Elections 2010 CUF-Uislam, CHADEMA - Ukristo, CCM - Mixture+UFISADI, Mungu epusha

Hizi fikira za udini katika mambo ya siasa zimetokea wapi? Mbona hivi sasa
yanakuzwa kama vile yana play part katika uongozi? Tanzania na masuala
ya dini ya mtu ni jambo ambalo halijatatiza nchi hii tangu kuasisiwa. Watu tangu
na enzi za zamani wanaishi pamoja wenye dini tofauti bila ya mikwaruzo tangu kuanzia
nyumba za kupanga mpaka kwenye uhuru wa kuabudu.

Ni akili finyu mtu kuamini mambo ya udini ndani ya vyama kwani kila chama
cha siasa kina watu wenye imani mbali mbali na wanaendesha vyama vyao
kistaarabu, chokochoko za watu wachache wanaojifanya wana elimu kushinda
wenzao na kuponda dini za watu ndizo zitakazotupeleka pabaya.

Kuchanganya usomi, udini na uongozi ni kupungukiwa na akili kiasi fulani.
KUWENI NA UPENDO KWA WATU WENYE DINI TOFAUTI ILI MUISHI NA
KUABUDU KWA AMANI.
 
Mkuu wangu Mkandara.
Nimekusoma. Mimi si shabiki wa siasa za dini. Lakini nimeona sana viongozi wa vyama na wanachama maarufu katika vyama wakijihusisha nazo. Hivyo hili si jambo la kufumbia macho likapita tu. Ni kweli si sera za vyama kukumbatia udini lakini ni wazi kama wanachama wanakumbatia udini basi ujue chama kiko katika muelekeo huo huo maana chama ni wanachama.
Naomba nikusahihishe kuwa siku relate udini wa sisi M na muafaka maana muafaka hautanufaisha kafu tu bali na vyama vingine vya upinzani. Lakini nina kila sababu kusema kuwa sasa na sisi M ni chama cha kiislamu kwani hapa kwenye mji nilipo na yale yaliyojitokeza katika uchaguzi uliopita, nimeona mengi yanayonilazimisha niseme hivyo, wala si muafaka.
Najua watu tukikaa vizuri siasa hizo ambazo utaona zimeasisiwa na sisi M yenyewe twaweza kuzishinda.
 
Hamjajua tu. Ccm ina kansa ya mifupa. Kwa mwenye ufahamu anaweza kunyambulisha hili
 
hAPANA, hakuna udini bali kuna hisia za udini tu, tuangalie sera na sio chuki za udini ambazo ndo silaha wanayoitumia CCM
 
huu ni ukweli ambao unauma sana na umesambazwa na ccm kwa manufaa yao wenyewe

cuf na chadema wanahitaji kureform vyama vyao na kuhakikisha kuna balance ya dini na wana attract watu wa dini nyingine, the best solution ni wao kuungana
hebu niambie CHADEMA wareform nini ? labda CUF .
CHADEMA hakuna udini, angalia hata mgawanyiko wa ngazi za uongozi, fananisha na ccm na cuf, utaujua ukweli.
acheni kusambaza majungu kwa kujidai washauri.
kwa kawaida mwenye udini ni wewe unayefikiri mambo yako kidini-dini. nyie ndo wale mkisikia rais katangaza baraza la mawaziri jambo la kwanza kupembua waislamu wangapi na Wakristo wangapi, wakwere wangapi na wasukuma wangapi.
tunamapungufu sana katika kuhoji mambo.
 
hebu nipe uwiano wa wagombea wakristo wa CHADEMA dhidi ya waislamu, nipe uwiano huo kwa ccm na cuf, kisha njoo na jibu ? mara nyingi mtu anaewaza kidinidini yeye ni mdini, siwezi kubishana na wewe,

mi sisemi kuwa cuf inanuka udini kama ambavyo mmeshindwa kutoka kwenye tuhuma hizo, na hoja inayojengwa dhidi yenu inajengwa kwenye mtazamo wa ngazi za Uongozi kwa Tanzania nzima, tangu vitongoji hadi Taifa, wakristo wachache waliokuwepo kina Tabwe Richard hiza nao wanakimbia,
kwa CHADEMA, wanaojenga hoja zao dhidi ya udini chadema, wanatumia hoja zisizo na mashiko, hoja tete, hahaaah, wasio na akili hupumbazika, wenye akili hung'amua, by the way ustawi wa cuf si kitisho kwetu, kwenu ustawi wa CHADEMA ni kitisho.
 

Acha uongo wewe,

Chadema waliwaunga CUF mkono mwaka 2000.
 
Hata hivyo, hii thread ya udini mbona bado iko hapa?

Au kwa vile inasema kuwa vyama vya upinzani (CUF na CHADEMA) ni vya kidini?

Nina hakika mods zaidi ya mmoja wameiona hapa. Ngoja nikaanzishe thread inayosema kuwa ccm ni chama cha kiislam (huu ni ukweli) kisha nione itachukua muda gani kabla ya kuondolewa kutoka hapa.
 
Suala la udini na siasa tuliweke mbali kwani Mungu alipootuumba hapakuwa na mambo ya sisi wakristo sisi waislaam wote familia moja la msingi ni kuchagua kiogozi bora bila kuweka udini!
 
Mchukia Ufisadi,
Mkuu wangu mimi sikubaliani na haya hata kidogo kwamba CCM ina Udini, wala sii CUF au Chadema isipokuwa wanachama wake au viongozi ndio wenye dini. Mwongozo (Katiba), sera na ilani za vyama vyote hivi hazina hata chembe ya mstari wenye Udini, hivyo kama kuna matendo yanayoashiria udini ktk vyama hivi ni kutokana na sisi wenyewe kuwatazama wengine kwa jicho la Udini hivyo kuwafanya hata wao wajione wadini - Sijui kama umenipata!

Nitakwambia kitu kimoja, majuzi Dr. Slaa alivaa kibaraghashia akiwa Zanzibar, hilo ni vazi tu wala halina asili ya Uislaam isipokuwa kwa fikra za kufikirika, lakini wapo watu walijiuliza maswali wengine wakisema anajipendekeza kwa Waislaam na wengine wakizua kila aina ya maneno hali hilo ni vazi la kiasili la visiwa hivyo na Pwani (utumwa -Oman) kama ilivyo hizi suti na mashati meupe. Na hakika Dr. Slaa pasipo kusema hata neno tayari sisi tumekwisha rushiana maneno lakini akija Harper wa Canada na akavaa kofia hiyo hiyo hatutaona wala kusema tofauti hizo.
Hii kitu Udini imepandikizwa akilini mwetu na kuikubali kuwepo ni kuendelea kutukuza fikra za kitumwa -Insecure..
Mtanisamehe lakini!
 

Jamani hebu angalieni Safu ya viti maalum ya Chadema ile iliyopita na hii ya sasa imatawaliwa na Ukristu na Ukanda (zaidi ya 85% wanatoka kaskazini)
 


Swadakta hakika Chadema hii imepata na ipo chini ya kivuli cha Kanisa ndio maana inapepea kwa kasi sana. Vile vile Chadema inatafunwa na Ukabila yaani ni chama cha Ukanda (Ukaskazini)
 
Sidhani kama wa Tanzania wata tradeoff our security kumruhusu Padre Slaa aongoze nchi hii secular na yenye amani, anatakiwa aonyesha kama anaweza kuiongoza chadema kuondoa udini na ukabila

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…