Elections 2015 CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake

JECHA Ni Wakala Na Mtekelezaji Wa Maagizo Ya Viongozi Wa CCM Na Serikali Yake Tu!!! Anatumika Kama Nyenzo Ya Kupatikana Kwa Maslahi Ya Kundi Hilo!!! NDIO Maana Ktk Matamko Yake Yote, Kuanzia Lile La KUFUTA MATOKEO Na Hili La KURUDIA UCHAGUZI Huo, AMESHINDWA Kabisa Kunukuu Hata Kifungu Kimoja Tu Cha Kisheria, Iwe SHERIA Ya Uchaguzi, Ya ZEC Au Kakatiba Ya ZANZIBAR Ambayo Inampatia Mamlaka Ya Kufanya Hivyo!!! ZAIDI Ya Kutangaza Tu KIENYEJI!!!
 

Haitakuwa mara ya kwanza CUF kususia uchaguzi. Kufikiria kuwa chama hiki kitafutika kwa kususia uchaguzi huo ni kujidinganya; tena kujidanganya kitoto. CUF kushiriki uchaguzi huo ni kujidhalilisha. Hao wanaotaka ushindi wa mezani wauchukue.
 
CCM Waso Haya washafanya haya 2005..CUF Walisusa na CCM Ikazoa vitu Pemba Maaruf Viti vya Maruhani. Hilo Hlikuathiri CUF Bali kimezidi kuimarika mara dufu .
Na hata mara hii CUF wakidinda basi CCM Watachaguliwa na Maruhani na kura za wizi ...
 
Cuf ni chama cha ukombozi hakiwezi kufa wakati wazanzibar bado wanaonewa, wanaishi chini ya uhuru bandia. Mapinduzi yao yametekwa.
 
Ni uongo upi huo uliorudiwa rudiwa ambao umegeuka kweli?
Kwamba Uchaguzi ulikuwa na dosari?

Anguko la CCM kufuatia uchaguzi wa tarehe 25 oktoba 2015 ni kutoweka kwa amani na utulivu?
Kwa Jeshi kukiweka chini ya ulinzi (lock down) kituo cha kutangazia matokeo Cha ZEC na Polisi kumteka nyara Makamu Mwenyekiti wa ZEC ilikuwa ni kuweka amani na utulivu?
Kwa hiyo amani na utulivu ni kwa CCM kukataa kushindwa? Au amani na utulivu ni CCM kungang'ania madaraka, kupiga DOMO-krasi na kugawia wananchi "maisha bora"?
Je chokochoko ni pale upinzani unaposhinda uchaguzi?
Pasco bana.

Zipo ripoti kuwa vikosi vimeanza na hiyo kazi ya kuhakikisha uwepo wa amani na utulivu kwa kupiga mabomu ya machozi wananchi waliokuwa wanapiga stori kwenye vijiwe vyao vya kahawa, halua na kashata.
 
Mkuu Pasco unanyata bila ya kupuliza, lakini ndivyo inavyotakiwa, maumivu yakiwa makali yanaleta changa moto pia.

Mimi nina imani 100% uchaguzi ni upotevu wa pesa za walipa kodi. Nina hakika ya kwamba kwa upande wa diwani na wawakilishi, washindi wote washapatikana, wameshatangazwa na wameshakabidhiwa vyeti vyao. Zitakapopigwa kura tena na kupatikana washindi wengine hapo ndio suala la kwenda mahakamani litaanza.

Na kutokana na sheria za uchaguzi, Zanzibar, Jecha na Tume kwa ujumla hawana mamlaka ya kutenguwa matokeo yale. Na kwa maana hiyo Madiwani na Wawakilishi walochaguliwa 25/10/2015 watabakiwa kuwa ni wateuzi halali. Hiyo haina mjadala. Hawa wanataka kufuja pesa tu. Na ikitokezea kura za madiwani na Wawakilishi wapya kutambulika kisheria katika mahakama basi mimi itakuwa wa kwanza kuihama Tanzania na I will personally DHL you my TZ passport torn into pieces. Take my words
 
