Elections 2015 CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake

Mkuu Dangadunguri, tunapojadili siasa, tujadili siasa na sio kuchanganya hoja za siasa na udini, kwa nini tuuchukie Uislamu?!, pamoja na tofauti zetu za kidini, sisi ni wamoja!, lazima tujifunze kukubaliana, kuvumiliana, kustahiliana na tukishindwa kabisa kukubaliana, then tunakubaliana kutokukubaliana!,haya mambo ya kuitana makafiri ni kama kututukana!. Tanzania ni nchi ambayo haina dini, lakini watu wake wana dini zao, dini kuu zikiwa mbili, Waislamu iliyoletwa na Waarabu, na Ukristo ulioletwa na wakoloni wazungu, wote hao walipokuja walitukuta tuna dini zetu za asili wakatufunza dini zao, na kuziona ndio bora, zile dini zetu za asili wakatuita wapagani na dini zetu wakaziona ni za kishenzi, dini zao ndio bora. Kitendo chaa kumuita mtu kafiri ni cha kibaguzi, na kujionyesha dini ndio bora huku unaelewa wazi kila mtu ana dini yake kama sio Mkristo ni Muislamu au anayefuata dini yake ya asili, hivyo hili suala la ukafiri linatokea wapi?!.

Mimi ni Mkristo lakini ninawaunga mkono Waislamu katika hoja ya Mahakama ya Kadhi-
Mwarobaini wa Kweli wa Mahakama ya Kadhi ni Huu,
Pia kwenye hoja ya OIC, mimi ni Mkristu lakini niliunga mkono hoja ya Tanzania kujiunga OAC

Tukija kwenye suala la Muungano na kuulinda kwa gharama yoyote, hapa ndipo ninapotofautiana na wengi. Nikiwarudisha nyuma katika maumbile ya nchi, Visiwa vyote vya bahari jirani na nchi kavu vilikuwa ni sehemu ya hiyo nchi kavu kabla ya kumeguka miaka milioni nyingi nyuma, hivyo visiwa vya Zanzibar ni sehemu halali ya Tanganyika, ni mali ya Tanganyika, hivyo Tanganyika kuhakikisha unaulinda muungano kwa gharama yoyote ni fulfillment of its duty.

Waarabu wakiongozwa na Sultan Seyyid Said, ile mwaka 1832, walivivamia visiwa vile na kuvitwaa kana kwamba wameviokota na havina mwenyewe, ambapo Sultan Said akaifanya Zanzibar kuwa makao makuu yake, bila kuwashirikisha wenyeji aliowakuta pale aliwaona ni sawa tuu na manyani na ngedere.

Mwaka 1884 wakati wakoloni wanagawana bara la Afrika kama mali mali yao, walimtambua Sultan wa Zanzibar na kungawia visiwa hivyo na ukanda pwani wa maili 10, chini ya ulinzi wa Muingereza, hivyo Mwarabu kujihalalishia visiwa vya Zanzibar kama halal yake.

Mwaka 1963 Muingereza akatoa uhuru wa bandia kwa Sultan na vibaraka wake, na ndipo Januari 12, mwaka 1964, wenye nchi yao, wakafanya Mapinduzi Matukufu, wakavitwaa visiwa vyao toka kwa Sultan mvamizi, ila kwenye mapinduzi yale. hawakuwatimua Waarabu, ila waarabu walikimbia wenyewe!.
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa!.
Shujaa Mkuu wa Mapinduzi Sheikh Abedi Amani Karume, akaomba ulinzi kutoka kwa Tanganyika, ili kuhalalisha nchi huru moja kuilinda nchi huru nyingine, bila ya kuonekana ni uvamizi, ikabidi Tanganyika na Zanzibar ziungane fasta fasta hapo Aprili 26, 1964.
Hivyo kwa sehemu moja, muungano unaipatia ulinzi Zanzibar, lakini kwa sehemu ya pili, muungano umeirudisha sehemu halali ya Tanganyika chini ya milki yake, hivyo lazima ulindwe kwa gharama yoyote maani ni mali yetu halali!.

Pasco
 
Mkuu Gamba la Nyoka, msimamo wangu kuhusu kilichotokea Zanzibar uko wazi kabisa, Jecha hakuwa na mamlaka yale ya kujiugeuza ZEC, alichofanya Jecha ni kitendo haramu, lakini ili haramu iwe ni haramu kweli, lazima iharimishwe, haramu isipoharimishwa hugeuka halal!. Kwa vile ile haramu ya Jecha haikuharimishwa, hivyo ikahalalishwa na uchaguzi wa marudio.

Pia nikatolea mfano wa kubakwa. Kubaka ni kosa la jinai, lakini ili liwe kosa, lazima anayebakwa alalamike, mwanamke akibakwa asipolalamika, na akabakwa tena na tena, atahesabika ameridhia, hivyo Wazanzibari katika umoja wao, wameridhia unakaji huu wa demokrasia Zanzibar, kwa sababu hakuna yoyote aliyelalamika rasmi, kulalamikia kwenye media sio utaratibu rasmi wa kuwasilisha , malalamiko.

Kuhusu hili la Zanzibar, mimi mwenyewe tuu nimepandisha nyuzi Zaidi ya 10 na hizi ni baadhi tuu.
  1. Zanzibar: Kama Maalim Kajitangazia Ushindi, kwa nini hajashitakiwa? Jecha Kapata Wapi Mamlaka ile?
  2. Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda
  3. Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua hatua zozote
  4. Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar?
  5. Zanzibar: Japo SMZ ya SUK sio de jure tena bali ni de facto, lakini ipo!, na hakuna aliyejiuzulu!
  6. CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake
  7. Hatimaye CUF 'Wameridhia' Rasmi, Kushiriki Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar!.
  8. Uchaguzi wa Marejeo Zanzibar ni Huru na Haki! Tuyasubiri Matokeo, Tuyakubali!
  9. Jee Kuna Uwezekano Siku Zote Huwa Hazitoshi, Bali Zinatosheshwa?!. Utosheshaji Ulipogoma, Ukafutwa?!
  10. Uhalali wa Rais Dr. Shein Wa Zanzibar ni Kutokana na Uchaguzi Halali, Huru na Wa Haki! .
  11. Ukweli Mchungu Zanzibar: Hakuna Mgogoro Wowote wa Kisiasa, Shein ni Rais Halali, Uchaguzi ni 2020!
  12. Pemba Chini ya CCM kuneemeka au Kujutia Kuichagua CUF Chaguzi Zilizopita?!
  13. Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!
Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…