CUF: Sasa ni vita ya kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi


CUF yataka Katiba mpya

Imeandikwa na Lucy Lyatuu; Tarehe: 16th December 2010 @ 06:13

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimesema kinaungana na Watanzania wapenda demokrasia na mabadiliko kudai Katiba mpya ya Tanzania itakayokuwa na misingi ya kidemokrasia ya kweli na itakayoweka dira ya maendeleo ya Taifa kwa maslahi ya kizazi cha sasa na kijacho.

Aidha, chama hicho kimempongeza Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuonesha msimamo thabiti katika kusimamia maridhiano ya kisiasa na kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuweka uwiano mzuri wakati wa kugawa Wizara kwa vyama vinavyoshiriki katika serikali hiyo.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akitoa maazimio ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF lililokutana Desemba 10 hadi 11, mwaka huu kwa ajili ya kufanya tathmini ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu.

"CUF inaungana na Watanzania wote bila kujali itikadi za vyama au nafasi walizonazo katika jamii kwa kutumia njia za kidemokrasia kudai mabadiliko ya Katiba ya nchi yetu ili ikidhi matakwa ya hali ya wakati tulionao," alisema Profesa Lipumba.

Alisema pamoja na madai ya Katiba mpya, Baraza Kuu liliagiza wadau mbalimbali na Watanzania kuendeleza madai ya mabadiliko ya sheria za uchaguzi na haja ya kuwepo kwa Tume huru ya uchaguzi ya haki ambayo itaheshimika na kila Mtanzania kwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo.

Profesa Lipumba alisema kutokana na matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Lewis Makame, imedhihirika wazi kuwa Tume iliyopo haina sifa za kuaminika mbele ya macho ya Watanzania hasa kwa kasoro, udanganyifu na mfumo wa uchakachuaji wa idadi ya wapiga kura kuwa waliojitokeza ni 8,626,283 kati ya waliojiandikisha 20,137,303.

"Waliopiga kura kwa mwaka 2010 ni sawa na asilimia 42.8 ya wale waliojiandikisha, hii ni tofauti kubwa sana ikilinganishwa na waliojitokeza kupiga kura 1995 kwa asilimia 76.7, mwaka 2000 asilimia 84.4 na mwaka 2005 waliokuwa asilimia 72.4, Watanzania wengi wamepoteza imani na Tume kama inaweza kusimamia uchaguzi ulio huru na haki," alisema Profesa Lipumba.

Aidha, Profesa Lipumba alisema chama hicho kinapongeza hatua iliyofikiwa ya uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa huko Zanzibar, ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya Katiba ya Zanzibar iliyofanyiwa marekebisho kutokana na maridhiano ya kisiasa yaliyofikiwa mwaka jana.

"CUF inampongeza Katibu Mkuu, Seif Sharif Hamad kuteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na pia kwa wanachama wengine wanane walioteuliwa kuwa mawaziri na wawili, naibu mawaziri," alisema.
 
CUF yazinduka matokeo Uchaguzi Mkuu


*Yatuhumu Tume ya Uchaguzi kwa uchakachuaji
*Yataka Watanzania kuungana kudai katiba mpya
*Yavunja na kupanga upya safu yake ya juu


Na Tumaini Makene
ZIKIWA zimepita takribani wiki nne tangu kutangazwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu yaliyompatia ushindi Rais Jakaya Kikwete, Chama cha
Wananchi (CUF) kimezinduka na kudai uchaguzi huo ulichakachuliwa na kwamba matokeo hayo yamepoteza imani ya Watanzania kwa Tume ya Uchaguzi (NEC) kwani haiwezi kusimamia uchaguzi huru na haki.

Chama hicho hicho pia baada ya kufanya tathmini ya kina ya Uchaguzi Mkuu na katika kujiimarisha ili kukabiliana na siasa za wakati uliopo pamoja na matokeo ya uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, kimefanya mabadiliko makubwa katika nafasi zake kadhaa za juu, ikiwa ni pamoja na kuunganisha baadhi ya kurugenzi zake.

CUF kimesema kutokana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba mwaka huu yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Lewis Makame imedhihirika wazi kuwa tume iliyopo haina sifa za kuweza kuaminika mbele ya macho ya Watanzania, hivyo kuna haja ya kuwepo kwa tume huru na ya haki.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam juu ya maazimio ya Baraza Kuu la Uongozi Taifa la CUF lililoketi siku Novemba 10 hadi 11 mwaka huu Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema;

"Baraza Kuu linawataka Watanzani wote wapenda demokrasia na mabadiliko kuungana pamoja kudai Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakayokuwa na misingi ya kidemokrasia ya kweli na itakayoweka Dira ya Maendeleo ya Taifa letu kwa maslahi ya kizazi cha sasa na vijavyo. CUF inaungana na Watanzania wote bila kujali itikadi za vyama au nafasi walizonazo katika jamii kwa kutumia njia za kidemokrasia kudai mabadiliko ya katiba mpya ili ikidhi matakwa ya wakati tulio nao.

"Sambamba na madai ya Katiba mpya, Baraza Kuu linawataka wadau mbalimbali na Watanzania wote kuendeleza madai ya mabadiliko ya sheria za uchaguzi na haja ya kuwepo tume huru na ya haki ya uchaguzi wa nchi yetu, ambayo itaheshimika na kila Mtanzania kwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo. Kutokana na matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa...