umewahi kusikiliza nyimbo unayoipenda kwenye sahani ya santuri yenye pengo? halafu kula wimbo unapoendelea unakuwa unajirudiarudia. Bsi ni sawa na mawazo ya PASCO. Mawazo yake sawa na nyimbo za Intarahamwe, kusudio lake halipishani la NKurunziza, ubaguzi wake sawa na CCM Kisonge. Lakini yote hayo yote tunayajua. Alishindwa Mreno , yakamtapika Sultan na si vigumu kumcheuka CCM Tanganyika. Kwa bahati mbaya sana PASCO nafikiria humjui mtu anaeitwa Mzanzibari. Kwa faida yako na watu wenye akili finyu na uwezo wa dhiraa moja ya kufikiri wangelikisoma kitabu kimoja maarufu kinaitwa CLOVE ISLAND. Ungemjua mzanzibari ni nani.Kwa ufupi ni mnyonge, mpole,mstahamilivu,msikivu lakini ni mwerevu na akiamua akisema QUN FAYAQUN basi ni QUN FAYAQUN kweli, ataulinda utu na heshima yake kwa gharama yoyote ile!

Zama za kutishana zimeshapitwa na wakati, wala kauli kama hizo haziwezi kubadilisha msimamo wa nafsi na maamuzi matakatifu ya wazanzibari waliowengi. Lakini kauli kama hizi wazungu wanasema " it is easy said than done" Ni makala ya kupata " cheap popularity"
Naamini Tanzania haina Amiri Jeshi mkali, katili jeshi kubwa, vifaa na silaha za maangamizi kuliko ilivyokuwa USSR!.Lakini ilibugujika kama unga wa AZAM seuze paka wa biti Hatiibu......Ukimtupia ganda la muwa la jana kwake anaona ....
!
 
Ikipendaroho... usitumie hasira mkuu... We ool want this to end Well... and Mola Akipenda litaisha.. I know how hard it is for All those cuf supporters in the island... lakn wat to do mkuu? Nuthn kwa kweli... je Will you continue hoping? That things will work out? Or? Mkiambiwa na viongzi wenu mkashiriki uchaguzi? Mtaenda?.
If all of you believe mkuu... kama wengine walivocomment kwenye uzi huu kuwa marejeo ya uchaguzi ni kumuezesha tu mwafulani ashinde? Would you be better of participating or not? Weigh out your options carefully...
 
Kwanza mimi siwezi kupiga kura Zanzibar, so regardless of what Ukawa or anyone else says, I cant vote.

La pili ni kuwa nina amini kurejewa kwa kura ni kitendo cha kinyume na sheria, na najuwa usumbufu nilioupata wakati wa kupiga kura, so am not stupid enough to waste my time unnecessarily even if I was eligible for the re-voting.

La tatu nasisitiza tena hata hizo kura zikipigwa, matokeo yake hayatosimama. Yatapingwa mahakamani. Hilo nina hakika nalo 100%. Kwa mtazamo wangu kuna miezi kama 6 mengine bila ya madiwani, wawakilishi na possibly raisi halali.
 
mnafikir watu watakuja kupiga kura?nchi ishakuwa ya kidikteta.kuna uchaguz gani unaofanywa bila kampenii?
kampeni zilishafanyika, imebakia kupiga kura tu, make maneno ya kampeni ni yaleyale, kwani imegundulika hakuna jipya.
 
Pasco
Nimekushutumu kuwa ni mfuasi wa ccm kwa sababu siku zote nakala au hata maoni yako ni kuukosoa upinzani au kuikosoa zanzibar, sioni nakala za kuikosoa ccm juu ya suala la muungano au something else.
Mkuu GHIBUU, uko very right kunidhania unavyonidhania kwa sababu wengi wa members humu wana take sides, mimi sina chama na sitake sides, CCM wakifanya mazuri, nawapongeza, wakifanya madudu nawakosoa vivyo hivyo kwa wapinzani wakifanya mazuri nawapongeza na wakifanya madudu nawakosoa, bahati mbaya wapinzani wamefanya madudu mengi kulio mazui, hivyo theads zangu za kusifu zimekuwa chache kuliko za kukosoa, ila pia kwa CCM nimewapongeza maa chache na kuwabalasa sana tuu tatizo hamsomi. Mimi ni mtu wa kutanguliza mbele maslahi ya taifa. Tafuta muda pitia nyuzi hizi
Kwa ku assume mimi ni pro CCM hebu pitia nyuzi hizi.

