Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Katibu wa Chama cha wananchi (CUF -The Civic United Front) mkoa wa Mbeya Ibrahim Mwakwama amesema wapinzani wanatakiwa kuachana na maslahi binafsi badala yake waungane ili kuhakikisha uchaguzi mkuu ujao wa 2025 wanashinda hususani Ubunge na Udiwani mkoani Mbeya
na kuwaletea maendeleo ya kweli wananchi
Kiongozi huyo mtendaji wa CUF mkoa wa Mbeya na wilaya ya Mbeya mjini amesema hayo wakati wa mazungumzo yake kuhusu masuala mbalimbali ya siasa za Tanzania, maendeleo ya mkoa wa Mbeya, Tanzania sanjari na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2025
Pia soma: Kuelekea 2025 - CHADEMA, ACT Wazalendo na CUF tengenezeni Alliance kupelekea uchaguzi 2025
Amesema chama chake kimejiandaa kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa wa ushindani kwani wameazimia kuungana na vyama vingine vinane vya upinzani mkoani Mbeya isipokuwa CHADEMA kuhakikisha kwa pamoja wanasimamisha mgombea ubunge atakayekuwa hitaji la wana Mbeya mjini ili kufanikisha kumuondoa madarakani kupitia sanduku la kura Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania akidai jiji la Mbeya limedumaa kimaendeleo
Aidha Ibrahim Mwakwama ameeleza kukerwa na sintofahamu na migongano anayoitaja kuwa ni ya kimaslahi miongoni mwa vyama vya wapinzani akigusia Wenyeviti wa CHADEMA Taifa Freeman Aikael Mbowe na Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba kuendelea kusalia madarakani akidai wangeacha nafasi kwa wengine badala ya kukaa nafasi za juu kwa muda mrefu
"Asili ya Mbeya ni wapinzani sasa kwa nini jiji la Mbeya ni chafu ni kutokana na aina ya viongozi tunaokuwa nao, walikuwepo CHADEMA walifanya kwa sehemu yao sasa wamekuja CCM lakini hamna wanachokifanya pamoja na kwamba tuna Spika wanasema ni Mbunge wa IPU (Rais wa Mabunge Duniani) mimi sioni faida ya IPU kulingana na mazingira yalivyo Mbeya ni chafu pamoja na kwamba tuna Spika jimbo halieleweki sasa ni zamu yetu (wapinzani) kwenda kuibadilisha Mbeya yetu"
Amesema ikiwa wapinzani wataungana itakuwa rahisi kushinda uchaguzi mkuu wa 2025 na kwenda kukemea na kuzuia maovu mbalimbali nchini ikiwemo utekaji, mauaji na uminyaji haki za wananchi na kuleta maendeleo ya kweli akidai CCM na viongozi wake hawana dhamira ya kweli kuwaletea maendeleo wananchi ikiwa ni zaidi ya miaka sitini ya uhuru lakini bado wananchi wana maisha magumu huku Taifa likiwa na raslimali lukuki.
Alipoulizwa kinachoendelea ndani ya CHADEMA ikiwa kinachagiza kukua kwa demokrasia na upinzani, Katibu huyo amesema, "kinachoendelea katika siasa za Tanzania ni kichekesho, huu ni wakati ambao wapinzani mimi nilitegemea tungeungana kwa sababu kuiondoa CCM madarakani sisi wenyewe kama CUF ni ngumu lakini vyama vingi vimeweka maslahi yao mbele, ni kwa nini tunagombana?
"Mimi ukiniuliza leo kwamba Lipumba alistahili kuwepo kwenye uwenyekiti ningesema hakustahili ilitakiwa tuone sura mpya ya Mwenyekiti wa CUF, ukiniuliza Mbowe anastahili kugombea uwenyekiti nitasema hastahili kwa sababu tunahitaji kuona mabadiliko kwasababu tunavyotaka kwenda kuchukua nchi mabadiliko huwezi kuanzia kwa jirani ni lazima uanzie kwako, mimi siwezi kufurahia kuhama kwa viongozi wa vyama vya upinzani kuhamia vyama vingine mfano Ibrahim Lipumba amerudi basi tumekubaliana kwenda kujenga chama mahali ambapo kilikuwa kimelegalega, CHADEMA ukiangalia kuna makundi mawili la Mbowe na la Lissu mimi ningewashauri CHADEMA kama wananisikiliza huu sio wakati wa kugombana bali tunahitaji kuunganisha umoja wetu"