Cruyff baba wa tik tak football duniani( Sehemu ya 2)

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Tuendelee....
.
Asubuhi moja pale Camp Nou kulikuwa na wachezaji wanafanyiwa vipimo ambapo mchezaji atakayefikia urefu wa 1.80m atabakishwa, mmoja wapo ambaye hakufikisha alikuwa Pep Guardiola
.
Kwa Cruyff ilikuwa tofauti sana akaenda La Masia akachukua vijana wembamba, wafupi hata nguvu hawana, watu kama Albert Ferrer, Serge na Guillerme Amor, kuna vitu alivitaka, ile speed, ubora wakiwa na mpira kifupi ni technical giftedness, kumbuka hakuna aliyezidi 1.8m hapo, viongozi walizidi kumshangaa
.
Cruyff aliweka wazi kuwa hata Pep hakuwa na vigezo vingi vya soka ila vision na ubora wake ndivyo vilimfanya amuamini, he pressed opponents like rats at every angle
.
Kwa mujibu wa Oriol Domenich ambaye alikaa na timu za vijana za Barca enzi za Cruyff ni kuwa, muda mwingi mazoezi yalikuwa ni kutumia mpira, mpaka pumzi mwamba alikuwa anawatengeneza kupitia mpira.
.
Kumbuka Cruyff mwenyewe enzi zake alikuwa zaidi ya shetani uwanjani, hivyo wanadai kila mara anasimamisha mazoezi anachora angles na kuwaekeleza wapi walipaswa kukaa wachezaji
.
Sumu aliyoipika ndio Barca tuliyokuja kuishuhudia ya wakina Andres Iniesta na Xavi Hernandez, zamani Barca hawakuamini kabisa aina hii ya viungo, siku moja alimfuata Pep alimwambia huyu Xavi atakufanya ustaafu mpira, lakini pia alimwaminisha kuwa Andres Iniesta na Xavi watatengeneza pacha moja hatari zaidi duniani kwenye soka.
.
Huyo ndie Cruyff bwana, kitu wengi wasichojua kuwa mwamba alikuwa muhuni mstaarabu sana, Eusebio anadai baada ya kupoteza mchezo muhimu wa La Liga 1990 kila mtu alikuwa anatetemeka wakijua Kocha atamind, aliingia vyumbani akasema tu nje baridi kali sana, ila tukutane kesho mazoezini
.
Cruyff huyu huyu ndie amemfundisha jeuri Guardiola, aliachana na mafundi kama Michael Laudrap, Andoni Zubizaretta, Salinas na Goikoetxea, huku viongozi wakihuzunika sana ila hakujali.
.
1995 wakati anaamuru Romario auzwe aliwahi kusema, "Romario sio mzuri kama nilivyokuwa mimi, bado mimi nafundisha wachezaji kucheza mpira sio kufunga magoli"
.
Mzee katangulia ila kaacha vitendo ambavyo Pep anasumbua navyo, ambavyo Barcelona imesumbua navyo,

Pumzika kwa Amani Johann Cruyff

 
Mimi binafsi Nadhani J. Cryffu ndio alistahili kuitwa mfalme wa soka duniani na sio Pele. Maana mambo alioufanyia huu mpira wa miguu akiwa kama mchezaji ni uzito wake ni sawa na yale aliyoyafanya nje ya uwanja.

Huyu ndio aliifanya Ajax na timu ya Taifa ya Uholanzi zikawa ni giant teams mpaka leo hii.

Vile vile ndio aliifanya Barcelona na timu ya Taifa ya Hispania zikawa giant teams mpaka leo hii.

Sasa nani mwingine amewahi kufanya hivi?

All hail to you Johan. Your legacy lives on
 
Kwahiyo pele is overrated?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…