[URL='https://www.jamiiforums.com/threads/kwa-hili-la-salum-mwalimu-cuf-inastahili-pongezi-ni-mwanzo-mzuri-wa-reality-ya-ukawa.848782/']Kwa Hili la Salum Mwalimu, CUF Inastahili Pongezi ni Mwanzo
Kwa Hili! Hongera Sana Chadema, Hongera Mhe. Mbowe!,
CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!
[/URL]

Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed ...
Matokeo ya Serikali za Mitaa: Ni mwanzo wa mwisho wa CCM?! Au ...
Yametimia!, CCM Imechokwa!, CHADEMA Njia Nyeupe 2015!-
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi
Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze: CHADEMA Muungeni mk
Kuelekea 2015: Ni Mbio Za Magari Kati ya Mkweche na Mashi
Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui MkubwKuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!...
Hivi Kweli Kuna Mtanzania, Mwenye Akili Zake Timamu, Ana
Nimekubali matokeo, UKAWA Kanda ya Ziwa wako vizuri, Mnyik
Octoba 2015:Tanzania Has a Choice Kati ya Kuendelea na Uma

Pasco
 
Hili la muungano, ni kweli ila chanzo sio Nyerere, chanzo ni Karume, baada ya Mapinduzi yale matukufu ya Zanzibar, Karume akaogopa kuvamiwa na manowari za Uingereza zilizotumwa kuja kumejesha Sultani, hivyo Karume akaomba ulinzi, majeshi ya nchi moja yatakwendaje kulinda nchi nyingine?. Ikaamuliwa dawa ni kuungana!.
Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano ...

Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, Then "Twe
Jee Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilic
Swali: Hivi Muungano Tanzania Upo Kweli?! au ni Dhana Tuu ...
Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Ga
Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar K
Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar? | JamiiForu
Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua ..
Zanzibar: Japo SMZ ya SUK sio de jure tena bali ni de facto
Ushauri wa bure kwa CCM: Hope for the best but get prepared f
Chonde Chonde Rais Kikwete: Msimamo wa CCM wa Serikal
Pasco
 
Nani aliamua?
Je kuna ukweli kuwa Mapinduzi ya Zanzibar yalipangwa Tanganyika?


Soma hapa link Ukweli wa historia ya mapinduzi ya Zanzibar
 
Nani aliamua?
Je kuna ukweli kuwa Mapinduzi ya Zanzibar yalipangwa Tanganyika?


Soma hapa link Ukweli wa historia ya mapinduzi ya Zanzibar
Nimemsikiliza Tundu Lisu na kuisoma ile makala, kiukweli hakuna kitu, hizi kauli za Mapinduzi ya Zanzibar yalipangwa na Tanganyika, ni kauli za kujifariji za vizalia wa waliopinduliwa, ili kujenga uhalali kuwa Wanzanzibari wenyewe wako tayari kuendelea kutawaliwa na Sultan, walioleta chokochoko sio Wazanzibari bali ni Watanganyika!.

Kuna mambo kuhusu Zanzibar hayasemwi, kama huku bara baada ya kutolewa kauli ya "Ni zamu ya Kaskazini", zilitolewa kauli kuwa kamwe Mkaskazini hawezi kuwa rais wa nchi hii!. Vivyo hivyo niliwahi kusikia kauli za "Kamwe Mwarabu hawezi kurudi kutawala Zanzibar!", mara "Kamwe Mpemba hawezi kutawala Zanzibar kwa hoja kuwa Pemba haikushiriki katika yale Mapinduzi Matukufu!". Hizi japo ni kauli za kibaguzi, na mimi binafsi siungi mkono ubaguzi wa aina yoyote lakini nimesema kilichosemwa, sometimes lisemwalo lipo, kama halipo linakuja!. Kauli huumba!.

