nini unaposema hawa ni 'Madada Poa?'
Mkuu wa Wilaya:
'Madada Poa' ni wanawake wanaojishughulisha na biashara haramu ya kuuza miili yao.
Wakili:
Je! Ulijuaje madada hawa wanafanya hiyo biashara uliyoisema?
Mkuu wa Wilaya:
Niliwakuta wamesimama usiku Sinza
Wakili:
Je! Ulipowakuta walikuuzia wewe miili yao
Mkuu wa Wilaya:
Hapana
Wakili:
Je! Unaweza ukataja majina ya wateja (wanaume) waliokuwa wananunua miili ya hawa madada?
Mkuu wa Wilaya:
Sikuwaona.
Wakili:
Unafahamu maana ya biashara
Mkuu wa Wilaya:
Biashara ni shughuli ya kuuza na kununua bidhaa au huduma
Wakili:
Je! kusimama Sinza usiku ni kufanya biashara
Mkuu wa Wilaya:
Hapana
Wakili:
Je! Kusimama Sinza usiku ni kosa la Jinai?
Mkuu wa Wilaya:
Hapana
Wakili:
Je! Unafahamu kuwaita madada hawa jina ulilowaita na kuwaweka kwenye Vyombo vya Habari ni kuwadhalilisha na kutweza utu wao mbele ya waume zao, familia zao na umma kwa ujumla (Defamation)?
Mkuu wa Wilaya:
Ndio
Wakili:
Je! Unafahamu kuwakamata watu na kuwashikilia rumande Polisi kwa muda wa ziadi ya siku tano pasipo kuwapeleka mahakamani ni kinyume cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura 20?
Mkuu wa Wilaya:
Najua
Wakili:
Kwa hiyo umefanya makusudi kuvunja Sheria za nchi?
Mkuu wa Wilaya:
Hapana. Nilikuwa nasafisha Wilaya yangu ya Ubungo
Wakili:
Je! Unamaanisha hawa madada ni takataka?
Mkuu wa Wilaya:
Hapana
Wakili:
Mhe. Hakimu sina maswali zaidi