"...na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imedhihirika wazi kuwa tume iliyopo haina sifa za kuweza kuaminika mbele ya macho ya Watanzania hasa ukizingatia kasoro, udanganyifu na mfumo wa uchakachuaji wa idadi ya wapiga kura waliojitokeza kuwa 8,626,283 kati ya wapiga kura 20,137,303 waliodaiwa kujiandikisha.

"Waliopiga kura 2010 ni sawa na asilimia 42.8 ya wale waliojiandikisha. Hii ni tofauti kubwa sana ukilinganisha na waliojitokeza kupiga kura 1995 (76.7%), 2000 (84.4%) na 2005 (72.4%). Watanzania wengi wamepoteza kabisa imani kuwa tume inaweza kusimamia uchaguzi ulio huru na wa haki.

Alisema kuwa Baraza Kuu la chama hicho limempongeza Bw. Alassane Ouattara kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Cote d'Ivoire na linaungana na jumuiya ya kimataifa ikiongozwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani ubadilishaji wa matokeo ya uchaguzi wa rais nchini humo uliofanywa na Serikali ya Bw. Laurent Gbagbo.

Alisema Baraza hilo limesikitishwa na hatua hiyo ambayo inadhihirisha muendelezo wa serikali za nchi za Afrika kuvuruga uchaguzi na kutoheshimu maamuzi ya wananchi " CUF tunatoa mwito kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa tamko la kumtambua Mheshimiwa Alassane Ouattara kuwa Rais halali wa Cote d'Ivoire,"alisema.

Akizungumzia mabadiliko ambayo ameyafanya kwa mujibu wa majukumu ya mwenyekiti yaliyoainishwa katika Katiba ya CUF, toleo la 2009 ibara ya 68 (1), Baraza Kuu limeidhinisha uwepo wa muundo mpya wa Kurugenzi za chama Taifa na kuthibitisha uteuzi wa manaibu katibu mkuu, wakurugenzi na manaibu wakurugenzi wapya.

Alisema Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara ni Bw. Julius Mtatiro, kwa upande wa Zanzibar ni Bw. Ismail Jussa Ladhu, ambao kila mmoja kwa upande wake, pamoja na masuala mengine watasimamia pia majukumu ya Kurugenzi ya Utawala na Ulinzi wa chama.

Kurugenzi ya Uchumi na Fedha itakuwa chini ya Bw. Salum Mandari (Mkurugenzi) na Bi. Zakiya Omari Juma (Naibu). Kurugenzi ya Oganaizesheni, Uchaguzi Baraza la Wawakilishi na Bunge itaongozwa na Bw. Salim Hemed akisaidiwa na Bw. Shaweji Mketo.

Kwa upande wa Kurugenzi ya Haki za Binadamu, Uenezi na Habari, Bw. Salim Bimani atasaidiwa na Bi. Amina Mwidau, huku Bw. Faki Haji Makame akiteuliwa kuwa Mratibu Ofisi ya Katibu Mkuu, Seif Shariff Hamad, ambaye sasa amekuwa na majukumu mengi ya kiserikali akiwa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Katika hatua nyingine pia, kwa mujibu wa Prof. Lipumba, Baraza hilo limewashukuru na kutoa pongezi maalum kwa wapiga kura wa Jimbo la Lindi Mjini kwa kumchagua Bw. Salum Barwany, ambaye ana ulemavu wa ngozi kuwa mbunge wao, kwa tiketi ya CUF. Alisema kuwa watu wa Lindi wameitoa kimasomaso Tanzania juu ya sifa hasi dhidi ya mauaji ya maalbino.

 
Mbona kwenye mada muhimu kama hii haina wachangiaji wengi??
Au wengi wetu ni wasindikizaji??
 

Humwelewi Mwanakijiji wewe, tunaomwelewa huwa tunachagua kuchangia posts zake. Sioni tofauti yake na Naibu katibu Mkuu wa chama fulani!
 
Ükifuatilia kwa makini utaona sasa CCM wanataka kupush ajenda ya Mahakama ya Kadhi na OIC na njia muafaka ni kuandika katiba mpya na kuchomeka vipengele hivyo. CUF ni mawakili wa CCM. Vigogo wa CCM wanaojitosa kudai katiba wamekuwa wengi na kwa hiyo sina shaka na maneno yangu
 
cuf kudai katiba mpya? Hiyo ajenda wameitoa wapi wakati wao ni Ccm wasiotaka katiba ibadilike
 
Ni bahati mbaya habari hii haikupata "Coverage ya kutosha" kwenye magazeti ya leo!!!
 
Hawa cuf wamerui tena kinyumenyume kuwahadaa watanzania? Wanataka kuwadanganya watanznia kuwa wako serious kwenye siasa ya upinzania. Noooooooo!!!! Ni matapeli tu hawa. Wanajileta kwa vile wanaona watanzania, taasisi na baadhi ya viongozi makini wameonesha nia ya kulazimisha katiba sasa nao wanajiingiza ili waonekane kuwa nao walishiriki. Wapuuzi wakubwa. Shiiiiit. Huyu lipimba asubiri nae kupewa chechote kama ndugu yake seif. Ni wanafiki na siyo wapinzani
 
Hii ni kitambo kidogo!! Kuna watu humu walitoa mawazo mazuri sana lakini leo washarukia upande wa pili. Julius mtatiro.
 
Tudai kwanza tume huru, dicteta wetu anataka sana tudai katiba badilishe sentensi mbili, nae aanze upya, tegueni huu mtego
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…