Huku bara wakati wa kupigania uhuru, kulijitokeza tofauti kati ya Mangi Mkuu Tomas Mareale na Mwalimu Nyerere, zikatolewa kauli za kichinichini kuwa nchi hii kamwe Mchagga au Nshomile, hawezi kuja kuwa rais wa nchi hii!, urais wa Tanzania na Zanzibar ni hakimiliki ya mtu kutoka Chama cha Mapinduzi, kwa sababu ni Chama Cha Mapinduzi pekee ndio wenye long eksipiriennsi ya uzoefu wa muda mrefu katika urais, sasa hayo makabila yalisemwa kamwe, sijawahi hata kusikia angalau hata wakijaribu kujitokeza kuchukua fomu kuomba kuteuliwa CCM, hivyo alichokifanya Jecha eza kuwa ni utekelezaji tuu wa kauli kama hizi za kibaguzi, na siku ile lile bango la maskani kitonge lilipopita pale mbele ya mgeni rasmi, lilishangiliwa sana hadi na mgeni rasmi!.

Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, yalifanywa na Wazanzibari wenyewe na wala sio Watanganyika!. Ila Muungano ndio ulifanywa na Watanganyika na Wazanzibari, tukaungana kuwa kitu kimoja na kuunda nchi moja ya Tanzania!, hivyo Muungano huu utalindwa kwa gharama yoyote!, kiongozi awaye yote, kutoka chama chochote, akionekana ni riski kwenye majaaliwa ya muungano wetu, hapewi nchi!. Wanaonyima nchi, wananyima kwa hiyo hoja ya gharama yoyote!. Poleni ndugu zetu, mnaweza kujikuta kumbe kauli zenu ndizo zinawaponza na kupelekea kutokea yaliyotokea, huku tukimlaumu Jecha, kumbe sii Jecha bali wenye nchi wenyewe!.

Mapinduzi Daima.

Pasco
 
Pasco tafadhali naomba unijibu hili, cuf itakufa vipi znz wakati inawabunge kule wasiopungua 25?
 
Pasco tafadhali naomba unijibu hili, cuf itakufa vipi znz wakati inawabunge kule wasiopungua 25?
Nguvu, ni kweli CUF ina wabunge 25 ndani ya bunge la JMT, ila Power ya CUF ni Zanzibar ndani ya BLW na ndani ya SUK na sio ndani ya Bunge la JMT!. CUF ikijitoa uchaguzi huu wa marudio CCM, itavunawawaklishi 50 kujumlisha na wabunge 25 juamla 75 kwa 25 madiwani wote watakuwa ni CCM. Strong hold ya CUF ni Zanzibar, ikiondolewa Zanzibar, na kuondolewa SUK, CUF is dead!.

Pasco.
 
Unakusudia huyu sultani ambaye anatawala Zanzibar kwa miaka 50 sasa?
Nikumbushe sultani huyu anaitwa nani?

Al-cuf? Au Al-waafrika?
 
Kwa kauli yako CUF haina jinsi ya kususia uchaguzi kwakuwa majina ya wagombea tayari yapo tume ,sasa swali langu ni rahisi, je hao wagombea wakiamua kuhamia ADC au wakifukuzwa uanchama kwa namna yoyote ile je tume itaenda mahakamani kupinga?naomba ushauri
Kwa kauli yako CUF haina jinsi ya kususia uchaguzi kwakuwa majina ya wagombea tayari yapo tume ,sasa swali langu ni rahisi, je hao wagombea wakiamua kuhamia ADC au wakifukuzwa uanchama kwa namna yoyote ile je tume itaenda mahakamani kupinga?naomba ushauri
 
Mkuu pasco..
Shkamoo bro... Mapinduziiiii....
Ama baada ya salam kaka... umenikumbusha article moja aliwahi kuandika Joseph Mihangwa about Jumbe... kuna sehem anasema kosa la jumbe lilikua ni "kutaka kukanyaga sehem ambayo hata malaika haruhusiwi kukanyaga"...
Back to the point mkuu... kuhusu experience and oool na mwenye haki ya kushika reigns za uongozi wa nchi yetu hii adhim... should we just get back to a one party state and get away with ool the theatrics of multypartism?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…